Njombe inakusanya na watu pia wanaendelea.Hiyo ndio tofauti,kinachoitofautisha Njombe na mikoa ya Kanda ya Ziwa ni divesity ya njia za uchumi,Njombe Kuna vitu vingi vya kiuchumi vinavyomnufaisha mtu binafsi moja kwa moja wakati mikoa mingine inategemea wawekezaji wakubwa kukusanya mapato ya serikali tu.Kodi ya wawekezaji inaenda haxina hivyo watu wanasubiri huruma ya serikali kuiridisha kidogo ndio maana mzunguko wa fedha unakua kidogo tofauti na Njombe,sababu nyingine ni Biashara za kati kua nyingi kwa watu wanjombe,unakuta karibu asilimia 30 ya kaya zina mtu anapiga Biashara hivyo inakua Kama Diaspora anayerudisha mzukunguko wa fedha.Ndio maana mikoa ya Nyanda za Juu haitegemei mhindi kuleta biadhaa muhimu au watu wa mbali ni sisi kwa sisi.