Kafulila: Bei ya Umeme Kenya ni mara mbili ya Tanzania

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,542
2,174
KAFULILA: BEI YA UMEME KENYA MARA MBILI YA TANZANIA

Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila amesema takwimu za ulinganisho wa bei ya Umeme Afrika mashariki zinaonesha kwa wastani watanzania wanatozwa bei chini ya umeme kuliko nchi zote Afrika mashariki na kusisitiza kuwa nafuu hiyo ya bei ni kielelezo cha serikali inayojali wananchi wake.

Kafulila amesema hayo leo kwenye mkutano wa mapokezi ya Katibu Mkuu, Comrade Chongoro wilayani Meatu ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Simiyu.

"Jana serikali imetoa bei mpya za mafuta zenye punguzo la takribani 300/= kwa lita kama mkakati wa kupunguza makali ya bei za bidhaa. Serikali itaendelea kuchukua hatua ili kupunguza makali ya gharama za maisha nchini. Tuelewe tu kwamba mbali ya mkakati huo kwenye mafuta, pia ni sera ya serikali kuhakikisha wananchi wake wanapata nishati ya umeme kwa bei nafuu zaidi. Takwimu za ulinganisho wa bei ya nishati ya umeme duniani zinaonesha kwamba wakati bei ya umeme Tanzania wastani ni dola senti 10, Kenya ni dola senti 21, Uganda dola senti 18 na Rwanda ni dola senti 26"

Aliongeza kusema " Hii maana yake wananchi wa Kenya wananunua umeme kwa bei kubwa mara mbili ya wananchi wa Tanzania. Na zaidi tunafahamu sera ya serikali kuhakikisha watu wa kipato cha chini kupata nishati ya umeme.. kwamba wananchi wanaotumia sio zaidi ya unit 75 kwa mwezi wanalipia unit 1 ya umeme kwa sh 100/= Yote hii ni namna ya kujenga maendeleo yanayobeba watu wengi" alisisitiza Kafulila na kuwataka wananchi kutambua juhudi za serikali katika maisha yao hata kama bado kuna changamoto kwani serikali inazitambua na kuonekana wazi kukabiliana nazo kwa vitendo" alihitimisha Kafulila
 
KAFULILA: BEI YA UMEME KENYA MARA MBILI YA TANZANIA
Hawa wasomi wetu wanatuangusha
Hivi anajua Bajeti ya Kenya kwa mwaka ni karibia marambili ya bajeti ya Tanzania kulingana na makusanyo yao YALIVYO MAKUBWA. Hii inamaanisha uchumi unavyo imarika vitu navyo huongezeka bei lakini pia; Vyanzo vya umeme vyao sio vingi. Najua huyu msomi husafiri Nje; namuomba akaulize bei ya suruali ya Jeans Marekani kama haita anzia kwenye dola 50 hadi dola 450hivi (shs laki moja hadi laki tisa hivi kwa suruali moja. Hiyo sio kwa sababu ya vita ya Ukraine; ni kwa sababu ya uchumi wao ni mkubwa sana.

Hii ni sawa na kulinganisha bei ya Petrol nchini Ujerumani na Tanzania wakati mshara wa chini wa Ujerumani ni karibia mara 8 ya mshahara wa hapa; Hapo sijaongelea mishahara ya ngazi tofauti inaweza kuwa mara 20 zaidi ya hapa; sasa unategemea ujerumani iuze mafuta kwa bei ya Tanzania?
Natamani mambo ya kiuchumi waachiwe wanauchumi!!!
 
KAFULILA: BEI YA UMEME KENYA MARA MBILI YA TANZANIA
Huyu jamaa ndio maana Werema alimuita TUMBILI.

Unapokuwa na wàtu wa namna hii katika nafasi za uongozi ni changamoto sana.

Kwa jinsi umeme unavyosumbua namshangaa sana kuja na kitu kama hiki...So what?.

Kafulila kweli kafulia sana.

Naona mwenezi Shaka baada ya kuwapiga mkwara wanafumuka kutoka mashimoni kwa staili hii...very useless.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kenya wanatuzidi vingi ila kwenye ufisadi hatujawafikia maana tuna vinarawa kufuja hela hapa
 
Ukiona hivyo ujuwe umeme unaenda kupandishwa muda si mrefu, lakini units 1 sio Tsh 100 Bali Tsh 357. Awamu hii ya Samia tutalimia meno.
 
Back
Top Bottom