Dig the EA
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 279
- 270
Ni ukweli usiopingika miji miwili hii ya Kanda ya Ziwa inakuwa kwa kasi sana Jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama. Lakini kasi ya ukuaji na maendeleo ya Manispaa ya Kahama inaleta projection ya kuwa Kama Jiji la Mwanza baada ya miaka 10 ikichelewa miaka 15..
Mwaka 2002 nilifanikiwa kufika Wilaya ya Kahama, ikiitwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama ikiwa na eneo kubwa la utawala lakini mji ukiwa mdogo sana. Eneo la mji ilikuwa ni Nyihogo, Uhindini, Malunga, Mungura(kidogo) , Majengo (padogo) na Nyasubi ndo walikuwa wanaanza kugawa viwanja na kujenga. Mhongolo, Igomelo, Masaki, Phantom, Mbulu nk kote hapakuwepo.
Baadaye mabadiliko na maendeleo yakaanza, mji ukapewa hadhi ya mji mdogo, haikuchukuwa muda ikapandishwa hadhi ya kuwa Halmashauri ya mji, na sasa miaka mitatu sasa ni Halmashauri ya Manispaa.
Mwaka 2003 nilifanikiwa kufika Mwanza. Kiwango cha Maendeleo ya Mwanza ya miaka hiyo ndiyo maendeleo ya Kahama ya leo. Mwaka huo 2003 stand katika mji wa Mwanza ilikuwa mjini katikati--- Sahara. Na Barabara ya lami iliishia Mkuyuni. Mwaka huo huo 2003 mwishoni ikawa inaanzishwa stand ya Nyegezi. Maeneo ya Mkolani na Buhongwa hayakuwa na watu. Wakati stand inaanzishwa pale Nyegezi watu walilalamika na kufoka kwa kupelekwa porini na kwenye mivumbi.
Kwa kasi inayoonekana Manispaa ya Kahama kwa watu kuongezeka kwa kuhamia, kuzaliana, mzunguko wa biashara na pesa, maghorofa kujengwa kama uyoga nk. Kuna uwezekano mkubwa Mwanza ya leo 2023 ikawa Kahama ya 2033 au 2038. Jiji la Mwanza miaka hiyo sijui itakuwa kama miji gani ya leo.
Changamoto iliyopo kwenye miji hii ni kukosa kuzingatiwa (upendeleo) support kubwa kutoka Serikalini. Imagine jiji lile la Mwanza hakuna University hata moja ya serikali. Barabara za njia nne hakuna ukiacha Ile ya Ilemela tu, hakuna hospital kubwa ya rufaa ya serikali (Ile ya Bugando ina mkono na mguu wa Wanatoloki).
Ebu imagine jiji la Mwanza, serikali itupie na kujenga Chuo Kikuu Kama UDOM na hospital nyingine kama Mloganzila au Benjamin Mkapa.... ? Ebu fikiria barabara ya kutoka Usagara hadi Mjini iwe njia nne au sita na Ile ya mjini hadi Kisesa iwe nayo njia nne. ..... Wakati huo huo pata picha zile barabara za Kahama mjini zote zipigwe lami, na serikali ipeleke miradi pale hata Chuo cha VETA tu!!! Hapa nasema kuwa maendeleo makubwa ya jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama mengi ni wananchi/wafanyabiashara. Serikali ikipeleka miradi kadhaa miji hiyo, tutaijua vzr lake zone. Hongerni wana Kahama na Wana Mwanza.