Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,892
- 3,196
Ooh!
Sawa kabisa.
Usipoelewa sasa, utaelewa baadaye.
Basi bhana, Mfalme Nebukadneza katika fahari yake, akawa anatembea kwenye kuta za mji wa Babeli huku akijisifu namna alivyoiboresha Babeli ndani ya kipindi chake cha uongozi.
Ni kweli hadi kufikia muda huo, Babeli ilikuwepo muda mrefu wa mamia ya miaka. Lakini ni wakati wa uongozi wake ndipo Babeli ilifikia kilele chake cha ustawi kutokana na hekima na uongozi wake bora. Kwa kweli kipindi cha Nebukadneza ilikuwa ni "Hapa Kazi Tu". Na kweli bhana, kazi ilifanyika, ikafanyika kwelikweli matokeo yake, Babeli likawa jiji la kuvutia duniani kote. Babeli ikawa "Super Power" ya dunia.
Baadhi ya vitabu vya dini, huipa Babeli hadhi ya Utawala wa DHAHABU. Hii ni kutokana na utajiri mkubwa sana iliokuwa nao kiasi kwamba vitu vingi vilitengenezwa kwa dhahabu na hata sarafu yao ilikuwa ni dhahabu pia.
Ni kutokana na utajiri huo, basi Mfalme Nebukadneza licha ya kuonywa mara nyingi na Mungu kupitia kwa watumishi wake, bado akaonesha kiburi na kujiona yeye ndo yeye!
Basi bhana, sauti ikasikika ikimwambia atafukuzwa atoke kwenye kiti chake cha enzi kwa muda wa miaka 7. Na kwamba, kwa muda huo wote, atakuwa pamoja na wanyama wa porini na kwamba chakula chake kitakuwa ni nyasi!
Haya bhana, ikawa hivyo. Miaka 7 akawapo porini akiwa na wanyama wa porini, akila nyasi. Baada ya miaka hiyo 7, akarudishwa ikulu na kuendelea na utawala wake huku kiburi chote alichokuwa nacho mwanzoni kikawa kimeisha. Kwa wale wasoma Biblia, mkasome Danieli sura ya 3 na 4.
Mfalme Nebukadneza akaona kwenye ndoto mti ukikatwa na kubakia kisiki ambacho kilikaa hivyo hivyo kwa muda wa miaka 7 kabla hakijaanza kuchipua tena. Baada ya miaka 7, kisiki kikaanza kuchipua na kadri siku zilipokuwa zinaendelea, nacho kikawa kinazidi kuchipua na kukua zaidi na zaidi! Kumbe haya maono yalimuhusu Mfalme Nebukadneza, na kwamba fahari yake ya mwisho ingekuwa maradufu kulinganisha na ile aliyokuwa nayo kabla ya kufukuzwa porini....
Basi bhana, mti wake wa kwanza ukakauka. Lakini ukajitokeza mwingine palepale ulipokuwa umepandwa wa kwanza uliokauka. Na kadri huo mti ulivyozidi kukua, ndivyo na nguvu zake zilivyozidi kuongezeka siku hadi siku.
Mara pap, aliyekuwa anaota ndoto za mchana, akaamka na kuanza kuitafakari ndoto yake.
Nyie!
Haya bhana.
Tafakari njema.
Rejea:
1. Holy Bible
2. The Richest Man In Babylon