Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Hata ukiwa na hiyo nyumba na gari hujamaliza. Nina nyumba na gari tangu nikiwa na miaka 27. Sasa nikaribia 31 lakini sina uhakika wa maisha na biashara zimekuwa zikienda vibaya sasa. Huwa napata stress nyingi pengine hata kuwazidi wasio na nyumba na gari.
 
Hiki ni kitu tofaut kamanda umekileta. Nakubal siwez ku controll uhai. Lakin hik sicho ulichokileta mezan kwenye mada kuu.

Ishu hapa namna watu wanayatazama mafanikio na kumsingizia Mungu kama sababu ya kutofanikiwa kwao, kitu ambacho sio sahihi.

Haya uliosema wewe mimi siko huko kabisa kamanda
Binafsi na kwa umri niliofikia pamoja na mapambano ya maisha naona kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ni namna umeweza kuzitumia fursa au bahati ulizopata sasa apa inategemea mtu na mtu na bahati yake wengine bahati inakuja direct kabisa anapata nafasi flani nzuri au dili flani na linampa mafanikio ya pamoja ila wengine bahati inayokuja inakuhitaji juhudi kubwa sana ili utoboe. Lakini kufanikiwa Bila kudra au Bahati useme upambane n uongo.
 
Hata ukiwa na hiyo nyumba na gari hujamaliza. Nina nyumba na gari tangu nikiwa na miaka 27. Sasa nikaribia 31 lakini sina uhakika wa maisha na biashara zimekuwa zikienda vibaya sasa. Huwa napata stress nyingi pengine hata kuwazidi wasio na nyumba na gari.
Iyo nyumba na gari kuwa nayo by 30's sio issue..Issue ni una financial freedom na nyumba na gari ulivo navo ndio ulivokuwa unavitaka kwenye izo plans zako
 
Binafsi na kwa umri niliofikia pamoja na mapambano ya maisha naona kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ni namna umeweza kuzitumia fursa au bahati ulizopata sasa apa inategemea mtu na mtu na bahati yake wengine bahati inakuja direct kabisa anapata nafasi flani nzuri au dili flani na linampa mafanikio ya pamoja ila wengine bahati inayokuja inakuhitaji juhudi kubwa sana ili utoboe. Lakini kufanikiwa Bila kudra au Bahati useme upambane n uongo.
Uko sahihi, ila hakunaga bahat au kudra tu inayokuja tu bila wewe kujihusisha kwa namna flan. Lazima uwe kwenye flow.
 
Sijui ndio ridhki ama ndio zali, bahati, uwezo binafsi au nyota ya mtu..

Ila nilichokisoma kwenye life, unahitaji mtu wa kukuinua maana hata Mungu hashuki chini kuja kukuinua ila hutumia watu.

Nimekutana na watu ambao wapo hardworking, passionate, God fearing, talented and skilled yaani wana kila sifa za kutoboa ila hawajapata sehemu na watu sahihi wa kuwainua

Halafu kuna wale ambao ni average tu na wengine ni wavivu pasee kama hawa tunaokutana nao kwenye ofisi za umma lakini wanatoboa kwa sababu wapo kwenye system lakini pia wana back up

Kwa hiyo maisha ukiyafikiria kiundani utakosa majibu ila cha msingi uishi tu
Upo sahihi ata ukiwa na talent lazima upate watu watakaiaminisha Jamii unatalent,upo sahihi kaka ila pia na maombi yanasaidia
 
Mtoa mada alishasema ana umri wa 30s na hajaelewa bado na nuda unaenda maisha hajayapatia.
Maisha hayana formula kikubwa ni kupuyanga kulingana na upeo wako wa kufikiri na connection zingine

Kwa upande wangu mafanikio nayapima kulingana na malengo niloweka kwa kipindi husika mfano

1. Nilitaka nifike chuo- nimefika(nimefanikiwa)

2. Nilitaka niwe na biashara- ninayo(nimefanikiwa)

3. Nilitaka niwe na familia- nmeoa na mtoto juu

4. Nilitaka kujenga-najenga n.k

Kwahiyo ukiangalia kwa kiasi fulani nimefanikiwa japo kila nikifanikisha hili napanga lingine na hayo ndio maisha
 
Hakuna mjanja wa kuchora fate yangu mimi.
am the only one to do that.
Mungu mwenyewe hafanyi hicho kitu.
Mungu anamuwazia mema kila mtu, na mpango wake ni kila mtu afanikiwe na aishi maisha bora yanayo reflect viwango vya utukufu wake.

Ila sasa ,bad news ni kwamba, Mungu anawapa watu wooote same ground ya kupambania ili kuyafikia mafanikio.

Pambana wewe.. Lala wewe. Hapo Mungu anakaa kando kuwaangalia wajuz wa kufuata principles and systems za ku unlock secretes of riches.

Success is predictable , so as Failure
Nime andika kwenye karatasi. Baadae nika vutie tumbaku.
👉Huenda vita niingia Ivan Stepanov
 
Sijui ndio ridhki ama ndio zali, bahati, uwezo binafsi au nyota ya mtu..

Ila nilichokisoma kwenye life, unahitaji mtu wa kukuinua maana hata Mungu hashuki chini kuja kukuinua ila hutumia watu.

Nimekutana na watu ambao wapo hardworking, passionate, God fearing, talented and skilled yaani wana kila sifa za kutoboa ila hawajapata sehemu na watu sahihi wa kuwainua

Halafu kuna wale ambao ni average tu na wengine ni wavivu pasee kama hawa tunaokutana nao kwenye ofisi za umma lakini wanatoboa kwa sababu wapo kwenye system lakini pia wana back up

Kwa hiyo maisha ukiyafikiria kiundani utakosa majibu ila cha msingi uishi tu
Uko sahihi Sana bro Eyce majuzi Kuna madogo want pata deal ya kusambaza sukari.
👉Imagine Wana pewa kwa Bei kitonga, ila wanavyo gonga people sio mchezo
 
Nakumbuka Jamaa mmoja shule nilimuuliza vipi milioni 80 unapiga kalamu chini na kuacha shule akasema hata milioni 100 hawezi kuufanya huo ujinga.
Kwa kipindi kile milioni 100 ilikuwa pesa haswa.
Jamaa kweli kapiga one Form four na six kapiga one pia kasoma UDSM ila sasa maisha yanamkimbiza kama alivyokuwa anayakimbiza masomo.
🤣🤣🤣🤣
Kaka nipeni laki 1, nawa choma na ma teacher kabisa😂😀
 
Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.
Sijui kwa watu wengine ila marafiki zangu wengi walioweza kufanya vizuri hadi chuo kikuu wengi zaidi hata ya 70% wana maisha mazuri kiuchumi. Vipanga karibu wote niliosoma nao wako njema. Na wale waliokuwa hawazingatii shule wengi wao hawako vizuri ni wachache waliobahatika kutoboa. Ingawa bahati zinahusika ila ni muhimu kupambana ili kama bahati itakuja ikukute uko tayari kwenda nayo sambamba. Kuna mdogo wangu alihitimu UDSM 2019 akakaa bila kazi hadi mwaka jana mwishoni bahati ya scholarship Ulaya ikamjia. Ile bahati ilikuja kwasababu dogo GPA yake ilikua safi na pia ni mtu mwenye nidhamu.
 
Nilipokuwa kijana mdogo niliona wenye miaka 30 ni wakubwa kweli kweli, baada ya kuifikia nikaanza kuona ni wadogo kweli kweli.

Miaka 40 kama sifa ya kugombea urais nchi hii niliona ni umri mrefu kweli kweli.

Sasa nimebakiwa na LIFE BEGINS AT 40, kikubwa uhai tu.
Semenya wa ukaldayo unashusha nondo za hatariii na kutema madini ya uhakika yaliyojitosheleza.
 
Habari za Jumapili!

Maisha sio Pouwa! Nakubaliana na wale wanaosema Maisha ni majaliwa. Na jitihada hazizidi kudura.

Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.

Ilifika hatua wakawa wanadharau wale ambao walikuwa wanaonekana hawana mipango na mikakati kutokana na kutoipenda shule.

Wengi walifikiri kuwa kabla ya miaka 30 tayari wangekuwa wamekomesha jeuri na kiburi cha Umaskini katika maisha yao.
Tayari kichwani walikuwa na picha za jumba kubwa la kifahari ambalo walijua ndio watakayoishi. Bongo zao zilishakuwa na miundombinu ya flyover ambapo gari yao ilikuwa ikipita juu yake huku ndani akiwa yeye na Pisikali moja matata ambayo ndio mkewe.

Kwa wasichana, wao nao walikuwa na maisha yao mazuri katika vichwa vyao. Wanaume Handsome, warefu na wenye vipato na Watanashati walikuwa katika fikra zao.

Sasa miaka imekimbia, hawaelewi nini kimetokea. Matumaini yameyoyoma, ngumi ya matumpa upper cut moja matata imepiga kidevu vijana chali.
Hata zile ramani za majengo na magari walizokuwa nazo miaka hiyo zimefutika.

Yule Mwanamke mrembo akilini waliyemfikiria wangekuja kumuoa wanawaona kwenye magazeti, filamu na kwenye riwaya. Hakuna faraja tena, tumaini limeota mbawa. Wamejiunga kwenye chama cha faraja ya mpito cha Kataa Ndoa.
Hawakumbiki tena ndoto ya kuwa na familia bora baada ya kuyapata maisha mazuri yanayotamanika.
Ni Tekniko Knockout.

Hawakujua kuwa maisha yanakupa yale ambayo hujayaomba na yale ambayo huyataki. Tena maisha hukupa yale ambayo hukudhania kwamba ungekuwa nayo. Kwa sababu maisha ni Nasibu, maisha ni bahati tuu.

Sasa mipango imevurugwa na kuvurugika. Kila kitu pangala pangala! Hata kupanga hawataki kupanga tena. Hata wakisema wapange wanaona wanapoteza muda wao. Sasa ni bora liende túu! Wapo tayari kwa lolote na huo ndio mfumo wa maisha unavyotaka.

Mtu ambaye alipanga kabla ya miaka 30 awe na jumba na gari leo hii hata kodi ya chumba cha laki moja hawezi kuhimili. Unaweza kuona pigo alilopigwa ni zito kwa kiwango kipi.

Kijana, unapopanga mipango yako. Muombe Mungu

Suleiman aliwahi kusema;

Mhubiri 9:11 NEN​

Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.

Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom