Wala sijasema ukubwa wa miji hata kidogo.
Bukoba ni kamanispaa kadogo ilo nakubaliana na wew sema kanajitosheleza .
Kana airport, barabara za lami,bandari,starehe,masoko,maji,umeme na Hadi viwanja vya mpira. Ambazo miji ya kusinni huwezi kukuta mji una Mambo yote hayo katika sehemu Kama ilivyo bukoba.
Lakin ukitembelea vijjiji vya kagera ndo utaona faida ya elimu aisee. Huko Kuna majengo na majengo na majumba.
Shida ya mikoa mingi bongo unakuta miji imeendelea Sana na mikubwa ( Kama ilivyo kusini) lakin haijitoshelezi na ukienda vijijini Sasa ndo majanga matupu.
Lakin hii ni tofauti kwa mkoa wa kagera . Wilaya ya muleba kwa mfano haina mji wowote ule zaidi ya Vicenter vidogo lakin vijijini huko Kuna majumba,maji ,umeme barabara,chakula ndo maana Ina population density ya juu.
Mkuu nikuulze swali. Hiv ni Lazima ukiwa na pesa uwekeze mjini?
Binafsi naona wahaya wako sahihi kuwekeza vijijini kwao ndo maana na serikali inawafata kwa kuwajengea barabara,umeme,maji nk.
Wilaya ya muleba ni barabara mbili tu ambazo hazina lami na hakuna Kijiji kisichokuwa na umeme