Kahama VS Njombe/Mafinga

Ndicho kinawaponza watu wa Geita,Mwanza,Shinyanga, Simiyu yaani migodi na kampuni zimeshika uchumi afu kodi wanalipa Serikalini unfortunately hazimfikii mtu wa chini directly.

Inasoma GDP kubwa lakini watu hoi kimaisha.Mkoa wa Kagera,Mara na Geita ilifaa ifanye diversification maana hata mvua za kutosha inapata lakini hakuna uwekezaji unafanyika kwenye kilimo wanakimbilia kuchimba na kuiba makinikia.
 
Yan unavyoipamba njombe


Bado mko nyuma Sana tuseme ukweli
Tuko nyuma ila sio Sana ,uwe unaona aibu mkoa wa juzi unaweza tunisha misuli kwa nyie wakongwe.Come 2025-2030,Njombe itakuwa haikamatiki.

Kanda ya Ziwa imeshikiliwa na Mwanza Jiji na Kahama basi.
 
wanakuchosha bure huwezi kutoka misenyi au muleba ukaenda kuishi makete au sijui ludewa utakufa kwa stress
Kwa mkoa wenu hizo Wilaya 2 na mjini ndio zina nafuu,Ila kwa Wilaya za Njombe ulizo Zi site zilikuwa na shida ya miundombinu tuu ndio kukawa na life hardships but with new development utakuja kuishi tuu pesa inabadili kila kitu.
 
Tuko nyuma ila sio Sana ,uwe unaona aibu mkoa wa juzi unaweza tunisha misuli kwa nyie wakongwe.Come 2025-2030,Njombe itakuwa haikamatiki.

Kanda ya Ziwa imeshikiliwa na Mwanza Jiji na Kahama basi.
Hii ndio hoja kuu mkoa wa 2012 uwe na watu wenye makazi bora na mkoa ulionzishwa 1969 Kama Kagera hadi leo unahesabika katika mikoa duni hii ni sawa na mtu aliyeanza mbio saa moja anapitwa na mtu aliyeanza mbio saa tisa alasiri.Njombe inatembea kwa mwendo wa SGR nenda vijijini Kuna nyumba za Maana Sana zinajengwa.Tukisema sisi tinaonekana kupendelea lakini wageni Wanajionea wenyewe.Iko taswira iliyowaingia watu kuamini kua mikoa ya kusini hakuna maendeleo watu walichosahau ni kua Mikoa ya Njombe,Ruvuma,Mtwara,mbeya iko kasikazini mwa Malawi,Zambia,Mozambique na sehemu ya Congo.Hivyo inaopportunity nyingi kuliko mikoa iliyopo katikati mwa nchi.Nyakati zimechange muda wa viongozi kupendelea tu kwao umeisha.Sasa ni kila mtu na Nguvu zake.
 
Kila mkoa nchi hii una fursa za kutosha ishu ni value ya hizo products.

Chai,kahawa na parachichi Njombe ni champions.

Timber products Njombe ni leading region.

Mazao ya chakula kama mahindi,viazi,matunda anuwai tuko front.

Vanilla imehamia huku kwetu huko kwenu imebakia historia.

Madini kama chuma,makaa nk yako ya kutosha.

Vyanzo vya maji na utalii ndio usiseme tutahost mabwawa 3 makubwa ya kuzalisha umeme Tzn.

Uvuvi na usafiri wa ziwani tumo.

Hilo la Kagera kuongoza kwenye uzalishaji wa maharage ni kichekesho kipya mkuu.

Mwisho wa siku value na uchapakazi ndio vitaamua utofauti .
 
Kijana mie sio mpiga porojo Kama nyie na uongo wenu hapa.


Karibia robo ya maharage nchini yanatoka kagera

Njombe ni champion kwenye kahawa. Wakati kagera inazalisha asilimia 70 ya kahawa yote nchini ikifatiwa na ruvuma.

Ndizi kagera inazalisha asilimia 52 ya ndizi zote nchini
 
Uzalishaji wa kahawa Tanzania.

Kagera ikizalisha zaidi ya nusu ya kahawa yote nchini.


Msisahau kahawa ni zao la tatu nchini kuchangia Pato la taifa baada ya tumbaku na karafuu.



Njombe yenu mna population ndogo sio kwamba mna maendeleo
 
Porojo za Mitandaoni


Uzalishaji wa kahawa nchini kagera ikizalisha nusu ya kahawa yote nchini
 
Porojo za Mitandaoni.


Uzalishaji wa maharage nchini kagera ikiongozoza.

Kagera inaonekana maskini kwa sababu ya population yake but vitu kwa ground iko mbali

Nani asiyekula maharage?
Basi heshimu mkoa wa kagera.
 
Uzalishaji wa sisal nchini.

Kagera ikiwa ya pili baada ya Tanga
 
Porojo za Mitandaoni.

Uzalishaji wa ndizi nchini kagera ikiongoza

52% ya ndizi zote hutoka kagera.

Halafu unasema kagera wavivu
 
Kagera inaongoza kwa uzalishaji wa maharage nchini


Eti kijana Leo hautakula maharage


Basi kumbuka mkoa wa kagera walimaji katika Sala


Endeleeni kuzalisha miti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…