Kama Hayati Magufuli alikuwa anaipeleka nchi shimoni tujuzwe. Watendaji wengi aliowafurumusha wamerejeshwa huku wake wakifurumushwa

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Watendaji wengi ambao hayati Magufuli alikuwa akiamka ama usiku wa manane akiwafurumusha hatimaye wengi wanarejeshwa kwa kasi tena wakipanda vyeo maradufu. Kwa uchache

1. Lawrence Mafuru alifurumushwa kutoka msajili hazina kwa kupinga kuwa hakuna mkurugenzi anayelipwa milioni 15. Leo amepandishwa cheo hadi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambayo hazina ipo chini yake.

2. Felschemi Mramba alifurumushwa kutoka ukurugenzi mkuu wa Tanesco leo ni katibu mkuu nishati ambayo Tanesco ipo chini yake.

3. Nape Mosses Nnauye alifurumushwa kutoka waziri wa habari na michezo. Leo kateuliwa kwenye nafasi ile ile.

Pia wapo watu wa karibu sana na hayati ambao walikuwa wakiaminika naye sana na walipewa kipaumbele huku tukiaminishwa kuwa upigaji umetokomezwa serikalini na kila fedha sasa inaenda sehemu sahihi. Cha ajabu mwaka mmoja baada ya Magufuli kufariki watu hao wamefurumushwa kwa kasi ya ajabu.

1. Uongozi wote wa wizara ya nishati na Tanesco uliokuwa umesimikwa na hayati umeondolewa na sasa wamerejeshwa wale waliokuwa wakiongoza hapo kabla. Nini tatizo?

2. Ndugu wa karibu wa hayati bwana Dotto James aliyekuwa hazina hapo kabla alihamishwa kwenda viwanda na biashara na sasa amefurumushwa kabisa. Nini tatizo?

3. Mawaziri pendwa wa hayati kina Kabudi, Kitila, Lukuvi wamefurumushwa. Hata waliobaki ni kama hawana amani.

4. Chawa wote wa hayati kwa sasa wameufyata kweli kweli kuanzia mitaani, kwenye media mpaka maofisini. Kwa ufupi ni kuwa wazee wa kutetea legacy wamepigwa ganzi vibaya mno.

Mradi pendwa wa hayati wa bwawa la umeme alilolipa jina la Nyerere unaenda kwa kusua sua mno na ni kama January Makamba hana mzuka nao. Hauongelei na wala haupi kipaumbele.

Vitambulisho vya machinga hatimaye vimezikwa na hakuna anayejishughulisha navyo tena.

Cha ajabu wakati anatumbua na kufanya haya yote msaidizi wake mkuu alikuwepo na huyo msaidizi alipochukua tu hatamu ameyabadilisha kwa kasi ya ajabu! Lipo tatizo tena kubwa. Sasa kuliko kuficha ficha moto kwa blanketi ni bora tukaambiwa mapema ikiwa hayati alibugi pakubwa.
 
Mafuru kilichomponza ni kusema ukweli clouds TV kuwa mzunguko wa fedha umepungua mtaani!
Na huko Tanesco ni nini kilitokea mpaka uongozi wote kuanzia waziri hadi watendaji ukaondolewa? Mbona huko ndiko tunakoambiwa kuwa kulikuwa na mafanikio tele?
 
Jamaa walikua wanaringa na madharau mazito mazito.
Ndio maana Msukuma aliwa suck out ili kuwaonesha kuwa wao sio ishu yani japo wazazi wao walikuwa kwenye system. Yani akili zao zilikuwa zile zile kama za watoto wa line police kufanya uhalifu na kujificha kwenye migongo ya baba zao.

Sasa zile hasira za kutupwa nje ndio iliwauma na mbaya zaidi walikuwa hawana la kufanya maana hata watetezi wao (washua) pia walikuwa wanapewa za uso kila wakienda kupenyeza vimemo.

Sasa ndio wana ahueni walau wamerudishwa kwenye system maana Meko angekuwepo still wangekuwa wanatubu mpaka sahizi. Kuondoka kwake ulimwenguni ndio chance yao kutamba. Maana wamepata mbeleko ya binti wa kikojani 😅!
 
Watendaji wengi ambao hayati Magufuli alikuwa akiamka ama usiku wa manane akiwafurumusha hatimaye wengi wanarejeshwa kwa kasi tena wakipanda vyeo maradufu. Kwa uchache

1. Lawrence Mafuru alifurumushwa kutoka msajili hazina kwa kupinga kuwa hakuna mkurugenzi anayelipwa milioni 15. Leo amepandishwa cheo hadi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambayo hazina ipo chini yake.

2. Felschemi Mramba alifurumushwa kutoka ukurugenzi mkuu wa Tanesco leo ni katibu mkuu nishati ambayo Tanesco ipo chini yake.

3. Nape Mosses Nnauye alifurumushwa kutoka waziri wa habari na michezo. Leo kateuliwa kwenye nafasi ile ile.

Pia wapo watu wa karibu sana na hayati ambao walikuwa wakiaminika naye sana na walipewa kipaumbele huku tukiaminishwa kuwa upigaji umetokomezwa serikalini na kila fedha sasa inaenda sehemu sahihi. Cha ajabu mwaka mmoja baada ya Magufuli kufariki watu hao wamefurumushwa kwa kasi ya ajabu.

1. Uongozi wote wa wizara ya nishati na Tanesco uliokuwa umesimikwa na hayati umeondolewa na sasa wamerejeshwa wale waliokuwa wakiongoza hapo kabla. Nini tatizo?

2. Ndugu wa karibu wa hayati bwana Dotto James aliyekuwa hazina hapo kabla alihamishwa kwenda viwanda na biashara na sasa amefurumushwa kabisa. Nini tatizo?

3. Mawaziri pendwa wa hayati kina Kabudi, Kitila, Lukuvi wamefurumushwa. Hata waliobaki ni kama hawana amani.

4. Chawa wote wa hayati kwa sasa wameufyata kweli kweli kuanzia mitaani, kwenye media mpaka maofisini. Kwa ufupi ni kuwa wazee wa kutetea legacy wamepigwa ganzi vibaya mno.

Mradi pendwa wa hayati wa bwawa la umeme alilolipa jina la Nyerere unaenda kwa kusua sua mno na ni kama January Makamba hana mzuka nao. Hauongelei na wala haupi kipaumbele.

Vitambulisho vya machinga hatimaye vimezikwa na hakuna anayejishughulisha navyo tena.

Cha ajabu wakati anatumbua na kufanya haya yote msaidizi wake mkuu alikuwepo na huyo msaidizi alipochukua tu hatamu ameyabadilisha kwa kasi ya ajabu! Lipo tatizo tena kubwa. Sasa kuliko kuficha ficha moto kwa blanketi ni bora tukaambiwa mapema ikiwa hayati alibugi pakubwa.

Mabadiliko ya kufurmushwa yanayotokea utafikiri nchi kaingia mpinzani chama wa chama kipya
 
Hao ndio ccm kindakindaki ,baba zao na babu zao walivuja jasho na damu kupigania ccm ,lazima watoto wao wafaidi ....

Wakati baba zao wanapigania chama ,baba yako alikuwa busy na Mambo yake ndio maana hutambuliwi kwenye mfumo

Magu alivoingia akaanza kuweka mamuruki ambao hawajui hata historia ya ccm ,mbaya zaidi hao mamruki wakawa wanawavimbia wazee wa chamaa ,kinana ,membe ,kikwete ....

Unategemea Nini kingetokea ,baada ya kuona wazee waliopigania chama wanaonewa na mamruki tu wa kawaida ,Sasa wenye chama wanarudi na hapo ikulu watakaa watoto wa wazee waliovujaa damu kupigania chama ....

Kama unaona hupendezwi na safu ya mawaziri hapo juu mlaumu baba yako kwanini hakutengeneza jina lake huko juu .....

Lazima nchi iendeshwe kwa misingi ya wazee wetu na hakuna mamruki yeyote atakayeleta ujinga wake akaishiii ....

Over
 
Na huko Tanesco ni nini kilitokea mpaka uongozi wote kuanzia waziri hadi watendaji ukaondolewa? Mbona huko ndiko tunakoambiwa kuwa kulikuwa na mafanikio tele?
Bana all in all mimi tu nina furaha sana, watu tuliishi kwa hofu, kutishana kila siku kama tupo vitani,, wakati maisha ni haya haya tu, maisha yetu mafupi tu kwann tutishane na tuache kufurahia? Hata kama naishi kwa kunywa uji tu na familia yangu ndani nalala kwa amani, poa sana

Me nachoelewa hii nchi watu asilimia kubwa wana furaha!! Wanaolalamika wengi ni wale chawa wa mwendazake waliokuwa wanafurahia watu kuteswa, kuumizwa na kupotezwa!!

Ila Karma is a bitch!! Wengi wao Mungu kashawalila sawa sawa na matendo yao!! Bado mmoja aliyekuwa anajiita mungu dar es salaam🤣🤣🤣🤣
 
Watendaji wengi ambao hayati Magufuli alikuwa akiamka ama usiku wa manane akiwafurumusha hatimaye wengi wanarejeshwa kwa kasi tena wakipanda vyeo maradufu. Kwa uchache

1. Lawrence Mafuru alifurumushwa kutoka msajili hazina kwa kupinga kuwa hakuna mkurugenzi anayelipwa milioni 15. Leo amepandishwa cheo hadi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambayo hazina ipo chini yake.

2. Felschemi Mramba alifurumushwa kutoka ukurugenzi mkuu wa Tanesco leo ni katibu mkuu nishati ambayo Tanesco ipo chini yake.

3. Nape Mosses Nnauye alifurumushwa kutoka waziri wa habari na michezo. Leo kateuliwa kwenye nafasi ile ile.

Pia wapo watu wa karibu sana na hayati ambao walikuwa wakiaminika naye sana na walipewa kipaumbele huku tukiaminishwa kuwa upigaji umetokomezwa serikalini na kila fedha sasa inaenda sehemu sahihi. Cha ajabu mwaka mmoja baada ya Magufuli kufariki watu hao wamefurumushwa kwa kasi ya ajabu.

1. Uongozi wote wa wizara ya nishati na Tanesco uliokuwa umesimikwa na hayati umeondolewa na sasa wamerejeshwa wale waliokuwa wakiongoza hapo kabla. Nini tatizo?

2. Ndugu wa karibu wa hayati bwana Dotto James aliyekuwa hazina hapo kabla alihamishwa kwenda viwanda na biashara na sasa amefurumushwa kabisa. Nini tatizo?

3. Mawaziri pendwa wa hayati kina Kabudi, Kitila, Lukuvi wamefurumushwa. Hata waliobaki ni kama hawana amani.

4. Chawa wote wa hayati kwa sasa wameufyata kweli kweli kuanzia mitaani, kwenye media mpaka maofisini. Kwa ufupi ni kuwa wazee wa kutetea legacy wamepigwa ganzi vibaya mno.

Mradi pendwa wa hayati wa bwawa la umeme alilolipa jina la Nyerere unaenda kwa kusua sua mno na ni kama January Makamba hana mzuka nao. Hauongelei na wala haupi kipaumbele.

Vitambulisho vya machinga hatimaye vimezikwa na hakuna anayejishughulisha navyo tena.

Cha ajabu wakati anatumbua na kufanya haya yote msaidizi wake mkuu alikuwepo na huyo msaidizi alipochukua tu hatamu ameyabadilisha kwa kasi ya ajabu! Lipo tatizo tena kubwa. Sasa kuliko kuficha ficha moto kwa blanketi ni bora tukaambiwa mapema ikiwa hayati alibugi pakubwa.
Kumbe JPM ulikuwa unamkubali.
 
Hivi lazima turudishe walewale kama vile Tanzania hatuna wataalamu
Tunateua kwa kuangalia 'inner circle' muhimu unafahamika na nani?....hayo ya utaalamu hatujafika huko bado.
 
Back
Top Bottom