Hii miaka 900 ya Adam ilikuwa ni hiihii ya mwezi 12, siku 30 kila mwezi au ?
Mwanzo 5:3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
Mwanzo 5:4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Mwanzo 5:6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
Mwanzo 5:7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:8 Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
Mwanzo 5:9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
Mwanzo 5:10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
Mwanzo 5:12 Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
Mwanzo 5:13 Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
Mwanzo 5:15 Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
Mwanzo 5:16 Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
Mwanzo 5:18 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
Mwanzo 5:19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
Mwanzo 5:21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
Mwanzo 5:22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
Mwanzo 5:24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Mwanzo 5:25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
Mwanzo 5:26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
Mwanzo 5:28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
Mwanzo 5:29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.
Mwanzo 5:30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
Mwanzo 5:32 Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.