Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.
Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.
Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.
Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.
Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.
Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?
Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.
Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?
Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.
Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.
Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.
Wewe hua nakukubali sana mana unapiga kote kote bila kujali chama.
Wapinzani wakija vibaya unawanyuka tu. CCM wakija vibaya unawapa za pua.
Huu ndio uzalendo wa kweli.
Mzalendo anasimamia ukweli hata kama unahusu chama chake.
CCM inataka kupata uhai na nguvu mpya kwa kuangamiza Taifa.
Kwa nchi zetu zisizo na mgombea binafsi mambo ya vyama yanatugharimu sana na ndiyo yanayoharibu nchi zetu.
Muda wote watu wanakua kwenye siasa na kampeni za ajabu ajabu.
Ukiangalia wizi na ufisadi mkubwa ulikuwa unafanywa kwa makusudi kati ya viongozi na wafanya biashara kwa lengo la kuimarisha chama ili kishinde chaguzi.
Sasa hayo yamepungua yamekuja mengine ya kufanya kila ulaghai na vikao vya chama mpaka ndani ya majengo matakatifu ya ikulu na kwenye shughuli za kijeshi kupambwa na mapambo na kampeni za chama. Wizi wa kura ,matumizi mabaya ya madaraka kwa wasimamizi wa chaguzi hasa wakurugenzi kuonyesha wazi kuwa wapo kwa ajili ya chama cha mapinduzi huku wakilipwa kwa kodi ya watanzania wote.
Haya yote yanalenga jambo moja tu kushinda uchaguzi.
Kampeni haziishi kwa serikali na chama tawala kwa hofu ya kushindwa.
Tunashindwa kukaa kama taifa moja na kuweka mjadala mpana wa namna ya kujenga nchi yetu tutakao warithisha watoto na wajukuu zetu badala yake watu wanawaza kujenga Chama kwa gharama yoyote.
Hata kama taifa linagwanyika lakini watu hawana habari alimradi chama kinajiinua na kuwa juu ya vyama vingine na sasa kwa mtizamo wa UVCCM wanataka wawe mpaka juu ya vyombo vya dola.
Ni bora sasa pawe na mgombea binafsi ili Baada ya uchaguzi wale wote wanaoshinda kupitia vyama vyote wawe na jambo moja tu la kusimamia na kutekeleza ahadi zao huku wakilinda katiba ya nchi kupitia kiapo walichoapa kwa imani zao.
Uchaguzi uliisha tangu mwaka 2015 lakini watu ni siasa tu na kupanga mikakati ya kuumizana badala ya kusaidiana na kuinuana kiuchumi.
Yana nchi inakua kama ina laana ya umaskini kumbe tatizo ni viongozi kukesha wakiwa wanawaza vyama vyao tu badala ya Taifa.
Mtu anasema kuwa wapigeni mana vyombo vya dola viko chini ya chama chetu.
Huu ni ujinga wa kupitiliza.
Bila kuyaacha haya mavyama yajiendeshe na kujipata uhai kwa sera na hoja tutajikuta siku moja tukiingia kwenye migogoro ya kiitikadi kwa maslahi ya wale wenye madaraka mana kupitia vyama ndipo wanapopata madaraka na maisha bora.
Tukiwa na wagombea binafsi watu watajitoa kutumikia Taifa na sio vikundi vinavyoitwa vyama.
Chama kitakua kinatoa ushauri tu kwa serikali na sio kuipa serikali maagizo amabayo mara nyingi ni ya kuwaumiza wale wanaokosoa mawazo na sera zao.
Tunaumizana kwa mambo ya kijinga kwa faida ya wachache wanaotaka kutawala muda wote bila kupingwa na wengine.