#COVID19 Kagera: Mkuu wa Mkoa apiga marufuku mikusanyiko isiyo lazima ili kukabiliana na Corona

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge, amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyokuwa ya lazima na kuwataka wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kuzuia kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Meja Jenerali Mbuge amesema hatua hiyo inatokana na mkoa wa Kagera kupakana na nchi nne ambazo tayari zimeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa covid-19.

Aidha amewaagiza watendaji wa halmashauri zote nane za mkoa wa Kagera kuhakikisha wanasimamia maagizo ya Serikali juu ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Mbali na mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge, pia Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Muhandisi Robert Gabriel na mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga nao tayari wameshatangaza kupiga marufuku kwa mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kwa wananchi wake.
 
Mikusanyiko hiyo ni ya CHADEMA tu au? Maana nilikua kwenye send off Mwanza Jana na kila baa mikusanyiko ni mikubwa mno.
 
Kwa hiyo na mashabiki hawataruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya michezo? Hakutakuwepo na makongamano ya dini, matamasha na show za wasanii?

Au marufuku ni kwa makongamano ya kudai Katiba Mpya pekee!! Maana hii nchi ina maajabu mengi sana.
 
Ina maana masoko yamefungwa?

Ina maana watu awaendi tena Bukoba Club?

Ina maana stendi ya vumbi apo Bukoba imefungwa?
 
Back
Top Bottom