Mgambilwa 04
Member
- Oct 19, 2023
- 25
- 42
Manispaa ya Kahama
Kanda ya Ziwa inajivunia kuwa na Jiji la Mwanza (City Council) tangu 2002 ambalo ni Jiji la pili kutangazwa baada ya Dsm. Katika miaka hiyo ya 2000s, Miji ya Musoma, Bukoba na Shinyanga ilipandishwa hadhi na kuwa Manispaa (Municipal Cluncil). Ilichukua tena miaka ipatayo 20 kwa Mji mwingine wa Kahama kupata hadhi ya Manispaa mwaka 2021.
Na kwa sasa, Miji yenye Mamlaka (Town Council) kamili ni Geita, Tarime, Bariadi na Bunda.
Hata hivyo, ukuaji wa kasi wa Miji ya Kahama na Geita, umesababisha kufunika Manispaa kongwe katika Kanda hiyo kutokana na ukuaji wa pole pole wa Manispaa hizo ambazo ni Bukoba, Musoma na Shinyanga.
Mathalani,
- Manispaa ya Kahama ina wakazi 453,000 ikishika namba 07 kwa watu wengi nchini.
- Mji wa Geita una wakazi 361,000 na unashika nafasi ya 09 kwa watu nchini.
- Mji wa Shinyanga - watu 214,000, Musoma - watu 164,000 na Bukoba - watu 144,000.
i) Uchimbaji wa dhahabu.
ii) Ipo Barabara Kuu ya kutoka Dar el Salaam kwenda Rwanda, Burundi, Uganda na Mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma.
iii) Kuna biashara kubwa ya mazao mathalani mchele, pamba na tumbaku.
Kwa upande wa Geita, ni:-
i) Uchimbaji wa dhahabu
ii) Ni Makao Makuu ya Mkoa
iii) Upo kwenye Barabara inayotoka Mwanza kwenda Kagera, Kigoma, Rwanda, Burundi na Uganda.
iv) Ni tajiri kwa matunda hususani mananasi.
v) Mkoa unaojihusisha na uvuvi.
vi) Ipo umbali mfupi wa km 35 pekee kutoka Mji wa Katoro ambao ni maarufu kwa biashara ya uchuuzi na maduka kwa Kanda ya Ziwa.
Kutokana na mazingira hayo, dalili zinaonyesha kuwa Kahama na Geita itakuja kuwa mojawapo ya miji mikubwa hapa nchini.
Hata hivyo, Kahama iko katika 'strategic position' kwenye Barabara Kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Rwanda, hali inayoipa advantage kubwa dhidi ya Mji wa Geita.
Hata hivyo kwa idadi hiyo kubwa ya watu, ni suala la muda tu kwa Geita kuwa Manispaa.
Mji wa Geita