Kaini alipata wapi mke wake?

Mkuu ni maswali ambayo niliona kupata majibu ya uhakika isingekuwa rahisi maana hata maisha ya Yesu Biblia inaonyesha kuzaliwa, kisha maisha yake akiwa na umri wa miaka 12 kisha maisha yake kuelekea kusulubiwa. Kuna miaka ya katikati ambayo hatukuelezwa alikuwa akiishi vipi na aliyokuwa anayafanya.
Ukitaka kujua haya mambo vizua lazima ujue Adam alitoka wap, na baada ya kuumbwa na kufanya makosa nakuletea dunian,, je, walikuja Kwa pamoja na hawa? Jibu hapa hawakuja pamoja, je, Adam alimtafuta Hawa Kwa miaka mingap mpak kupata? Jibu nimiaka arobain.je Adam aliishi miaka mingapi? Jibu nimiaka 960.

Sasa tuangalie hii miaka 960 katika maisha ya Adam ilikuaje Kuanzia yy na mkewe, walivo Pata Familia. Nakuja,
 
Nahisi Ni kwa sababu biblia inataja vizazi vya watu kwa kupitia watoto wa kiume mfano Ni :Adam kumzaa kain,Abel na Seth so hii haimaanishi kuwa hao waliotajwa ndio peke yao tu walizaliwa na ADAM NA HAWA ukute Kain hata hakuwa wakwanza kuzaliwa kwa Hawa Bali waeza kuta walizaliwa wa kike wengi alafu yeye Ndo akafatia na kwa kuwa biblia kuhesabu watu ilikuwa inahesabu wanaume tu peke yao labda ndio maana
Hoja yako imeeleweka, ila swali jingine linakuja kama walianza kuzaliwa watoto wa kike, au hata kama walizaliwa baadaye, kwa maana hiyo ili kukuza ukoo ilibidi kaka na dada zao walalane ili waweze kutengeneza ukoo?
 
Swala la biblia limekaa kimitego sana..

Majibu mengi ni ya kufikirika... bila reference
 
Nilishwahi uliza swali hili kwa mchungaji wangu mmoja na alinipa majibu haya.

1. Biblia tunayotumia haina rekodi ya kila kitu kilichotokea mwanzo, yaani siyo vyote viliandikwa na inasemekana kuna biblia ambayo ina record ya yote yaliyotokea mwanzo ( binafsi sijawahi kuiona ).

2. Matukio ya kwenye Bible yalikuwa yanaandikwa baada ya kupita muda fulani, yaani utaratibu wa kukusanya mistari ilikuwa ikifanyika ambapo kuna mistari ilibeba rekodi za miaka kadhaa mpaka mstari mwingine kutokea.

Kwa mfano hilo la Kaini, haijulikani ni baada ya miaka mingapi tukio hilo lilitokea na ndani ya huo muda Je, Adam na Hawa hawakufanikiwa kupata watoto wengine ? Ambao nao walitapakaa maeneo tofautitofauti.

3. Kupitia sababu hiyo ya pili ndipo hapo Kaini alipata mke ambaye inaonekana alikuwa ndugu yake either wa damu au alikuwa ndugu yake na ndugu zake wa damu.

Nilimuuliza mchungaji, kwanini sasa kwasasa mtu kumuoa dada yake au ndugu yake ni dhambi ilihali hapo zamani Kaini aliweza kufanya hivyo??

Alinipa jibu hili:

Kwa kipindi kile Mungu aliruhusu iwe hivyo ili watu waendelee kuzaliana na kuijaza dunia hivyo haikuwa dhambi tofauti na inavyotafsirika leo.

Baada ya kunipa ufafanuzi huo nilikuwa na maswali mengi sana ila nilimuaga mchungaji ili nisijeibua maswali yasiyokuwa na majibu
niulize hapa hayo maswali nikujibu mie...

Biblia tunayosoma ni summary tu ya kile alicho fanya Mungu.

Km tungeandika kila kitu Biblia ni kubwaaa mno km ghorofa 16 hivi!!kkm ingeandikwa kila kitu.

Hii. ya leo Ukisoma na vima tumboni kamwe hutaelewa wala usipoteze muda.ni mali ya wateule tu!

Na kweli imeandikwa umo kuwa IMANI SI MALI YA KILA MTU. km huielewi iache!...tu
 
Kuna mahali nilipata kusikia kuwa biblia wakati inaandaliwa iliwalazimu kukusanya vitabu visivyokinzana na kunavitabu vingi tu vilikuwa vinaelezea mambo nyeti ya dola la kirumi na hivyo vilipigwa vita visitumike
 
Sasa kwa nini watupatie biblia ambayo haijakamilika kwa mafundisho yote?
Biblia imekamilika.
Ukweli ni kwamba Mungu hakuandika kila kitu alichokifanya hapa Ulimwenguni.
Mambo mengine alituachia wanadamu tuyagundue kwa akili zetu alizotupatia na alijua tutaendelea kuyagundua.
Ndio maana tafiti za Kisayansi zinaendelea kugundua mambo kadhaa wa kadha.

(Kuku jibu swali lako la Mke wa Kaini)

Ki ushahidi wa Kiteolojia Mwanadamu wa kwanza aliishi Mashariki ya Kati kama sio Iran basi ni Iraq ambapo ndipo kulipokuwa Bustani ya Aden.
Kuna ushahidi wa Mto Tigris ambao unapita huko.

Lakini tafiti za Kiakolojia zinatuambia Mwanadamu wa Kwanza aliisha Tanzania Kondoa Irangi Olduvai Gorge. Kutokana na Ugunduzi wa Dr Leakey.
Hivyo Zinjanthropas anaweza kusemekana kama Binadamu wa Kwanza kutokana na ushahidi wa Kihistoria.

Tunagundua nini hapa.
Bila shaka hapa tunagundua kuwa Mungu, kwanza kabisa aliumba Adam na Eva (Hawa) huko Iraq.
Hao walikuwa race ya ama Kiarabu, Kishirazi, au Kikuresh, yaani moja ya hizo race za Mashariki yakati.
Hapo akatuambia ktk Biblia.

Baada ya hapo Mungu akawaumba Binadamu wengine wawili Mume na Mke ktk Race ya Kiafrika ( weusi )
Weusi akawaweka katika Bonde la Olduvai, ndio Babu zetu sisi blacks.

Akawaumba Wanadamu wawili Mke na Mume Wazungu akawaweka nchi moja huko kwa Wazungu.
Vivyo hivyo kwa Race nyingine za Wahindi, Wachina ambao ni jamii moja na Wakorea, Wajapan Nk.

Wote hao wakazaliana na baadae kuweza kuongezeka na kukutana na kuoleana na race nyingine na kutengeneza watu Chotara.

Hao ndio aliokutana nao Kaini baada ya kuondoka kwao.
Inasadikiwa kuwa Kijakazi wa baba wa Imani Ibrahimu, Hajiri, alikuwa Mwarabu ndio maana akamzalia Ibrahim watoto Maseyidi.
Leo ukienda uarabuni utakuta watu wanajulikana kama Seyidina Abubakar nk.

Kuhitimisha ni kuwa kila Race ilikuwa na Adam na Hawa wao.
Mungu baada ya kuwaumba Adam na Eva. Aliendelewa kuwaumba Wanadamu wawili tena Mume na Mke katika Race nyingine na kuwaweka ktk mabara mengine ndio maana ktk kila bara kuna race flani tofauti na nyingine.

Inasadikiwa Wahindi wekendu waligundulika zamani kabisa huko bara la Amerika, walikutwa wao tu bila mchanganyiko na race
nyingine

Waafrika tulikutwa na watafiti wa kale hapa Afrika.
Mungu hakuwaamuru Manabii waandike ktk Biblia hiyo habari. Aliacha watu kama Dr. Leakey wavumbue.
 
Kwa hapa naomba nieleze na mimi kwa upeo wangu kidogo; ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:26-31 kuna fumbo pale ya kwamba, Mungu alimuumba Mtu yaani mwanamke na mwanamume kwa mfano wa sura yake na akawaamuru wakazaliane na kwenda kuijaza Dunia na akawapa mamlaka ya kuvitawala vyote alivyoviumba.

Ukisoma pia Mwanzo 2:7-8, utagundua ya kwamba, viumbe ambao aliwaumba Mungu kabla walikuwa sio viumbe wa kawaida na ndio maana hapa Mungu anasema, "akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai".

Ukisoma tena Mwanzo 2:18-24, utaona Mungu alivyo muumba mwanamke wa kufanana na Adam kupitia ubavu wake hivyo, katika yote ya yote hayo unapata kuelewa kuwa kulikuwa na uzao mwengine wa Adam ambao ulikuwepo kabla ya kuzaliwa kwa Kaini, Abel na Sethi ambao ulikuwa ni kizazi cha Adam lakini ni kwa mwanamke tofauti na Hawa. Hapa ndipo unapata kufahamu uwepo wa Lilith katika uumbaji wa Mungu, ambaye alizaa na Adam majitu katika nchi nyingine. Kutokana na kwamba Lilith hakupenda kutawaliwa, basi ndio maana Mungu akaamua kumuumba Mwanamke (Hawa) katika ubavu wake iliaweze kufanana nayeye.

Asante!!..
 
Alimuoa dada yake kwa kipindi hicho ilikuwa halali tu ndiyo maana hata Ibrahimu naye alimuoa dafa yake pia, Yakobo na Isaka walioa ndugu zako simply kwa sababu popn haikuwa kubwa sana na wengi walitoka kwa Adam baada ya jamii kupanuka na watu kuongezeka ndiyo hilo Mungu akalikataza
Ni andiko gani linasema Mungu alikataza kuoana ndugu kwa ndugu
 
Alioa toka kwa mijitu au wanefilo au nephilim kwa kimombo kitabu cha mwanzo 6: 4
The Nephilim were on the earth in those days—and also afterward—when the sons of God went to the daughters of humans and had children by them. Hii inaonyesha uongo wa biblia na quran kuwa Adam ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
Inavoonekana duniani kulikua na binadamu wengine ukiacha Adam na hawa
 
Biblia imekamilika.
Ukweli ni kwamba Mungu hakuandika kila kitu alichokifanya hapa Ulimwenguni.
Mambo mengine alituachia wanadamu tuyagundue kwa akili zetu alizotupatia na alijua tutaendelea kuyagundua.
Ndio maana tafiti za Kisayansi zinaendelea kugundua mambo kadhaa wa kadha.

(Kuku jibu swali lako la Mke wa Kaini)

Ki ushahidi wa Kiteolojia Mwanadamu wa kwanza aliishi Mashariki ya Kati kama sio Iran basi ni Iraq ambapo ndipo kulipokuwa Bustani ya Aden.
Kuna ushahidi wa Mto Tigris ambao unapita huko.

Lakini tafiti za Kiakolojia zinatuambia Mwanadamu wa Kwanza aliisha Tanzania Kondoa Irangi Olduvai Gorge. Kutokana na Ugunduzi wa Dr Leakey.
Hivyo Zinjanthropas anaweza kusemekana kama Binadamu wa Kwanza kutokana na ushahidi wa Kihistoria.

Tunagundua nini hapa.
Bila shaka hapa tunagundua kuwa Mungu, kwanza kabisa aliumba Adam na Eva (Hawa) huko Iraq.
Hao walikuwa race ya ama Kiarabu, Kishirazi, au Kikuresh, yaani moja ya hizo race za Mashariki yakati.
Hapo akatuambia ktk Biblia.

Baada ya hapo Mungu akawaumba Binadamu wengine wawili Mume na Mke ktk Race ya Kiafrika ( weusi )
Weusi akawaweka katika Bonde la Olduvai, ndio Babu zetu sisi blacks.

Akawaumba Wanadamu wawili Mke na Mume Wazungu akawaweka nchi moja huko kwa Wazungu.
Vivyo hivyo kwa Race nyingine za Wahindi, Wachina ambao ni jamii moja na Wakorea, Wajapan Nk.

Wote hao wakazaliana na baadae kuweza kuongezeka na kukutana na kuoleana na race nyingine na kutengeneza watu Chotara.

Hao ndio aliokutana nao Kaini baada ya kuondoka kwao.
Inasadikiwa kuwa Kijakazi wa baba wa Imani Ibrahimu, Hajiri, alikuwa Mwarabu ndio maana akamzalia Ibrahim watoto Maseyidi.
Leo ukienda uarabuni utakuta watu wanajulikana kama Seyidina Abubakar nk.

Kuhitimisha ni kuwa kila Race ilikuwa na Adam na Hawa wao.
Mungu baada ya kuwaumba Adam na Eva. Aliendelewa kuwaumba Wanadamu wawili tena Mume na Mke katika Race nyingine na kuwaweka ktk mabara mengine ndio maana ktk kila bara kuna race flani tofauti na nyingine.

Inasadikiwa Wahindi wekendu waligundulika zamani kabisa huko bara la Amerika, walikutwa wao tu bila mchanganyiko na race
nyingine

Waafrika tulikutwa na watafiti wa kale hapa Afrika.
Mungu hakuwaamuru Manabii waandike ktk Biblia hiyo habari. Aliacha watu kama Dr. Leakey wavumbue.

Duh hatari sana hii comment
 
Duh hatari sana hii comment
Ndivyo ilivyo ndugu, Mungu hajazungumza kila kitu kwenye Biblia

Hawa ni Wajukuu wa Hajiri, ambao ni Moja ya jamii ya Kiarabu.

Mwanzo 17:20
Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
Mwanzo 17:21
Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.

Mtafiti Columbus sijui miaka gani, alipounda Merikebu yake na kufanya safari ya Kwanza Bara la Amerika alikutana na Watu Jamii ya Wahindi Wekundu.

Sio rahisi race moja kuzaa race nyingine, yaani Mke na Mume Wazungu wazae mtoto Mwafrika mweusi.
Au kinyume chake.
 
Inavoonekana duniani kulikua na binadamu wengine ukiacha Adam na hawa
Inavoonekana duniani kulikua na binadamu wengine ukiacha Adam na hawa
Bila shaka. Ndiyo maana tuna races tofauti duniani. Kimsingi, stori ya Adam na Eva ni ngano za waarabu na wazungu kutaka kuitawala dunia. Hakuna ajuaye vitu vilivyomo duniani vilianza na vitaisha lini.
 
Biblia ni copy & paste kutoka katika
Masimulizi ya acient Sumerian civilization sema walichofanya wayahudi ni kuicopy na kumpa character mkuu YHW Mungu wao Ila according to Sumerians hizo Hadith za adamu na Eva wanadai Anunaki ndio waliwatengeza wawe mordern kutoka kua primitive a.k.a watu pori na wakawafunza elimu kubwa za nyota,ujenzi,uchimbaji madini,madawa,kujipamba,kuvaa nguo,na vingine viiiingi hapo ndipo binadamu akaanza jitambua na kuwaita hao ni miungu sababu wametoka angani kwenye Galaxy za mbali
Nk!
 
Yapo wapi hayo maandiko
 
Back
Top Bottom