Kaini alipata wapi mke wake?

Kaini alipata wapi mke wake?

HOJA YA MSINGI

“Ikiwa Adamu na Hawa walikuwa na wana wawili, Kaini na Abeli, na baadae Seth, Je, mke wa Kaini alitoka wapi?”
Biblia ina habari za kutosha kujibu swali hilo kwa njia inayofaa, na kwenye hii mada tutajibu hili swali linalo wachanga sana watu.
MUKTASARI:
Katika Mwanzo sura ya 3 na ya 4 tunapata habari zifuatazo:

(1) Hawa alikuwa “mama ya kila mtu anayeishi.”

(2) Muda fulani ulipita kuanzia wakati Kaini alipozaliwa mpaka wakati alipotoa dhabihu ambayo ilikataliwa na Mungu.

(3) Baada ya kufukuzwa na kuwa “mwenye kutanga-tanga na mkimbizi,” Kaini alikuwa na wasiwasi kwamba huenda ‘mtu yeyote akakutana naye’ na kujaribu kumuua. [Angalia hoja hapa "Kaini anaogopa kuuwawa na watu wengine"] Hapa panaonyesha kuwa Kaini alikuwa na ndugu wengine.

(4) Mungu aliweka ishara ya kumlinda Kaini, jambo lililoonyesha kwamba ndugu au dada zake, au watu wengine wa ukoo wangejaribu kumuua. Kumbe basi Kaini alikuwa na ndugu wengine zaidi ya Abel na Seth.

(5) “Baadaye” Kaini alilala na mke wake “katika nchi ya Ukimbizi.”—Mwanzo 3:20; 4:3, 12, 14-17.

Naomba majibu tafadhari.
Alimuoa dada yake. Na pia ni mojawapo ya chanzo cha ugomvi na mdogo wake abel. Ilikuwa aolewe na abel lakini kaini akawa anamtaka. Soma apocrypha kitabu cha adam, 1-6
 
HOJA YA MSINGI

“Ikiwa Adamu na Hawa walikuwa na wana wawili, Kaini na Abeli, na baadae Seth, Je, mke wa Kaini alitoka wapi?”
Biblia ina habari za kutosha kujibu swali hilo kwa njia inayofaa, na kwenye hii mada tutajibu hili swali linalo wachanga sana watu.
MUKTASARI:
Katika Mwanzo sura ya 3 na ya 4 tunapata habari zifuatazo:

(1) Hawa alikuwa “mama ya kila mtu anayeishi.”

(2) Muda fulani ulipita kuanzia wakati Kaini alipozaliwa mpaka wakati alipotoa dhabihu ambayo ilikataliwa na Mungu.

(3) Baada ya kufukuzwa na kuwa “mwenye kutanga-tanga na mkimbizi,” Kaini alikuwa na wasiwasi kwamba huenda ‘mtu yeyote akakutana naye’ na kujaribu kumuua. [Angalia hoja hapa "Kaini anaogopa kuuwawa na watu wengine"] Hapa panaonyesha kuwa Kaini alikuwa na ndugu wengine.

(4) Mungu aliweka ishara ya kumlinda Kaini, jambo lililoonyesha kwamba ndugu au dada zake, au watu wengine wa ukoo wangejaribu kumuua. Kumbe basi Kaini alikuwa na ndugu wengine zaidi ya Abel na Seth.

(5) “Baadaye” Kaini alilala na mke wake “katika nchi ya Ukimbizi.”—Mwanzo 3:20; 4:3, 12, 14-17.

Naomba majibu tafadhari.
... sijui lengo lako ni kupotosha au nini kwa sababu Biblia imeeleza vizuri tu. Soma Mwa 5: 1 - 5;

1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.

... kumbe Adam na mkewe walikuwa na wana (wa kike na kiume) zaidi ya Kaini, Abel, na Sethi! Very clear indeed!
 
Hilo ndilo jibu sahihi.

Biblia inaeleza kuhusu uumbaji wa Adam, mtu wa kwanza, na Hawa mkewe aliyetoka ubavuni mwake. Narejea baadhi ya maandiko matakatifu. Kwamba Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi (Mwanzo 1:1).

Baada ya kukamilisha uumbaji huo Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.(Mwanzo 1:26 - 28).

Kutokana makusudi ya uumbaji huo, imeandikwa Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. ((Mwanzo 4:1,2, 25)

Kimsingi Adam na Hawa walizaa watoto wa kiume na kike japo kwenye Biblia wametajwa hao wanaume tu. Kaini na nduguze walioa dada zao kama ambavyo Hawa alivyotolewa kwenye ubavu wa Adam. Imeandikwa Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. (Mwanzo 2:21 - 23)

Hiyo ndio siri ya wake wa watoto wa Adam na Hawa (Kaini, Habili na Sethi), chimbuko la familia za binadamu wa sasa. Kila mtoto wa Adam na Hawa alikwenda kuanzisha Taifa lake (Soma Kitabu Mwanzo, Sura ya 4 na 5, kujua uzao wa Adam na Hawa ambao ndio kizazi cha binadamu kinaendelea), kama ilivyoandikwa Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. (Mwanzo 6:1, 2)
 
Haiwezekani tu watoto wawili, walikuwa na dada yao, na Mungu alihalalisha kaka kuzaa na dada yake.
 
Ikiwa kulikuwa na familia moja tu, Kaini alipata wapi mke wake?

Mwa. 3:20: “Adamu akamwita mke wake jina lake Hawa, kwa sababu ndiye angekuja kuwa mama ya kila mtu anayeishi.” (Kwa hiyo, wanadamu wote wangekuwa wazao wa Adamu na Hawa.)

Mwa. 5:3, 4: “Adamu akaishi miaka 130. Ndipo akazaa mwana kwa mfano wake, kwa sura yake. Akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zikawa miaka 800. Wakati uleule akazaa wana na mabinti.” (Mmoja wa wana wa Adamu alikuwa Kaini, na bila shaka mmoja wa binti za Adamu alikuja kuwa mke wa Kaini. Wakati huo, wanadamu walipokuwa wangali wana afya bora na nguvu kimwili, kama inavyoonyeshwa na urefu wa maisha yao, hapakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwapitishia wazao wao kasoro kwa sababu ya kuoa mtu wa ukoo.

Hata hivyo, baada ya miaka 2,500 hivi ya historia ya wanadamu, wakati hali ya kimwili ya wanadamu ilipokuwa imezorota sana, Yehova aliwapa Waisraeli sheria zilizokataza ngono kati ya watu wa familia moja.)

Mwa. 4:16, 17: “Kaini akaenda zake kutoka usoni pa Yehova na kukaa katika nchi ya Ukimbizi [au, Nodi] upande wa mashariki wa Edeni. Baadaye Kaini akalala na mke wake [“akamjua mkewe,”] naye akapata mimba, akamzaa Enoko.” (Ona kwamba Kaini hakukutana na mke wake katika nchi aliyokimbilia, kana kwamba mke huyo alitoka katika familia nyingine. Badala yake, huko ndiko alipolala na mke wake ili amzalie mwana
Unawezaje kusema Mungu alikataza ngono kwa watu wa familia moja na wakati sisi sote asili yetu ni watoto wa baba na mama mmoja? Maana yake kwa namna moja ama nyingine bado tuna oana watu kutoka asili ya baba na mama mmoja ( Adam na Hawa)
 
Kaini alimwoa dada yake ambae walizaliwa wote(pacha) na mdogo wake Seth akamwoa pacha wa marehemu Abel. Kwa Taarifa ni kwamba Adam alipata watoto watano tu. Wavulana watatu na wasichana wawili. Baada ya Abel kuuawa wakabaki wanne. Kutoka hao wanne ndipo dunia ikajazwa.
Kwahiyo tunakubaliana kimsingi kwamba, Adamu na Hawa walizaa watoto wengine wa kike na hawakua recorded sawa na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati? Right!?
 
Ndugu hizi informations umezitoa wapi?
 
Kwahiyo tunakubaliana kimsingi kwamba, Adamu na Hawa walizaa watoto wengine wa kike na hawakua recorded sawa na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati? Right!?
Ukisoma vizuri kitabu cha mwanzo kimeeleza kuwa Adamu na Eva walipata watoto wakike na kiume., Japo maelezo zaidi ya hao wa kike hayakutolewa hapo.
 
Ndio
Ndio maana hadi leo
Hatuzidishi kuishi zaidi ya miaka 120
Ukivuka hapo huwi Binadamu tena bali Kiumbe tu.
Kutokana na tamko la Mwanzo 6:3
Napata taabu kuamini hili. Maana siku Moja kwa Mungu, ni miaka elfu kwetu huku.
 
Swali:- Wakati Yesu yupo duniani anatoa pepo/majini wachafu, kuna wakati pepo walikuwa wanatamka "Tuna nini nawe mwana wa Mungu?"

Inawezekana Majini/mapepo yameishi hapa duniani kwa miaka mingi sana, sasa kwanini binadamu wasitumie hayo majini kujua ukweli wa dunia hii?

Nasikia kuna watu wanafuga majini basi wafanye hizo tafiti.
Na kuna watu ni watalaam wa kuongea nayo. Si wayaulize, ?
 
Zile ni hadithi tu, usipende kuamini sana vitabu vilivyotungwa na binadamu kusingizia ni vya Mungu, ule ni usanii tu mkuu toka kwa Waroma.
Na kitabu cha Ufunuo ni hadithi tu?
 
... sijui lengo lako ni kupotosha au nini kwa sababu Biblia imeeleza vizuri tu. Soma Mwa 5: 1 - 5;

1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.

... kumbe Adam na mkewe walikuwa na wana (wa kike na kiume) zaidi ya Kaini, Abel, na Sethi! Very clear indeed!
Naomba nikanushe swali langu ni kupata jibu na sio kupotosha
 
Dah iyo mambo mim ndio inanifanyaga nione biblia ni kama chapisho la wagiriki
 
Back
Top Bottom