a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 3,632
- 4,145
Ushahidi wa Kisayansi
Sayansi kupitia nadharia ya Big Bang na fizikia (PHYSICS) ya kisasa inaonyesha kuwa ulimwengu ulikuwa na mwanzo. (Time ,space and matter)Wakati, nafasi, na maada havikuwepo kabla ya hapo, bali vilianza kwa pamoja kwa wakati mmoja.
Sheria ya Sababu (Law of Causality):
Kila kilichopata mwanzo kinasababishwa na kitu kingine. Ulimwengu ukiwa na mwanzo wa kuwepo kwake, unahitaji chanzo ambacho kiko nje ya ulimwengu huo
Kuhusu Sifa za Chanzo Hicho (Mungu)
Kama mtengenezaji au chanzo cha hivi vitu kiliweka au kuumba space, time, na matter, basi chanzo hicho lazima kiwe na sifa zifuatazo:
1)Bila Muda (Timeless/Eternal):
Hakuna kikomo cha muda; kipo nje ya muda ulioumbwa ili kiweze kuumba muda wenyewe.
2)Bila Nafasi (Spaceless/Omnipresent): Hakitawaliwi wala hakifungiwi na nafasi (dimensions), bali kiko nje ya nafasi.
3)Bila Maada (Immaterial/Spirit):
Hakina asili ya maada au nishati ya kimwili ya ulimwengu huu, bali kina uwezo mkuu unaovuka maada.
Mtazamo huu unafanana na maelezo ya
kitabu cha
Mwanzo 1:1 ("Hapo mwanzo Mungu alizifanya mbingu na nchi"), ambapo "hapo mwanzo" kunawakilisha muda, "mbingu" zinawakilisha nafasi, na "nchi" inawakilisha maada.