Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,554
- 109,967
Hakuna wa kunichoma moto nikifa😁Unaweza kupractice sio lazima uwepo korea au japani mkuu.
Swala la imani linatoka ndani na utayari wako.
Hakuna wa kunichoma moto nikifa😁Unaweza kupractice sio lazima uwepo korea au japani mkuu.
Swala la imani linatoka ndani na utayari wako.
Hoja yako inavutia, lakini kuna jambo la kutofautisha hapa: je, energy ni sawa na ufahamu? Kisayansi, nishati ni sifa ya kimwili inayopimika, lakini haijathibitishwa kwamba nishati ina ufahamu au kwamba Mungu ni nishati. Hilo linaingia zaidi kwenye falsafa na imani.Neno energy ndiyo spirit kidini ..vitu vyote ni energy hata Mungu ni energy...sisi pia ni energy tulikuwako milele ndani ya uungu wa mungu ...uungu ni miliki yote ya energy na mungu ni ufahamu wa hiyo energy..sisi binadamu ni sehemu tu ya ufahamu ila mungu ni utimilifu wa ufahamu (nafsi)
Ukiwa na Imani linatimia mkuuHakuna wa kunichoma moto nikifa😁
Wewe Papai huna unalolijua,acha kutujazia Nzi hapa,nenda kampikie mumeo.Hakuna mtu anayejua na mwenye majibu ya kueleweka mpaka sasa.
Hata nyie Wali nazi,mchicha mwiba hamna majibu?Jambo la msingi ni kwamba hakuna mwenye jibu lenye mantiki na mashiko kuhusu hili swali mpaka sasa, labda huko mbeleni jibu litakuja kupatikana ila mpaka sasa hakuna jibu la maana kuhusu hili swali.
Kabla ya Ulimwengu kuwepo kulikuwa na Ulimwengu.Wakuu, kuna swali ambalo ukilifikiria kwa kina, unaweza kujikuta una maswali mengi kuliko majibu.
Tunaishi katika ulimwengu ambao tunaona vitu, tunahesabu muda, tunazaliwa na kufa. Lakini kuna jambo moja ambalo nimekuwa nikilitafakari:
Kabla ya ulimwengu huu kuwepo, kulikuwa na nini?
Kama kulikuwa na kitu, basi hicho kitu kilitoka wapi?
Kama hakukuwa na kitu chochote kabisa, ni kwa namna gani tukafika kwenye hali ya kuwa na ulimwengu kama huu?
Na kama ulimwengu umekuwepo milele, je, ina maana kwamba haujawahi kuwa na mwanzo?
Sitaki kuhitimisha kwamba nina majibu ya maswali haya. Nataka kusikia mitazamo tofauti kutoka kwa watu wanaopenda kutafakari zaidi ya yale tunayoyaona kwa macho.
Maswali ya mjadala:
1. Je, kila kitu lazima kiwe na mwanzo?
2. Inawezekana kitu kuwepo bila kuumbwa?
3. Je, sayansi inaweza kueleza chanzo cha kila kitu, au kuna maswali ambayo yanahitaji falsafa na imani?
4. Kama kila kitu kinahitaji chanzo, je, chanzo cha kwanza nacho kilihitaji chanzo kingine?
Karibuni kwa hoja zenye mantiki. Tusibishane kwa lengo la kushinda, bali tubadilishane mitazamo na kupanua uelewa wetu.
Huko hakuna Mapapai wenzako.Nauelewa zaidi ubudha ila nilipo sioni M-budha hata mmoja, itabidi nihamie Korea au Japan.
Agree. Nadhani hakuna kitu ni concept ya mwanadamu kuelewa anachotafsiri kuwa kipo otherwise hakuna kitu ni uwepo wa kisichoeleweka kwa mwanadamu.Hapo ndipo penyewe mkuu. 🤔 Huenda tunapouliza kilichokuwepo kabla ya ulimwengu, tunachukulia kwamba “kutokuwa na kitu” ni hali inayowezekana, wakati hatujathibitisha hata kama hali hiyo inaweza kuwepo.
Kwa sababu ukisema hakuna kitu kabisa, je, unamaanisha hakuna maada, hakuna nishati, hakuna nafasi, hakuna muda, wala hakuna hata sheria za asili? Na kama hakuna chochote kabisa, inawezekanaje hali hiyo kuwa na maana ya kuwepo?
Huenda siri haipo tu kwenye swali la nini kilikuwepo kabla ya ulimwengu, bali pia kwenye swali hili: Je, kutokuwepo kabisa kunawezekana, au kuwepo ndiyo hali ya msingi ya uhalisia? 🔥
Nakubaliana na hoja yako kwa kiasi fulani. Huenda “hakuna kitu” ni dhana iliyojengwa na akili ya mwanadamu kuelezea kutokuwepo kwa kitu anachoweza kukitambua. Lakini swali linabaki: ikiwa hakuna kitu kabisa, hata nafasi na muda havipo, tunatumia nini kuthibitisha kutokuwepo huko? Inawezekana kabisa kwamba tunapojaribu kufikiria kutokuwepo, tayari tunakigeuza kuwa aina fulani ya uwepo katika fikra zetu. Hapo ndipo fumbo linapoanzia. 🤔Agree. Nadhani hakuna kitu ni concept ya mwanadamu kuelewa anachotafsiri kuwa kipo otherwise hakuna kitu ni uwepo.
Ndiyo, lakini ningependa kusikia mtazamo wako pia. Historia ya muda inavutia kwa sababu tunajua jinsi muda unavyopimwa, lakini swali ni je, muda wenyewe ulianza lini? Je, muda ulikuwepo kabla ya ulimwengu, au muda wenyewe ni sehemu ya ulimwengu ulioanza kuwepo? Hapo ndipo mjadala unakuwa wa kina zaidi. 🤔Kwanza kabisa unajua historia ya muda?
Hata huyo unayedai ana miliki vitu vyote hivi, hawezi kutokea tu from nowhere.Mwenye kuweza kukupa majibu fasaha ni mwenye anamiliki hivi vitu vyote...
Haiwezekani vitu vikatokea tu pasipo kuwa na nguvu ya umiliki tusoijua kabisa...
Yes. Hahaha.Nakubaliana na hoja yako kwa kiasi fulani. Huenda “hakuna kitu” ni dhana iliyojengwa na akili ya mwanadamu kuelezea kutokuwepo kwa kitu anachoweza kukitambua. Lakini swali linabaki: ikiwa hakuna kitu kabisa, hata nafasi na muda havipo, tunatumia nini kuthibitisha kutokuwepo huko? Inawezekana kabisa kwamba tunapojaribu kufikiria kutokuwepo, tayari tunakigeuza kuwa aina fulani ya uwepo katika fikra zetu. Hapo ndipo fumbo linapoanzia. 🤔
Nakuelewa boss. Ukweli ni kwamba kuna tofauti kati ya kile tunachoamini, kile tunachoweza kuthibitisha, na kile ambacho bado hatukijui. Huenda tumekuta imani hizi kutoka kwa waliotutangulia, lakini hilo halimaanishi moja kwa moja kwamba ni za uongo au ni za kweli. Swali langu ni hili: je, kutokuwa na ushahidi wa kuthibitisha jambo kunatosha kusema kwamba hatuwezi kulijua, au bado kuna uwezekano wa kulielewa siku zijazo?Umeelewa nilchokwambia boss..hakuna binadamu wa kawaida kujua ukweli wa hilo.. sababu hatuna ushahidi halisi wa kujibu hiloo kwa uwezo wetu kwa sasa,ni imani tu tuliyoyakuta ulimwenguni
Najua boss. Dunia (Earth) ni sayari tunayoishi, wakati ulimwengu (Universe) unajumuisha Dunia, sayari nyingine, nyota, galaksi, nafasi na muda. Dunia ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu. Swali letu ni kuhusu mwanzo wa ulimwengu mzima, si mwanzo wa Dunia pekee. 🤝 The IcebreakerTunaishi Duniani "Earth"
Au hujui maana ya Ulimwengu na Dunia?
Special pleading fallacy.Alikuwa mwenyezi Mungu na hapakuwa na kitu chochote kabla yake,Arsh yake ilikuwa juu ya maji.kisha akaumba mbingu na ardhi na akaandika kila kitu katika dhikr (lawhul mahfudh)
Alikuwepo mwenyezi Mungu peke yake.