ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,308
- 41,055
Unalewaje ukisikia neno KUJIPENDEKEZA?
Neno kujipendekeza mara nyingi lina ladha ya dhihaka Ukisema
Fulani naye anajipendekeza sana mara nyingi unamaanisha mtu anajishusha au anajitahidi kupita kiasi ili apate kukubalika, kupewa nafasi, au kupata kitu fulani
Au apate attention
Lakini kuna tofauti kubwa kati ya upendo na kujipendekeza
Mtu anapompenda mwingine kwa dhati, huwa tayari kujitoa, kujali na kufanya mengi kwa hiari
Tatizo linakuja pale ambapo upande mmoja unapokea kwa mkono wa kukunja huku mwingine akiendelea kujituma kupita kiasi yaani unajigalagaza ila holaaaa
Mwishowe, huyo anayejitoa sana anaweza kuonekana kama anajipendekeza, ilhali labda alikuwa anaonyesha upendo tu
Kwa upande mwingine, kuna watu wanaojipendekeza wakiwa na lengo maalumu(umakini unaitajika hapa)
Wanaweza kuwa wema kupita kawaida, kukusifia kila wakati au kuwa karibu nawe kwa sababu kuna kitu wanakitaka (Akili kicwani hisia mfukoni)
Punde wanapokipata, ule ukaribu na juhudi zote huisha. Mission accomplished
Sasa swali linakuja: Unawezaje kutofautisha kati ya upendo wa kweli na mtu anayeonekana kuonyesha upendo ilhali anajipendekeza kwa sababu ya maslahi?
Kwa mtazamo wangu, upendo wa kweli huwa na uthabiti hata pale ambapo hakuna faida ya moja kwa moja upendo wa kweli haiutaji maslahi japo yakiwepo upendo hua mtamuuu zaidi
Kujipendekeza kwa maslahi mara nyingi hubadilika haraka pale lengo linapofikiwa au matumaini yanapokatika
Mtu akikamilisha akipata alichokua anakitaka anaonyesha rangi zake harisi yeye ni nani
Pia, mara nyingi mtu anayejipendekeza kwa muda mrefu huja kugundua kwamba anatumia nguvu nyingi sana kujaribu kueleweka, kukubalika au kuthaminiwa
Utajipendekezaaa ila itafika pahala utashtuka kua hutakiwi
Anajikuta anafanya juhudi zote wakati upande mwingine hauonyeshi jitihada zinazofanana Hapo ndipo mtu huanza kujiuliza Je, napenda au najipendekeza?
Vip wewe umewahi kuona mtu akijipendekeza kwako?
Wewe umewahi kugundua kuwa unajipendekeza kwa mtu? Ulifanya nini baada ya kugundua unatumia nguvu kubwa sana kujieleza na kujithibitisha? 🤔💭
ShesRise_1 Blue Monday 💙