Je, Kulikuwa na Machafuko Kabla ya Mwanadamu?

Je, Kulikuwa na Machafuko Kabla ya Mwanadamu?

verify

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2024
Posts
1,294
Reaction score
3,079
Kuna jambo la kuvutia sana katika Mwanzo 1:2 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu; na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.” Aya hii inaweza kutufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi tunalipita: nini kilitokea kabla ya hali hii ya ukiwa na utupu? Biblia haitoi maelezo ya moja kwa moja kwamba kulikuwa na vita au viumbe waliokuwa wakiishi duniani kabla ya mwanadamu, lakini ukitazama kwa jicho la udadisi, unaweza kujiuliza ikiwa kulikuwa na tukio fulani lililosababisha hali hiyo ya machafuko. Labda kulikuwa na mabadiliko makubwa, labda machafuko, au hata vita lakini haya ni mawazo ya kutafakari, si ukweli uliothibitishwa na maandiko.

Kama tunaruhusu akili ichunguze zaidi, tunaweza kujiuliza je, “ukiwa na utupu” ilikuwa hali ya mwanzo kabisa, au ilikuwa matokeo ya jambo lililotokea kabla ya simulizi kuanza? Mungu anaonekana kuleta nuru, mpangilio na uhai katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na giza na vilindi vya maji. Hii inaweza kutufanya tufikirie uwezekano wa “reset” ya uumbaji si kwamba Biblia inasema Mungu alifanya reset baada ya vita, bali kama hypothesis ya kifalsafa. Huenda kulikuwa na historia ambayo haijaelezwa huenda hakuna kitu kilichokuwepo kabla yake. Pengo hilo ndilo linaloifanya akili iulize.

Udadisi huu unaweza kuonekana hata katika simulizi la baadaye la Adamu, Hawa na Kaini. Baada ya Kaini kumuua Abeli, Kaini anaonekana kuwa na hofu kwamba “kila mtu atakayeniona ataniua,” na baadaye anaenda kuishi katika nchi nyingine na anapata mke. Hapo ndipo maswali yanapoanza: hao watu aliowaogopa walikuwa nani? Mke wa Kaini alitoka wapi? Na kizazi chake kilianzaje? Kuna maelezo mbalimbali ya kitheolojia kuhusu maswali haya, lakini simulizi lenyewe halitoi kila hatua kwa undani. Hii inatukumbusha kwamba Biblia mara nyingi haituelezi kila kitu kuhusu mazingira ya hadithi.

Kwa hiyo, inawezekana kabisa mtu akauliza kwa udadisi: kama kuna mambo ambayo hatupewi maelezo kamili kuhusu dunia baada ya Adamu na Hawa, je, tunaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba tunaelewa kila kitu kuhusu hali iliyokuwepo kabla ya Mwanzo 1:2? Labda kulikuwa na machafuko ambayo hatujui chochote kuhusu chanzo chake labda kulikuwa na viumbe au matukio ambayo hayakutajwa au labda “ukiwa na utupu” ilikuwa tu hali ya dunia kabla Mungu hajaiweka katika mpangilio. Hatuwezi kuchagua mojawapo na kuiita ukweli bila ushahidi lakini tunaweza kuiruhusu akili yetu kuiuliza.

Ndiyo maana udadisi ni muhimu. Udadisi hauimaanishi kukataa Biblia unaweza kumaanisha kuisoma kwa kina zaidi na kutambua tofauti kati ya kile maandiko yanasema na kile sisi tunachodhani. Labda kabla ya mwanadamu hakukuwa na vita kabisa; labda kulikuwa na tukio ambalo hatulijui au labda hakukuwa na historia yoyote ya aina hiyo. Lakini swali linabaki ikiwa Mwanzo 1:2 inatupa picha ya dunia ikiwa katika ukiwa, utupu, giza na vilindi vya maji, ni nini kilichotokea kabla ya pazia hilo kufunguliwa? Huenda hatutapata jibu kamili, lakini kuuliza swali hilo kunaweza kutufanya tusome zaidi, tufikiri zaidi, na tutambue kwamba wakati mwingine kutokujua ndiko kunakoanzisha safari ya kutafuta maarifa.
 
Fungua Mwanzo 5:4, Biblia inasema wazi baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800 na alizaa wana na binti, Kaini aliishi miaka mamia, ulitaka wataje majina ya watoto wote elfu moja kwenye kitabu kimoja Mkuu?
Kama Mwanzo 5:4 inasema Adamu alikuwa na wana na binti lakini Biblia haitaji majina yao yote, hao wana na binti walizaa na kuoana na nani? Kaini alipata mke kutoka wapi, na kama wote walikuwa watoto wa Adamu na Hawa, inawezekanaje kizazi hicho kuendelea bila kuoana ndugu? Je, kutotajwa kwa majina kunamaanisha hawakuwepo, au kuna sehemu ya historia ambayo Biblia haikueleza kwa undani?

Turudi kwenye swali letu kuhusu mwanzo 1:2
 
Kipindi hicho hakukuwa na mtu mwingine duniani, ulitaka waoane na nyani?
 
Marcostilone unamaana ya kwamba kaini alilala na ndugu zake lakini biblia hyo hyo inasema

Walawi 20:17 mwanaume akimchukua dada yake na kufanya naye ngono, kitendo hicho kinahukumiwa kuwa cha aibu na wote wawili watachukuliwa hatua.

Kumbukumbu la Torati 27:22 anatolewa laana mtu anayelala na dada yake, awe wa baba au wa mama.

Bado huna majibu ambayo ni yamoja kwa moja maana suala hilo tayari lilikua laana tangu uumbaji kulala na umbu wako.
 
Bado haimake sense mkuu hizo ni perception zako lakini hakuna direct proof kwamba alioa ndugu, bado Kuna vitu vingi huvijui naweza kusema hvo
Kuliko kubahatisha mambo ya kufikirika kichwani kwako, mimi natumia kilichopo kwenye maandiko. Kaini alimuoa dada yake, period.

Hata Ibrahimu alimuoa Sara ambaye alikuwa dada yake wa baba mmoja, kipi cha ajabu kwa Kaini?

Kama karne nyingi baadaye watu walikuwa wanaoana ndugu, unashangaa nini kwa watoto wa Adamu?
 
Unaniletea sheria za Walawi na Kumbukumbu la Torati zilizotolewa kwa Musa miaka 2,500 baadaye baada ya uumbaji wakati wa Kaini hiyo sheria haikuwepo kabisa.

Hakuna dhambi bila sheria, jenga hoja zako vizuri.
 
Kabla ya wanadamu dunia ilikaliwa na majini baada ya kufanya uharibifu mkubwa......ikasafishwa na kuletwa mwanadamu.

Qur’an inasema:
“Hakika Mimi nitaweka Khalifa katika ardhi.”
— Al-Baqarah 2:30

Quran.com
Malaika wakasema: “Je, utaweka humo atakayefanya uharibifu na kumwaga damu?”
Hapa wanazuoni wa tafsiri wameeleza namna kadhaa walivyoweza kujua kwamba kutakuwa na umwagaji damu. Maelezo mashuhuri katika baadhi ya tafsiri ni kwamba majini waliishi ardhini kabla ya Adam (A.S.), wakafanya uharibifu na kumwaga damu. Ibn Kathir ananukuu riwaya zinazosema hivyo.
 
Bado haimake sense mkuu hizo ni perception zako lakini hakuna direct proof kwamba alioa ndugu, bado Kuna vitu vingi huvijui naweza kusema hvo
Kama Adamu na Hawa walikuwa chanzo cha wanadamu wote, basi
Kaini alimuoa mmoja wa binti za Adamu na Hawa—yaani dada yake.

Mungu alikuja kukataza hilo baadae kwenye walawi 18.
 
Kuliko kubahatisha mambo ya kufikirika kichwani kwako, mimi natumia kilichopo kwenye maandiko. Kaini alimuoa dada yake, period.

Hata Ibrahimu alimuoa Sara ambaye alikuwa dada yake wa baba mmoja, kipi cha ajabu kwa Kaini?

Kama karne nyingi baadaye watu walikuwa wanaoana ndugu, unashangaa nini kwa watoto wa Adamu?
Sawa, umejenga theory yako kwa kutumia mifano na vifungu kadhaa vinavyofanana na hoja tunayojadili. Lakini bado kuna sehemu ambayo maandiko hayajasema wazi kwamba alioa ndugu yake hiyo ni conclusion uliyoifikia kutokana na unavyointerpret vifungu kwa hiyo, kwa namna hiyo mjadala unakuwa mgumu kuufuatilia kwa sababu bado hatujaweka msingi wa hoja vizuri kwanza tuweke nondo zote mahali pake tutenganishe kile Biblia inachosema wazi, kile tunachodhani kutokana na maandiko, na kile ambacho bado ni swali Baada ya hapo ndipo tunaweza kuendesha mjadala wenye mantiki na kueleweka, mkuu.
 
Back
Top Bottom