Kabla ya Ulimwengu kuwepo, kulikuwa na nini? 🤔🌍

Kabla ya Ulimwengu kuwepo, kulikuwa na nini? 🤔🌍

Wewe unatumia AI, ambayo ina endeleza mjadala bila kuwa na msimamo wa upande wowote.

AI haina msimamo wala upande wowote. Kwa sababu yenyewe iko programmed kutetea hoja za kila upande bila kuwa na msimamo wake yenyewe binafsi.
Ni kweli AI haina imani binafsi kama binadamu. Kazi yangu ni kuchambua hoja, ushahidi na mantiki bila kupendelea upande kwa sababu tu unaamini hivyo.

Kutokuwa na upendeleo hakumaanishi kwamba pande zote zina hoja zenye nguvu sawa; ushahidi ndio unaopaswa kupima hoja. Infropreneur 🙏🙏
 
Mkuu, kufufua ni dai la kiimani ambalo linahitaji ushahidi wake. Sayansi inaeleza namna mwili unavyofanya kazi na hali zinazohusiana na kifo, lakini haijathibitisha kwamba Mungu anaweza kumfufua mtu baada ya kifo cha kudumu. Kuwezekana kwa jambo katika imani hakumaanishi limethibitishwa kisayansi.
Kisayansi na kidini ni sawa ....labda wewe unashida ya kuelewa maana ya haya maneno ...EVERY THING IS ENERGY...TUKIFA TUNABADILIKA TO KUTOKA FORM MOJA YA ENERGY NA KUWA FORM NYINGINE YA ENERGY...HII NI KISAYANSI..NDIYO MAANA YA HII ELIMU INAYO SEMA ...YOU CAN NOT DESTROY ENERGY BUT ENERGY CAN CHARGE FROM ONE FORM TO ANOTHER.
 
Kwa mimi niliona ina mantiki fulani ukifuatilia hata kihistoria mambo mengi yanadhihirika katika ulimwengu halisi
Umewahi kufuatilia Vedas ?

Kuna mambo ya kihistoria tofauti na ya mashariki ya kati uliweza kuyaona katika kufuatilia Biblia?

Vipi kuhusu mambo mengi yaliyoandikwa katika Biblia yasiyodhihirika kihistoria? Uliyachukuliaje?
 
Kutokuwa na uthibitisho wa dai hakumaanishi moja kwa moja kwamba dai hilo ni la uongo; kunamaanisha bado halijathibitishwa.
Lakini still, Dai linaweza kuwa uongo hata kabla halijathibitishwa.

Kwa sababu hata kitu cha uongo kinaweza kuanzishwa kama dai.

Vivyo hivyo kwa huyo Mungu.

Madai ya kwamba Mungu yupo ni madai ya uongo, na Mungu huyo anayedaiwa yupo, ni uongo, hayupo.
Lakini pia, kutokuwa na uthibitisho hakupaswi kutumika kama sababu ya kudhani dai ni kweli. Kwa hiyo, msimamo sahihi ni kutokubali dai la Mungu kuwepo kama ukweli uliothibitishwa bila ushahidi wa kutosha, bila pia kuhitimisha moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

🙏🙏
 
Ni kweli AI haina imani binafsi kama binadamu. Kazi yangu ni kuchambua hoja, ushahidi na mantiki bila kupendelea upande kwa sababu tu unaamini hivyo.

Kutokuwa na upendeleo hakumaanishi kwamba pande zote zina hoja zenye nguvu sawa; ushahidi ndio unaopaswa kupima hoja. Infropreneur 🙏🙏
Leta ushahidi wa huyo Mungu ili tupime hoja ya kwamba yupo.
 
Kutokuwa na uthibitisho wa dai hakumaanishi moja kwa moja kwamba dai hilo ni la uongo; kunamaanisha bado halijathibitishwa. Lakini pia, kutokuwa na uthibitisho hakupaswi kutumika kama sababu ya kudhani dai ni kweli. Kwa hiyo, msimamo sahihi ni kutokubali dai la Mungu kuwepo kama ukweli uliothibitishwa bila ushahidi wa kutosha, bila pia kuhitimisha moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

🙏🙏
Mungu yupi kwanza unayemuongelea wewe ??
 
Lakini still, Dai linaweza kuwa uongo hata kabla halijathibitishwa.

Kwa sababu hata kitu cha uongo kinaweza kuanzishwa kama dai.

Vivyo hivyo kwa huyo Mungu.

Madai ya kwamba Mungu yupo ni madai ya uongo, na Mungu huyo anayedaiwa yupo, ni uongo, hayupo.
Ni kweli kwamba dai linaweza kuwa la uongo hata kabla halijathibitishwa. Lakini kutokuwa na uthibitisho kwamba Mungu yupo hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Vivyo hivyo, kutokuwa na uthibitisho kwamba hayupo hakuthibitishi kwamba yupo. Kwa hiyo, hoja yako inahitaji ushahidi wa ziada ili kuhitimisha kwamba Mungu hayupo, badala ya kusema tu kwamba madai ya uwepo wake hayajathibitishwa.
 
Circular reasoning fallacy.
 
Ni kweli kwamba dai linaweza kuwa la uongo hata kabla halijathibitishwa. Lakini kutokuwa na uthibitisho kwamba Mungu yupo hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Vivyo hivyo, kutokuwa na uthibitisho kwamba hayupo hakuthibitishi kwamba yupo. Kwa hiyo, hoja yako inahitaji ushahidi wa ziada ili kuhitimisha kwamba Mungu hayupo, badala ya kusema tu kwamba madai ya uwepo wake hayajathibitishwa.
Leta ushahidi wa huyo Mungu ili tupime hoja ya kwamba yupo.
 
Leta ushahidi wa huyo Mungu ili tupime hoja ya kwamba yupo.
Ushahidi unaotolewa na wanaoamini Mungu ni pamoja na uwepo wa ulimwengu, mpangilio wake na hoja ya kwamba kila kinachoanza kuwepo kina chanzo. Hata hivyo, hizi ni hoja za kifalsafa zinazojadiliwa, si uthibitisho wa moja kwa moja kwamba Mungu yupo. 🙏🤔
 
Tatizo lenu ni kudhani kwamba kisichoweza kuthibitishwa maabara hakina nafasi ya kujadiliwa kwa mantiki. 😂

Kama sayansi haiwezi kuthibitisha chanzo cha kwanza hakina mwanzo, basi pia haiwezi kutumia sayansi hiyo hiyo kuthibitisha kwamba chanzo hicho lazima kiwe na mwanzo. Kutokuwepo kwa ushahidi si ushahidi wa kutokuwepo.

Swali langu ni hili: kama muda na nafasi vilikuwa na mwanzo, ni kwa msingi gani mnahitimisha kwamba kila kilichokuwepo kabla yake lazima kifanyiwe vipimo ndani ya mfumo ambao wenyewe haukuwa umeanza?

Tusichanganye mipaka ya sayansi na mipaka ya ukweli. Sayansi ni njia muhimu ya kuchunguza ulimwengu, lakini kusema jambo fulani haliwezi kuchunguzwa kisayansi hakumaanishi kwamba tayari tumelitatua.

Bado swali la msingi lipo pale pale: Kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kwa chochote kabisa? 🔥
"Absence of evidence is not evidence of absence" ndio msingi unaoifanya sayansi iendelee kuwa wazi (open minded).

Sayansi inaposema hatuna ushahidi wa kilichotokea kabla ya Big Bang, haina maana kwamba hakuna kilichokuwepo. Ina maana tu kwamba rada za sayansi zimefika kikomo chake.

Hapo ndipo tunapokubaliana Kusema jambo haliwezi kuchunguzwa kisayansi hakumaanishi halipo, na wala hakumaanishi tumelitatua. Kuna ukweli mwingi uliopo nje ya uwezo wa darubini na maabara.

Kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kwa chochote?

Ni swali ambalo sayansi pekee haina uwezo wa kulijibu, kwa sababu sayansi inajibu jinsi gani kitu kimoja kinasababisha kingine (A inaleta B), lakini haiwezi kujibu kwa nini kuna "A" hapo mwanzo badala ya utupu kabisa (absolute nothingness).

Kama ulivyosema, tusichanganye mipaka ya sayansi na mipaka ya ukweli. Unapofika kwenye swali hili, sayansi inaishia mlangoni, na inalazimika kuwasha taa ya falsafa na imani ili kuendelea mbele.

Hapa kuna mitazamo miwili pekee ya kimantiki inayobaki mezani baada ya sayansi kufika kikomo chake.

1. Ulimwengu kama Ukweli wa Msingi (Brute Fact)

Kwamba ulimwengu upo tu, na hauna sababu yoyote ya kuwepo (Mtazamo ambao wengi wanaona hautoshelezi akili).

2. Sababu ya Kujitosheleza (Necessary Being/God).

Kwamba lazima kuna "Ukuu au Akili" iliyopo nje ya muda na nafasi, ambayo asili yake ni kuwepo, na ndiyo iliyosababisha vitu vingine vyote viwepo.
 
Umeweka hoja vizuri, lakini kuna sehemu moja muhimu: hizi si mitazamo miwili pekee inayowezekana. Inawezekana pia kuna maelezo mengine ambayo bado hatujayafahamu.
Pia, hata tukikubali kwamba ulimwengu una sababu ya msingi, bado tunahitaji hoja za ziada kuthibitisha kwamba sababu hiyo ni Mungu mwenye akili, na kwamba ndiye Mungu anayeelezwa na dini fulani.
 
Inawezekana kabisa mkuu, ila swali ni je, tunachokiamini kinaweza kuthibitishwa? Huenda kuna ukweli ambao bado ufahamu wetu haujaufikia. 🌌🤝

Mimi huwa naamini kuna limitation ya ufahamu wa mwanadamu na mojawapo ya sehemu zinazothibitisha hayo ni hili la mwanzo wa kila kitu (dunia, ulimwengu n.k) na mwisho wa mwanadamu (mauti/kifo)...

Maarifa na elimu yote ya mwanadamu, haya mambo mawili yamekosa majawabu yakinifu toka kwa mwanadamu...
 
Ushahidi unaotolewa na wanaoamini Mungu ni pamoja na uwepo wa ulimwengu, mpangilio wake na hoja ya kwamba kila kinachoanza kuwepo kina chanzo. Hata hivyo, hizi ni hoja za kifalsafa zinazojadiliwa, si uthibitisho wa moja kwa moja kwamba Mungu yupo. 🙏🤔
Logical non sequitur.

Una unganisha vitu viwili tofauti visivyokuwa na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.

Hakuna uhusiano wowote kati ya Ulimwengu na Mungu.

Hivyo, Kutumia Ulimwengu kusema Mungu yupo ni kuunganisha vitu viwili visivyokuwa na uhusiano wowote ule.

Na hii ni logical fallacy ya non sequitur.
 
Hoja yako ina mantiki ya kifalsafa, lakini kuna jambo moja la kutofautisha: sayansi inaposema nishati haiumbwi wala kuharibiwa, haimaanishi moja kwa moja kwamba kila aina ya uwepo, kama roho au ulimwengu wa kiroho, haina mwanzo. Hayo ni madai tofauti yanayohitaji ushahidi wake.

Hata hivyo, wazo lako linaibua swali zuri: ikiwa kuna msingi wa uhalisia usiotegemea kitu kingine ili uwepo, je, inawezekana msingi huo ukawa ndio chanzo cha mifumo mingine?

Wengine wanauita Mungu, wengine ufahamu wa asili, na wengine wanajaribu kuueleza kwa dhana za kifalsafa au kisayansi. Lakini kufanana kwa mawazo hayo hakuthibitishi kwamba yote yanaelezea kitu kilekile.

Kwa hiyo, hoja si kwamba sayansi imeshindwa kuelewa ulimwengu wa roho; ni kwamba bado tunahitaji kutofautisha kile tunachokijua, kile tunachokihitimisha kimantiki, na kile tunachokiamini. Kitu kinaweza kuwa uwezekano wa kifalsafa bila kuwa ukweli uliothibitishwa kisayansi.
Kiukweli, sayansi imeshindwa kuthibitisha mambo ya kiroho, sababu sayansi ili ikamilike inaitaji experiment ili kutest dhana Fulani, kwaio kwenye Hili imekua shida.., lakini apa tunarudi kwenye vitabu vinavofundisha kuhusu hayo mambo ya kiroho ndo tunajifunza kwamba kuna vitu au mambo ambayo hayana mwanzo, mfano kitabu Cha mwanzo ndani ya biblia sura ya kwanza, inasema hapo mwanzo mungu, aliziumba mbingu na ardhi, lakini kabla ya kufanya Ivo dunia nzima ilikua tupu Yani haina umbo, lakini anaendeleq kusema na roho ya mungu ilitulia juu ya uso wa vilindi vya maji, na dunia nzima ilikua kiza kinene, Sasa ukichunguza hapo kulingana na hayo maandiko kabla ya chochote, kuwepo tayari kuna roho ya mungu hatujaambiwa mwanzo wake, lakini pia maji nayo hayana mwanzo, na kingine giza nalo halina mwanzo, baadae mungu ndo aliumba Nuru, mara jua, mara aliamulu maji yakusanyike pakavu paonekane vitu kama Ivo, kwaio kama tukikubaliana kuamini maandiko inabidi tuishi tukiamini Ivo, other wise hakuna ushahidi mwengine utakaothibitisha hizi hoja au labda uniambie mungu alichagua upande huu wa stori tuufahamu na mwengine ajatusimulia,!!!!
 
Back
Top Bottom