Kabla ya Ulimwengu kuwepo, kulikuwa na nini? šŸ¤”šŸŒ

Ni kweli kwamba imani pekee si sawa na uthibitisho. Lakini pia, kutokuwepo kwa uthibitisho unaokubalika kwa wote hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.
Sasa thibitisha Mungu yupo.
Theism ni msimamo wa kuamini Mungu yupo, huku atheism ikiwa na misimamo tofauti kuhusu uwepo wake.

Hoja yangu ni hii: je, kutokuwa na uthibitisho wa Mungu ni uthibitisho kwamba Mungu hayupo, au ni kukiri kwamba bado hatuna jibu la mwisho? Tofautisha kati ya kutothibitisha jambo na kuthibitisha kwamba jambo hilo si kweli.
Don't shift the burden of proofs to Atheists.

Madai ya kwamba Mungu yupo ni yenu theists. Na nyie waamini Mungu ndio mna mzigo wa kutoa uthibitisho wa Mungu huyo mnayedai yupo.

Falsafa ya uthibitisho inamtaka anayeanza kudai kitu kipo ndio mwenye mzigo wa kuthibitisha.

Kama unakataa Mungu hayupo, it means unajua yupo. Na unaweza kuthibitisha yupo.

Sasa thibitisha Mungu yupo.

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo na hapohapo unakataa kwamba hayupo. Utakuwa huelewi hata unataka nini. Na wala hueleweki msimamo wako ni upi.
 
Nakubaliana nawe kwa kiasi fulani mkuu. Kusema ā€œsijuiā€ pale ambapo hatuna uhakika ni uaminifu, si udhaifu. Lakini kutokujua jibu leo hakumaanishi swali halina maana au halistahili kuchunguzwa. Wakati mwingine, kukubali tusichokijua ndiyo hatua ya kwanza ya kutafuta ukweli. šŸ¤
Sawa lakini kutafuta majibu si kitu kibaya

Lakini katika ulimwengu wa wafu jitihada zako zinafua dafu wapi.!

Me katika kujiridhisha kupata majibu nimefikia kwenye kwenye kinyaa cha kifo

Nilitaka kupingana nacho ila nikajikuta nakipenda kuliko kuishi.. kitamu kuliko usingizišŸ¤—

Sawa utawawezesha watu katika kila idara ya maisha mwisho utatambua Kuna watu na tamaa zisizo na ukomo.! What fvk
 
Nimeelewa hoja yako. Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, na hakuna kilichokuwepo kabla yake. Lakini swali la kifalsafa linabaki: tunathibitishaje kwa ushahidi kwamba ulimwengu ulitoka kwa Muumba, badala ya kulichukulia hilo kama ukweli unaokubalika kwa imani? Hapo ndipo tofauti kati ya imani na uthibitisho inapoanzia.

Bwana Utam
Na tunathibitishaje huyo muumba ni Allah na sio Jehovah au Brahma
 
Sasa thibitisha Mungu yupo.

Don't shift the burden of proofs to Atheists.

Madai ya kwamba Mungu yupo ni yenu theists. Na nyie waamini Mungu ndio mna mzigo wa kutoa uthibitisho wa Mungu huyo mnayedai yupo.

Falsafa ya uthibitisho inamtaka anayeanza kudai kitu kipo ndio mwenye mzigo wa kuthibitisha.

Kama unakataa Mungu hayupo, it means unajua yupo. Na unaweza kuthibitisha yupo.

Sasa thibitisha Mungu yupo.

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo na hapohapo unakataa kwamba hayupo. Utakuwa huelewi hata unataka nini. Na wala hueleweki msimamo wako ni upi.
Kwanza, nakubaliana nawe kwamba anayetoa dai ndiye anayepaswa kutoa sababu za kulitetea. Lakini kuna tofauti kati ya kusema ā€œMungu hayupoā€ na kusema ā€œsijaona ushahidi wa kutosha kuniaminisha kwamba Mungu yupo.ā€

Mimi nikisema Mungu yupo, hoja yangu si kwamba kila kitu lazima kiwe na muumbaji, bali ni kwamba uwepo wa ulimwengu wenyewe unazua swali la msingi: Kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kwa chochote?

Hii peke yake haithibitishi Mungu, lakini ni hoja ya kifalsafa inayohitaji kujadiliwa. Vivyo hivyo, kutokuwa na uthibitisho wa Mungu hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Kwa hiyo, sitadai kwamba nimekuthibitishia Mungu kwa kuuliza swali tu. Nitakachofanya ni kutoa hoja, wewe uzichunguze na uzipinge kwa hoja. Mwisho wa siku, tunapaswa kutofautisha kati ya kile kilichothibitishwa, kile kinachowezekana na kile tunachoamini.
 
Sawa lakini kutafuta majibu si kitu kibaya

Lakini katika ulimwengu wa wafu jitihada zako zinafua dafu wapi.!

Me katika kujiridhisha kupata majibu nimefikia kwenye kwenye kinyaa cha kifo

Nilitaka kupingana nacho ila nikajikuta nakipenda kuliko kuishi.. kitamu kuliko usingizišŸ¤—

Sawa utawawezesha watu katika kila idara ya maisha mwisho utatambua Kuna watu na tamaa zisizo na ukomo.! What fvk
Umeingia kwenye swali zito la falsafa ya maisha. Lakini nadhani kuna tofauti kati ya kutambua kwamba maisha yana mwisho na kufikia hatua ya kuona kifo ni bora kuliko kuishi. Kutokuwepo kwa majibu ya kila swali hakumaanishi kwamba maisha hayana thamani. Na kuhusu tamaa za binadamu, huenda tatizo si kutokuwa na mwisho kwa mahitaji yetu, bali ni kutokujua ni wakati gani tunapaswa kuridhika.
 
Na tunathibitishaje huyo muumba ni Allah na sio Jehovah au Brahma
Hapo ndipo umuhimu wa kuchunguza madai ya kila dini unapokuja. Kuthibitisha uwepo wa Muumba hakutoshi kuthibitisha moja kwa moja kwamba ni Allah, Jehovah au Brahma. Hilo linahitaji hatua nyingine ya hoja na ushahidi unaotofautisha madai yao.
 
Umeingia kwenye swali zito la falsafa ya maisha. Lakini nadhani kuna tofauti kati ya kutambua kwamba maisha yana mwisho na kufikia hatua ya kuona kifo ni bora kuliko kuishi. Kutokuwepo kwa majibu ya kila swali hakumaanishi kwamba maisha hayana thamani. Na kuhusu tamaa za binadamu, huenda tatizo si kutokuwa na mwisho kwa mahitaji yetu, bali ni kutokujua ni wakati gani tunapaswa kuridhika.
Kweli umenielewa
 
Kwanza, nakubaliana nawe kwamba anayetoa dai ndiye anayepaswa kutoa sababu za kulitetea. Lakini kuna tofauti kati ya kusema ā€œMungu hayupoā€ na kusema ā€œsijaona ushahidi wa kutosha kuniaminisha kwamba Mungu yupo.ā€
Walioanza kudai Mungu yupo, wao walikuwa na ushahidi gani kusema yupo?

Utadaije kitu ambacho huna ushahidi nacho?
Mimi nikisema Mungu yupo, hoja yangu si kwamba kila kitu lazima kiwe na muumbaji, bali ni kwamba uwepo wa ulimwengu wenyewe unazua swali la msingi: Kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kwa chochote?
Utasemaje Mungu yupo bila kuwa na ushahidi na uthibitisho?
Hii peke yake haithibitishi Mungu, lakini ni hoja ya kifalsafa inayohitaji kujadiliwa. Vivyo hivyo, kutokuwa na uthibitisho wa Mungu hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.
kama kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja Mungu hayupo, Sasa thibitisha Mungu yupo.

Using'ang'anie kusema tu, kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Mpaka useme Mungu yupo, ulijuaje yupo?

Au ulijitungia tu?

Na sasa unafosi awepo kwa kushikilia point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo".

Kwa sababu huwezi kudai kitu kipo halafu huna uthibitisho.

Unafosi kitu cha kutungwa kisichokuwepo. Kwa kufanya circular reasoning fallacy.

Ukiambiwa thibitisha Mungu yupo, huwezi. Unazunguka tu palepale kwenye point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo"

Yani unatumia point hii, kama ndio uthibitisho wa Mungu huyo.

Badala ya kumthibitisha huyo Mungu yeye kama yeye bila kuzunguka zunguka.
Kwa hiyo, sitadai kwamba nimekuthibitishia Mungu kwa kuuliza swali tu. Nitakachofanya ni kutoa hoja, wewe uzichunguze na uzipinge kwa hoja. Mwisho wa siku, tunapaswa kutofautisha kati ya kile kilichothibitishwa, kile kinachowezekana na kile tunachoamini.
Kwa nini udai kitu ambacho huwezi kuthibitisha?

Kwa nini unadai Mungu yupo na huwezi kuthibitisha?
 
Wakuu, kuna swali ambalo ukilifikiria kwa kina, unaweza kujikuta una maswali mengi kuliko majibu.

Tunaishi katika ulimwengu ambao tunaona vitu, tunahesabu muda, tunazaliwa na kufa. Lakini kuna jambo moja ambalo nimekuwa nikilitafakari:

Kabla ya ulimwengu huu kuwepo, kulikuwa na nini?

Kama kulikuwa na kitu, basi hicho kitu kilitoka wapi?

Kama hakukuwa na kitu chochote kabisa, ni kwa namna gani tukafika kwenye hali ya kuwa na ulimwengu kama huu?

Na kama ulimwengu umekuwepo milele, je, ina maana kwamba haujawahi kuwa na mwanzo?

Sitaki kuhitimisha kwamba nina majibu ya maswali haya. Nataka kusikia mitazamo tofauti kutoka kwa watu wanaopenda kutafakari zaidi ya yale tunayoyaona kwa macho.

Maswali ya mjadala:

1. Je, kila kitu lazima kiwe na mwanzo?
2. Inawezekana kitu kuwepo bila kuumbwa?
3. Je, sayansi inaweza kueleza chanzo cha kila kitu, au kuna maswali ambayo yanahitaji falsafa na imani?
4. Kama kila kitu kinahitaji chanzo, je, chanzo cha kwanza nacho kilihitaji chanzo kingine?

Karibuni kwa hoja zenye mantiki. Tusibishane kwa lengo la kushinda, bali tubadilishane mitazamo na kupanua uelewa wetu.
Siti ya mbele
 
Walioanza kudai Mungu yupo, wao walikuwa na ushahidi gani kusema yupo?

Utadaije kitu ambacho huna ushahidi nacho?

Utasemaje Mungu yupo bila kuwa na ushahidi na uthibitisho?

kama kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja Mungu hayupo, Sasa thibitisha Mungu yupo.

Using'ang'anie kusema tu, kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Mpaka useme Mungu yupo, ulijuaje yupo?

Au ulijitungia tu?

Na sasa unafosi awepo kwa kushikilia point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo".

Kwa sababu huwezi kudai kitu kipo halafu huna uthibitisho.

Unafosi kitu cha kutungwa kisichokuwepo. Kwa kufanya circular reasoning fallacy.

Ukiambiwa thibitisha Mungu yupo, huwezi. Unazunguka tu palepale kwenye point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo"

Yani unatumia point hii, kama ndio uthibitisho wa Mungu huyo.

Badala ya kumthibitisha huyo Mungu yeye kama yeye bila kuzunguka zunguka.

Kwa nini udai kitu ambacho huwezi kuthibitisha?

Kwa nini unadai Mungu yupo na huwezi kuthibitisha?
Nakubaliana na hoja yako. Lakini nadhani kigezo cha kwanza ni kutotumia imani yenyewe kama ushahidi wa kuthibitisha imani hiyo. Tuchunguze madai ya kila dini kwa mantiki, ushahidi wa kihistoria, uhalisia wa madai yake na kama yanajipinga yenyewe.
 
Walioanza kudai Mungu yupo, wao walikuwa na ushahidi gani kusema yupo?

Utadaije kitu ambacho huna ushahidi nacho?

Utasemaje Mungu yupo bila kuwa na ushahidi na uthibitisho?

kama kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja Mungu hayupo, Sasa thibitisha Mungu yupo.

Using'ang'anie kusema tu, kutokuwa na uthibitisho hakuthibitishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Mpaka useme Mungu yupo, ulijuaje yupo?

Au ulijitungia tu?

Na sasa unafosi awepo kwa kushikilia point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo".

Kwa sababu huwezi kudai kitu kipo halafu huna uthibitisho.

Unafosi kitu cha kutungwa kisichokuwepo. Kwa kufanya circular reasoning fallacy.

Ukiambiwa thibitisha Mungu yupo, huwezi. Unazunguka tu palepale kwenye point ya "kutokuwa na uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo"

Yani unatumia point hii, kama ndio uthibitisho wa Mungu huyo.

Badala ya kumthibitisha huyo Mungu yeye kama yeye bila kuzunguka zunguka.

Kwa nini udai kitu ambacho huwezi kuthibitisha?

Kwa nini unadai Mungu yupo na huwezi kuthibitisha?
Hoja yako ina msingi kwenye jambo moja: kusema tu kwamba kutokuwepo kwa uthibitisho hakumaanishi Mungu hayupo, si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Hapo nakubaliana nawe.

Lakini swali la msingi ni hili: je, kutoweza kuthibitisha dai fulani kwa sasa kunamaanisha dai hilo ni la uongo, au kunamaanisha bado halijathibitishwa?

Msimamo wangu si kwamba Mungu yupo kwa sababu tu hujathibitisha kutokuwepo kwake. Ni kwamba dai la uwepo wa Mungu linapaswa kuchunguzwa kwa hoja na ushahidi wake wenyewe.

Kwa hiyo, kama unauliza uthibitisho wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba Mungu yupo, ni lazima tujadili hoja zinazotolewa kuthibitisha uwepo wake na kuona kama zinatosha. Sitadai kwamba kutokuwepo kwa uthibitisho wa kutokuwepo kwake ni uthibitisho wa uwepo wake, kwa sababu kimantiki hilo halitoshi.
 
Sasa kama sayansi imeweza kusema mambo Fulani kuhusu energy, na mwisho ikahitimisha kwamba energy can neither created nor destroyed manake, haina mwanzo Wala mwisho..., kama ni Ivo kwanini inashindwa kuelewa kwamba kuna mifumo nayo kama energy tuu, mfano huo ulimwengu wa roho, nao hauna mwanzo Wala mwisho, na huo ndo ulivofanya vingine viwe na mwanzo, ndo concept Ile ile ya energy haina mwanzo ila kupitia enyewe imedunda mifumo mengine, ya energy, kwaio mtu alisema kulikuwa na ufahamu, mwengine roho sijui lakini vyote vinaingia kwenye ishu ya kua na nguvu ya asili ambayo haina mwanzo Wala mwisho, ila kupitia hio ndo ina tengeneza mifumo mengine, Sasa Io nguvu kila mtu anaielewa kivyake watu wa dini wanaita mungu, wengine, wanaita ufahamu ni vile uelewa wako utapoishia.
 
Wakuu, kuna swali ambalo ukilifikiria kwa kina, unaweza kujikuta una maswali mengi kuliko majibu.

Tunaishi katika ulimwengu ambao tunaona vitu, tunahesabu muda, tunazaliwa na kufa. Lakini kuna jambo moja ambalo nimekuwa nikilitafakari:

Kabla ya ulimwengu huu kuwepo, kulikuwa na nini?

Kama kulikuwa na kitu, basi hicho kitu kilitoka wapi?

Kama hakukuwa na kitu chochote kabisa, ni kwa namna gani tukafika kwenye hali ya kuwa na ulimwengu kama huu?

Na kama ulimwengu umekuwepo milele, je, ina maana kwamba haujawahi kuwa na mwanzo?

Sitaki kuhitimisha kwamba nina majibu ya maswali haya. Nataka kusikia mitazamo tofauti kutoka kwa watu wanaopenda kutafakari zaidi ya yale tunayoyaona kwa macho.

Maswali ya mjadala:

1. Je, kila kitu lazima kiwe na mwanzo?
2. Inawezekana kitu kuwepo bila kuumbwa?
3. Je, sayansi inaweza kueleza chanzo cha kila kitu, au kuna maswali ambayo yanahitaji falsafa na imani?
4. Kama kila kitu kinahitaji chanzo, je, chanzo cha kwanza nacho kilihitaji chanzo kingine?

Karibuni kwa hoja zenye mantiki. Tusibishane kwa lengo la kushinda, bali tubadilishane mitazamo na kupanua uelewa wetu.
Ulishawahi kufikiria hizi emoji picha or video katika simu kuna siku moja hazikuwapo lakini unajua yupo alizebuni zikafanyika, hivyo katika ulimwengu huu hatukuako lakini yupo aliyetuumba, kifupi ukisoma biblia itakwambia kulikuwa na nchi yenye utupu na maji na giza mengine sijui natambua yupo aliyetuumba
 
Kwa nini Biblia na sio Vedas ?
 
Nimeelewa hoja yako. Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, na hakuna kilichokuwepo kabla yake. Lakini swali la kifalsafa linabaki: tunathibitishaje kwa ushahidi kwamba ulimwengu ulitoka kwa Muumba, badala ya kulichukulia hilo kama ukweli unaokubalika kwa imani? Hapo ndipo tofauti kati ya imani na uthibitisho inapoanzia.

Bwana Utam
Kwaakili yetu ya kibinaadam na ufinyu wetu wa akili (ukomo) hatuwezi kupata hilo jibu
Na sio hilo tu majibu tu ya maswali ya kawaida tu yanaweza yakatukwamisha njiani
 
Hoja yako ina msingi kwenye jambo moja: kusema tu kwamba kutokuwepo kwa uthibitisho hakumaanishi Mungu hayupo, si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Hapo nakubaliana nawe.

Lakini swali la msingi ni hili: je, kutoweza kuthibitisha dai fulani kwa sasa kunamaanisha dai hilo ni la uongo, au kunamaanisha bado halijathibitishwa?
Utaanzishaje dai bila kuwa na uthibitisho nalo?

Dai lisilothibitishwa ni uongo ndio.

Kwa sababu hata kitu cha uongo kinaweza kuanzishwa kama dai.

Na ili dai lijulikane ni ukweli, lazima dai hilo lithibitishwe kwa uthibitisho.

Dai la kwamba "Mungu yupo" halina uthibitisho mpaka dakika hii, kwa hiyo hao walio anzisha dai hili, ni WAONGO na hili dai lao ni UONGO pia.

Kwa sababu hata sasa ukitaka uthibitisho wa dai hili "Mungu yupo" hakuna mwenye anaweza kutoa uthibitisho. Ni blah! blah! tu zinatolewa.
Msimamo wangu si kwamba Mungu yupo kwa sababu tu hujathibitisha kutokuwepo kwake. Ni kwamba dai la uwepo wa Mungu linapaswa kuchunguzwa kwa hoja na ushahidi wake wenyewe.
Chochote kinachodaiwa bila uthibitisho kinaweza kutupiliwa mbali bila uthibitisho.

Mungu huyo mnayedai kwamba yupo bila kuwa na uthibitisho, tunamtupilia mbali.

kwa sababu madai yenu ni ya uongo.

Huyo Mungu mnayedai yupo, hayupo.

Mmejitungia tu madai ya uongo ya Mungu wa uongo.
Kwa hiyo, kama unauliza uthibitisho wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba Mungu yupo, ni lazima tujadili hoja zinazotolewa kuthibitisha uwepo wake na kuona kama zinatosha. Sitadai kwamba kutokuwepo kwa uthibitisho wa kutokuwepo kwake ni uthibitisho wa uwepo wake, kwa sababu kimantiki hilo halitoshi.
Nataka uthibitisho wa huyo Mungu akiwa yeye kama yeye.

Sio hoja za mara Mungu hivi, mara vile.

Leta uthibitisho DIRECTLY.

Usizunguke zunguke, Mara Mungu hivi, mara vile, mara kikapanda kikashuka.

Mlete huyo Mungu yeye kama yeye straight.

Au aje yeye mwenyewe. Kama ana huo uwezo.

Sio wewe unahangaika kumtetea huyo Mungu.

Aje yeye mwenyewe ajitetee kama yupo.

Usimtetee wewe, aje yeye mwenyewe ajitetee.
 
Sasa kama sayansi imeweza kusema mambo Fulani kuhusu energy, na mwisho ikahitimisha kwamba energy can neither created nor destroyed manake, haina mwanzo Wala mwisho..., kama ni Ivo kwanini inashindwa kuelewa kwamba kuna mifumo nayo kama energy tuu, mfano huo ulimwengu wa roho, nao hauna mwanzo Wala mwisho, na huo ndo ulivofanya vingine viwe na mwanzo, ndo concept Ile ile ya energy haina mwanzo ila kupitia enyewe imedunda mifumo mengine, ya energy, kwaio mtu alisema kulikuwa na ufahamu, mwengine roho sijui lakini vyote vinaingia kwenye ishu ya kua na nguvu ya asili ambayo haina mwanzo Wala mwisho, ila kupitia hio ndo ina tengeneza mifumo mengine, Sasa Io nguvu kila mtu anaielewa kivyake watu wa dini wanaita mungu, wengine, wanaita ufahamu ni vile uelewa wako utapoishia.
Hoja yako ina mantiki ya kifalsafa, lakini kuna jambo moja la kutofautisha: sayansi inaposema nishati haiumbwi wala kuharibiwa, haimaanishi moja kwa moja kwamba kila aina ya uwepo, kama roho au ulimwengu wa kiroho, haina mwanzo. Hayo ni madai tofauti yanayohitaji ushahidi wake.

Hata hivyo, wazo lako linaibua swali zuri: ikiwa kuna msingi wa uhalisia usiotegemea kitu kingine ili uwepo, je, inawezekana msingi huo ukawa ndio chanzo cha mifumo mingine?

Wengine wanauita Mungu, wengine ufahamu wa asili, na wengine wanajaribu kuueleza kwa dhana za kifalsafa au kisayansi. Lakini kufanana kwa mawazo hayo hakuthibitishi kwamba yote yanaelezea kitu kilekile.

Kwa hiyo, hoja si kwamba sayansi imeshindwa kuelewa ulimwengu wa roho; ni kwamba bado tunahitaji kutofautisha kile tunachokijua, kile tunachokihitimisha kimantiki, na kile tunachokiamini. Kitu kinaweza kuwa uwezekano wa kifalsafa bila kuwa ukweli uliothibitishwa kisayansi.
 
Ulishawahi kufikiria hizi emoji picha or video katika simu kuna siku moja hazikuwapo lakini unajua yupo alizebuni zikafanyika, hivyo katika ulimwengu huu hatukuako lakini yupo aliyetuumba, kifupi ukisoma biblia itakwambia kulikuwa na nchi yenye utupu na maji na giza mengine sijui natambua yupo aliyetuumba
Kuna tofauti moja mkuu: emoji au video tunajua zilibuniwa na binadamu kwa sababu tuna ushahidi wa mchakato wake. Lakini kuhusu ulimwengu, swali ni hili: je, kuwepo kwa kitu kunathibitisha moja kwa moja kwamba kuna aliyekiumba? Hapo ndipo mjadala ulipo. Biblia inaeleza imani ya uumbaji, lakini kuthibitisha kuwa maelezo hayo ni ya kweli kunahitaji hoja zaidi ya mfano wa emoji.
 
Kwaakili yetu ya kibinaadam na ufinyu wetu wa akili (ukomo) hatuwezi kupata hilo jibu
Na sio hilo tu majibu tu ya maswali ya kawaida tu yanaweza yakatukwamisha njiani
Ni kweli, akili ya binadamu ina ukomo, lakini ukomo wa uelewa wetu haumaanishi kwamba hatupaswi kuendelea kutafuta majibu. Kutokujua jibu si uthibitisho kwamba hatuwezi kulipata, wala si uthibitisho kwamba maelezo yoyote tunayoyaamini ni ya kweli. Muhimu ni kuendelea kuuliza, kuchunguza na kukubali pale ambapo bado hatuna jibu la uhakika.
 
Back
Top Bottom