Kaka unapooa mrembo kubaliana na haya

zegamba180

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
818
536
Vijana wenzangu unapoamua kuoa mrembo, msomi na binti wa digital, lazima ukubaliane na haya;

1. Wasichana wengi sasa hawajui kupika. Wanajifanya wamechoka nitanunua msosi sana tu, tena usipokaza hata chai ataenda kununua.

2. Usishangae nguo zako kutofuliwa wiki mbili, anaweza kumuita mdogo ake anamlipa afue. Yeye anachart sio na wewe ujue ni shotizooo.

3. Kupiga deki sahau kijana mwenzangu. Aanze tu kupinda mgongo. Kama unataka usafi wa nyumba yako tafuta housegirl.

4. Jua kuwa utawahi wewe kuamka, yeye bado kalala. Amechoka kazi za ofisini za jana yake.

5. Bajet ya saloon iwepo ya kila wiki nywele na kucha.
 
Hahaha hao ni wale wanawake mnaaoa mmekutana club...
Mpk unaoa ulikua hujui km hajui kazi...kabla hujaoa msome..mlete ghetto uone anachofanya..
By the way wako warembo ambao kazi zooteee tunajua..km unabisha njoo umuulize mme wangu....lol
 
Unaweka mgomo baridi, usitoe hela ya matumizi, nyasi za chooni zikianza kuota tu mbona atajirekebisha. Tabia zingine chanzo ni mwanaume mzembe.
 
Unapooa mke mwenye sura kama anakamuliwa jipu kumbuka kuna outings za maana
angalia nafasi hiyo ikachukuliwa na michepuko
ulichosema hapo n fact ila kama wazur tuu ndo waolewe wabaya watabak na nana by the way wabaya hao ukimwoa anakuzalia matoto ya maana kinyama (ie, vivwanda vyao vya kutengeneza watoto viko sawa sana).
 
Dah,sasa umenikatisha tamaa mana kuna demu wangu kiukweli ni mrembo ila tabia zake akija maskani ni mvivu cjapata kuona.
 
Dah,sasa umenikatisha tamaa mana kuna demu wangu kiukweli ni mrembo ila tabia zake akija maskani ni mvivu cjapata kuona.
Cmp sikukatishi tamaa nimeamua kuwaambia ukweli vijana wenzangu mjue. Hili jambo aliwekwi wazi. Ukweli ndo huo na wewe shahidi. Uamuzi upo mikononi mwako.
 
Mwanamke yeyote anaejiona kuwa ni mrembo, na mwenye kujivunia huo urembo, kazi ama pesa. Si mwanamke sahihi wa kuoa. Kama itabidi kumuoa au ukajikuta umetumbukia katka janga hilo suluhisho ni kukubali muishi kwa kila mmoja kufanya majukumu ya nyumbani pamoja.
Ikiwa ni pamoja na kupanga bajeti ya matumizi likiwemo la saloon, kuweka pamoja mishahara kulea watoto jinsi ya kutoka, kuchelewa kurudi nyumbani. Tatizo kubwa kwa hawa wanawake hawapendi kutulia na mwanaume mmoja, wanajiona wana soko kwa hiyo hawahitaji kuwa chini ya mwanaume hili tatizo si kwa warembo bali kwa kila mwanamke anaye jiona aidha kuwa ni mrembo au mwenye elimu na cheo ama kwa mafanikio kibiashara ni asilimia ndogo sana wanakaa na waume zao kwa amani. Huhesabu ndoa ni utumwa
 
Last edited:
Kosa letu wanaume tunafuata hisia zaidi kuliko akili ktk kupata mke. Kosa la pili, kumpeleka mtarajiwa kwa mama zetu, kama kipimo cha kufanyakazi ni wazi atajitahd kufanyakazi. Chezea ukweni wewe wakati ndoa anataka.
 
suala si binti MREMBO au MSOMI, ukweli uliopo ni kwamba kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha(life style) ,dada zetu BAADHI yao au pengine WENGI WAO hawajui kupika na ni wavivu katika kazi za nyumbani. na hili si kosa lao kutojua kupika ila ni mabadiliko ya mfumo wa maisha. binti anaanza chekechea(baby class) mpaka chuo yupo BWENI tu, na akija likizo anakuwa ametingwa na masomo ya ziada, akirudi nyumbani giza limeingia. Je atajifunza kupika saa ngapi? halafu shule za bweni za siku hizi si kama zile za nyakati zetu ambapo elimu ya kujitegemea(self reliance) ilipewa kipaumbele....ni shule za kusoma madesa tu, nyingine mpaka vitanda wanafunzi wanatandikiwa na kina mama wanaofanya usafi mabwenini. binti anakuwa hajui hata kutandika kitanda.
Pia kuna mabinti hawasomi bweni wako shule za kutwa lakini kwa changamoto ya mji kama Dsm binti anatoka nyumbani saa kumi alfajiri,akitoka shule anapita masomo ya ziada.hiyo ni jioni tayari anakwenda kugombania daladala, akifika nyumbani saa mbili tayari kila kitu kimeshapikwa.
NINI KIFANYIKE. wazazi pamoja na changamoto zilizopo za kimaisha lakini ni LAZIMA wahakikishe mabinti wawapo nyumbani hata kama ni kwa likizo ya wiki moja basi wawe wanawajibika ipasavyo kujua yale yanayowahusu wao kama kina dada. Ni aibu kwa mwanamke kutojua kupika au akawa mvivu kupindukia kwa sababu tu hakuzoea kufanya hizi kazi. kwa upande wa mabinti wenyewe nao wajielewe na wawe na ari ya kujifunza. wakiwa na nia hasa,kupika si kugumu,ni suala tu la kuwa na INTEREST nalo basiiiii!. ikiwa binti hujui kupika na unaridhika kabisa hujui na huoneshi juhudi,je watoto wako watakuwaje? halafu maisha yanabadilika,mabinti wasitegemee kuwa watakuwa na uwezo wa kuwalipa madada wa nyumbani kila siku....kuna wakati maisha yanakuwa magumu na hata hiyo hela ya kumlipa house girl usiipate....things do change!!
 
Back
Top Bottom