Mjasiri na Mali
JF-Expert Member
- Jun 24, 2017
- 5,365
- 14,184
Atubu
Sheria zipi ndugu yangu labda atumie maguvu ya Afande Zirro.Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
=UlofaUnamkosoaje Raisi yeye ndio Baba mwenye nyumba. Wewe mtoto Unamkosoaje baba. Acheni Upumbavu na Urofa jamani.
..angeshughulika na mafisadi na wazembe hakuna mtu angekuwa anamlaumu.
..badala yake anatumia muda mwingi na nguvu kubwa zaidi kuwakandamiza na kuwahujumu wapinzani kana kwamba wao ndiyo waliosababisha matatizo[uzembe, ufisadi,..] ya nchi hii.
..Binafsi tangu akiwa Waziri kutokana na matamshi aliyokuwa akiyatoa nilimuona kama mtu asiyeamini ktk demokrasi ya vyama vingi. pia ni mtu asiyeweza kujibu hoja za mwenzake bila kujaribu kumchafua, kumkejeli, au kupotosha hoja.
Yaani utoe maelezo kutokana na mahubiri uliyotoa kanisani kuhusiana na uongozi,hii ni.kujengea watu woga na mbaya zaidi wanaopewa maelezo niweupe hakuna kitu kabisa.Vijana wa kitanzania bwana; tumejivika akili ya kutoelewa. Nani alikuambiwa atakamatwa. Kwanza kwenda kutoa maelezo ya kauli ulizozitoa ni kukamatwa. Mbona ni jambo la kawaida. Lowasa alienda kutoa maelezo juu ya kauli yake; Katibu wa chadema alienda kutoa maelezo juu ya kauli aliyoitoa. Je hili ni geni?. lazima ifikie wakati mtoke katika hayo matongotongo mliyojivika na mje na ajenda zenye tija.
Wewe umemkosoa Huyo jamaa kwa staha na umeeleweka.Hivi umejaribu kupitia wengine jinsi walivyomkosoa?Ulichokifanya ww ndio maana halisi ya ukosoaji.Wenzio huko juu wameishia kutukana na kejeli kibao.Hivi kukosoa ni lzm utumie lugha yenye kudhslilisha?Mbona ww umekosoa bila matusi?Nani wa kulaumiwa ?
Nchi nyingi za kiafrika mamlaka yote yanawekwa kwa mtu mmoja matokeo yake kila eneo linapwaya.
Nchi za afrika zina ukabila, uchama, harufu ya udini udini,ufisadi,wizi, unafiki,uongo, woga, migogoro ya ardhi, wafanyabiashara kukosa kifumo bora ya kuwapa motisha ili biashara zao zikue na kuongeza ajira kwenye jamii, wakulima kukosa masoko na kuporomoka kwa maadili kwa ngazi zote kuanzia juu mpka chini.
Yote hayo yanatokea wakati mamlaka yote yako chini ya mtu mmoja.
Wale wanotawala hawataki kabisa kusikia wakikosolewa kuhusu mifumo hii tuliyoirithi kwa wakoloni waliokuja kutukandamiza kwa manufaa yao.
Sasa tunaposema kuwa watu wakosoe kwa staha tuna maanisha nini bila kuwa na mifumo thabiti ya kusimamia maadili ya viongozi?
Pawe na mifumo isiyopendelea ya kusimamia tamaduni zetu ,mila zetu, heshima kwa jamii. Umoja wetu, amani yetu utaifa wetu kwa vitendo na sio kuigiza kwa malengo ya kisiasa. Maadili liwe ni suala la kisheria na sio anavyoona mtu.
Huku Afrika kiongozi anaweza hata akachukua mke wa mtu halafu mwenye mke akadhibitiwa na asipate hata pa kulalamikia na akibisha basi anafichwa. Wakijitokeza watu kupinga wanaitwa wachochezi na wasio na staha kwa viongozi bila kujua kuwa maadili yalitakiwa yawepo kwa wote kwanza ili jamii istarabike.
Tuweke sheria bora ya kusimamia maadili bora kwa watanzania wote.
Madaraka yasibaki kwa mtu mmoja kwenye usimamizi wa kila kitu matokeo yake hata wale wanaomuunga mkono watajiona kama miungu watu wanaoweza kufanya jambo lolote bila kuulizwa.
Ndio maana tunaina tume ya uchaguzi kupitia wakurugenzi hawafanyi kazi tena kwa mujibu wa sheria za uchaguzi bali kwa matakwa yao ninafsi na kulinda uteuzi wao.
Nani wa kusikiliza kilio cha wale wasio wa upande wa chama tawala endapo kila wanapoenda pameegemea upande wa mwenye madaraka yote ambaye naye ameegemea chama chake?
Tujitathmini kwanza kama tumeweka mazingira ya kupata staha?
Na hiyo staha iwe kwa watawala tu au hata wananchi wa kawaida nao wanapaswa kuheshimiwa kama binadamu?
sijawahi kusikia popote Rais kukataza kukosolewa.
Kinachotokea ni baadhi ya watu kutumia vibaya uhuru walio nao kupotosha kwa malengo binafsi ya kisiasa.
Mara kadhaa Rais amekuwa akionesha kusikitishwa na aina hii ya watu/aina ya siasa wanayoifanya.
Wewe umemkosoa Huyo jamaa kwa staha na umeeleweka.Hivi umejaribu kupitia wengine jinsi walivyomkosoa?Ulichokifanya ww ndio maana halisi ya ukosoaji.Wenzio huko juu wameishia kutukana na kejeli kibao.Hivi kukosoa ni lzm utumie lugha yenye kudhslilisha?Mbona ww umekosoa bila matusi?
Kiujumla hatuna wakosoaji,tuna watoa matusi,kejeli,wadhalilishaji nk na hawa wote wanajificha chini ya mwamvuli wa KUKOSOA.
Ebu lete mifano hiyo ya jamaa kutokuwa na staha.Sipingi unachosema wala unachotetea, ila ukiaangalia huyu anayekosolewa hana lugha za staha, na tatizo hili halijaanza jana wala leo. Hii ni tabia aliyokuwa nayo miaka yote, ila kwakuwa kulikuwa na wengine juu yake, hiyo tabia yake ilijificha. Sasa yeye ndio yuko juu, hivyo chochote anachofanya kinaoonekana zaidi. Nisikufiche wala kuuma maneno jamaa mwenyewe hana staha, sema ni ile kuna msemo usemao mtenda akitendewa hujihisi kaonewa. Hapo kinachomlinda ni nafasi yake na sio tabia yake.
Mapenzi hupofushaEbu lete mifano hiyo ya jamaa kutokuwa na staha.
Mkuu Mimi si muumimini wa ulipotupo na sio kibendera.Napenda kujadili vitu kwa fact sio kubwata ovyo.Kwanini usilete hizo kauli zisizo za stahaMapenzi hupofusha
Ebu lete mifano hiyo ya jamaa kutokuwa na staha.
gu dunia hii tunapita uungu watu utaishia hapahapa duniani,haya yote ni ubatili mtupuRais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Kuita watu wapumbavu na wajinga ni kauli za staha? Ama unataka uwekewe video clip kabisa? Akisema mawaziri wake ni wajinga?! Ama alipowaita wake walienda kuhonga, halafu hawakutokea, kisha akawaita “wapumbavu kabisa”. Mimi wala siyo big deal, lakini unataka ushahidi. Na yeye shida yake akiitwa hivyohivyo anavyoita wengine anachukia.Mkuu Mimi si muumimini wa ulipotupo na sio kibendera.Napenda kujadili vitu kwa fact sio kubwata ovyo.Kwanini usilete hizo kauli zisizo za staha
Hahahahah mkuu,kajipange upya urudi kama ndo unataka kusimamia humu.Sorry lkn,hakuna hoja ya mcng hapo.Nikusomeshe bure upate mimba bure, ukipata mimba ni mwiko kwenye utawala wangu kurudi shule. Sasa angalia ilani ya chama chake inasemaje kwa mwanafunzi akipata mimba.
Heshima, Comrade.
Kukata mti ni kung'oa mzizi na siyo kuchanja matawi. Kuzuia kujikwaa ni kung'oa kisiki na siyo kufukia na kusawazisha ardhi ya ulikojikwaa.
Rais ni zao la Jamii ya Kitanzania. Hajatokea Peponi wala kusikojulikana. Katokea katika Jamii hiihii isopenda kukosolewa. Hivi ni Mtanzania gani/yupi ukimkosoa kwa mantiki hang'aki na kukunja ndita?.
Kuanzia ndani ya Familia, ikiongozwa na asasi iitwayo baba. Je baba anakosolewa?. Tumekwenda mbali mpaka tumejiumbia semi za hovyo "Mkubwa hakosei". Unategemea nini?.
Shuleni, hosipitalini, katika nyumba za Ibada, katika vyombo vya usafiri hakuna anayetaka kubishana kimantiki. Ukimkosoa anakuundia tume. Na mwisho mnaishia kubaya.
Binafsi sidhani kama kumshutumu Rais ni sahihi ilhali ni zao la Jamii yetu. Huu utamaduni tumeujenga kuanzia karne na karne. Tusing'ake, tuukubali na tuurekebishe kwa kuanzia kwenye misingi.
Tukate mti kwa kungoa mzizi na siyo tuchanje matawi. Tungoe kisiki na siyo kufukia ardhi ya tulikojikwaa.
Ebu lete mifano hiyo ya jamaa kutokuwa na staha.
Aliwaita ktk mazingira gani?Tuseme yyt Yale je aliwaita akina nani?Na wanaoreact ni akina nani?Kuita watu wapumbavu na wajinga ni kauli za staha? Mimi wala siyo big deal, lakini unataka ushahidi. Na yeye shida yake akiitwa hivyohivyo anavyoita wengine anachukia.