Kaka unapooa mrembo kubaliana na haya

Kaka unapooa mrembo kubaliana na haya

Siyo swala la kazi zote za ndani mkuu ishu ni kwamba uwe na mke ambaye ni msafi wa asili siyo kubumba owa wewe mwenye kucha za kubandika, kope za kubandika, Wigi au aliyefuga kucha alafu uwe na mtoto mdogo ndani utamkumbuka mtoa mada.
Huyo hajaoa bado ht usihangaike..ikifika wkt anataka oa .atajua
 
Mi nataka mwanamke mwenye akili ya kutafuta hela.

Hata asipopika au kufua sawa tu.

Yeye sio hausgel au mfanyakazi, ni msaidizi na mke wangu.

Hausgel atafanya hayo.
 
Sasa huyo ni MKE au mfanyakazi wa nyumbani?Mambo ya MKEO ndiyo awe anapika na kufua ni MAMBO ya zanani sana mkuu!Mke ni mshauri wangu mkuu pia ni mtu wangu wa karibu kimwili na kiroho!

Mke wangu kupika ni weekends tu tukiwa home tena anapika chakula chetu tu!Tuache haya mambo kugeuza mke kama mfanyakazi!!Chakula cha watu wote hapa kwangu wapo wanaopika sio WIFE
Nini maana ya Msaidizi? Kama hata kukutengenezea chai hawezi je anakusaidia nini? Uchi tu?
 
I'm one up on you hommie.

Me and my [imaginary] wife cook together😉.

And I can vouch to you that that is one of the most romantic things you and your better half can do.

I mean, what's more romantic than cooking dinner together at home and eat it under candlelight.....?

Marriage is a two-way street. In order for it to be successful, a lot of give-and-take is required from both husband and wife.

The synergistic effect of working together as a tag team just can't be beat.

I can't be an arrogant and domineering husband. My [imaginary] wife is my life partner. Not my maid.
This is so sweet..lakini huku mwishoni kumbe ni imaginary wife tena...
 
Vijana wenzangu unapoamua kuoa mrembo, msomi na binti wa digital, lazima ukubaliane na haya;

1. Wasichana wengi sasa hawajui kupika. Wanajifanya wamechoka nitanunua msosi sana tu, tena usipokaza hata chai ataenda kununua.

2. Usishangae nguo zako kutofuliwa wiki mbili, anaweza kumuita mdogo ake anamlipa afue. Yeye anachart sio na wewe ujue ni shotizooo.

3. Kupiga deki sahau kijana mwenzangu. Aanze tu kupinda mgongo. Kama unataka usafi wa nyumba yako tafuta housegirl.

4. Jua kuwa utawahi wewe kuamka, yeye bado kalala. Amechoka kazi za ofisini za jana yake.

5. Bajet ya saloon iwepo ya kila wiki nywele na kucha.
U have spoken something you are experiencing recently,sio wote wapo hivyo its hast generalization fallacy
 
Issue ya kuoa inahitaji kutulia sana waweza angukia pua,kule usukumani kuchapakazi huongeza credit kwa binti ili aweze kuolewa.Ni kweli maisha yamechange lkn kazi za kupika,kufua pamoja usafi wa nyumba ni kazi za mwanamke haijalishi kama ni mwajiriwa au mama wa nyumbani.Haya maisha ya kisasa hayapaswi kuendekezwa,Nilikua na gf wangu cha kushangaza alikua akinikuta nafua ama nafanya usafi hakuweza kunisaidia yeye alitaka tu hela ya saloon na kuelekea out, uzalendo ulinishinda nikajiweka kando .
 
Ila labda tuseme kitu kimoja hivi unapokwenda kuoa mwanamke wa jinsi hiyo unataraji nini.

Ila mimi msimamo wangu bado upo pale pale usioe mwanamke ili awe mfanyakazi mwanamke ni pambo la ndani.

Hivi unaona tabu gani wewe ukimfulia nguo zake na ukafangia ndani hivi kuna sheria gani ambayo inaeleza kwamba mwanamke afanye kazi zote hizo.
Pambo la ndani ndiyo liwe chafu
 
Nini maana ya Msaidizi? Kama hata kukutengenezea chai hawezi je anakusaidia nini? Uchi tu?
Huyo jamaa hazimtoshi eti anapika chakula chao tuu kwa hiyo dada yeye ale kwa jirani ua alale njaa acheni hizo chakula cha familia kinaliwa na wote chenu. Ni tendo la ndoa tuu.
 
kazi ipo tena si ndogo. Wanaume mpooooooooo?
 
Nini maana ya Msaidizi? Kama hata kukutengenezea chai hawezi je anakusaidia nini? Uchi tu?
Kazi namba moja ya mke ni kutengenwza familia na ushauri ndani ya ndoa!Haiwezekani umchukie mke wako sababu hapiki chakula wala hafui

Ndoa za zamani sana hizi,ndoa za babu zetu
 
Kazi namba moja ya mke ni kutengenwza familia na ushauri ndani ya ndoa!Haiwezekani umchukie mke wako sababu hapiki chakula wala hafui

Ndoa za zamani sana hizi,ndoa za babu zetu
Kutengeneza familia na kutoa ushauri sio usaidizi? Kwanini asikusaidie na hilo la kupika?

Kwahiyo ndoa za sasa ni bora kuliko za wakati wa mababu zetu kutokana na changes hizo?
 
Kutengeneza familia na kutoa ushauri sio usaidizi? Kwanini asikusaidie na hilo la kupika?

Kwahiyo ndoa za sasa ni bora kuliko za wakati wa mababu zetu kutokana na changes hizo?
Ni usaidizi halali huo na akishindwa kutimiza haya ni halali kuachana LKN siwezi muacha mke sababu hajapika supu!

Kwa mawazo yangu ndoa za.zamani zilikuwa za mfumo dume mno na ni jukumu langu mm na ww kuyakataa haya mambo!Kyela mme anaoa Wanawake wengi ili wawe wanamtunza
 
Ni usaidizi halali huo na akishindwa kutimiza haya ni halali kuachana LKN siwezi muacha mke sababu hajapika supu!

Kwa mawazo yangu ndoa za zamani zilikuwa za mfumo dume mno na ni jukumu langu mm na ww kuyakataa haya mambo!Kyela mme anaoa Wanawake wengi ili wawe wanamtunza
Mkuu hilo la kuoa wake wengi ili kutunzwa achana nalo linahitaji mada yake special....

Swali langu ni kwanini hizo ndoa za mababu unazoita za mfumo dume ndizo zilizodumu haswa na mpk leo mababu na mabibi zetu wanaishi pamoja? Unajua mikasa ya ndoa za sasa zenye lifestyle unayoisupport.
 
Back
Top Bottom