Labda hujauelewa ule Uzi vizuri.
Wenzetu huwa wanadai kwamba kila kitu kizuri ni chao sisi Tanzania hatuna kitu kizuri cha kuonyesha.
Ule Uzi ni wa evidences. Wao wanasema wanajua kupika na wanakula chakula kizuri kuliko sisi anaweka chakula chake, ukimbishia anakwambia onyesha chako tukione inabidi uweke.
Wanasema wanavaa vizuri na nguo za gharama kwasababu wana uchumi mzur na sisi Watanzania hatuwezi kumudu kuvaa hivyo. Tunawaptove wrong.
Wanasema wana wanawake wazuri eti sisi Watanzania wanawake wetu ni wabaya. Wewe binafsi unaamini hivyo? Tunatuma picha.
Kwahiyo wao wako kimkakati zaidi kuichafua Tanzania na sisi tunawakosoa kila angle ili kuonyesha watu kwamba Tanzania ni nchi nzuri na tuna vitu vizuri.
Elimu hivyo hivyo eti Watz hatujasoma huku wakiweka vyeti vyao vya mchongo lakini wanaumbuliwa. So siyo uzi wa kipuuzi kama unavyodai. Ukiacha uvumi wa uongo ukadumu muda mrefu baadaye ugeuka na kuwa ukweli.
Hapo sijazungumzia utalii,miundombinu,demokrasia n.k. Zingatia kwamba siyo sisi tu kwenye jukwaa ndio tunaufuatilia hata walioko nje wanaufuatilia pia.