Makamu Mwenyekiti wa CCM Kinana anauma na kupuliza kuhusu maendeleo ya Mkoa wa West Lake (Kagera)

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
Kuwa na Maprofessor wengi siyo kigezo cha kuongeza kipato Mkoani West Lake (Kagera).

Makamu Mwenyekiti anaongelea tangu Uhuru Serikali imeweka miundombinu gani kuwezesha Mkoa wa West Lake (Kagera) kuzalisha.

Nadhani hasikwepeshe wajibu wa serikali kwa walipakodi wa West Lake (Kagera) kwa kusingizia Maprofesa.
Kama ni mkweli aeleze madhara ambayo Mkoa wa West Lake (Kagera) umepitia kuanzia vita vya Uganda, Operation Uhujumu Uchumi, zao la Kahawa kutelekezwa, ukosefu wa miundo mbinu ya usafiri, unyanyasaji wa wafanya biashara mipakani, kuingilia vyama vyetu vya ushirika vilivyokuwa imara,nk.

Kuhusu Maprofessor waangaliwe kwa maendeleo yao wenywewe maana hatulipi kodi kwao.

Suala la Ardhi kubwa na yenye rutuba, Makamu Mwenyekiti Kinana awe mkweli serikali imesaidiaje watu wa West Lake kuhusu pembejeo, wataalam wa kilimo na masoko? Zao la migomba lilipata changamoto ya ugonjwa wa mnyauko mpaka leo serikali haijafanya lolote la maana kusaidia wakulima na hata msaada wa chakula maana ndizi ndio chakula kikuu Mkoa wa West Lake

Kwasasa Wananchi wamelima Vanila kwa vingi lakini serikali imeshindwa kuwatafutia masoko, lakini majirani zetu wa Uganda wana masoko na bei iko juu ikilinganishwa na West Lake.

Hizi kauli za kutubeza na Maprofessor wetu nadhani hazifai kabisa Serikali ya CCM itimize wajibu wake kwa walipakodi wa West Lake.

Mwisho, baada ya kuchoshwa na hizi kauli, serikali ya CCM ieleze bayana ina mkakati gani imeweka kwenye masuala ya kilimo kwa walipakodi wa West Lake baada ya Makamu Mwenyekiti kuona kuna Ardhi kubwa na yenye rutuba.

Matatizo ni mengi sana Mkoa wa West Lake ambayo yakianishwa yote Watanzania wanaweza kujua chanzo ni nini na mchawi wao ninani tangu Uhuru mpaka sasa wala sio Maprofessor.

Jambo dogo tu hivi hao wasomi ndo wanasababisha mfuko wa sementi iuzwe shs 25,000 na kuendelea au mbolea mfuko mmoja zaidi ya shs 100,000 maana ya ruzuku inapatikana kwa mizengwe mikubwa sana.

West Lake serikali ya CCM imegoma kuwekeza kabisa kwenye miundombinu zaidi ya kutukashfu tu kwa kutumia Elimu ya watu wa West lake!

West Lake inapakana na Burundi, Rwanda, Uganda, DR CONGO na Kenye lakini serikali imekuwa ikipiga danadana Mkoa huu makusudi mpaka kuuburuta mwisho kabisa!

IMG-20231212-WA0010.jpg
 
Back
Top Bottom