Kabla hujafika Dar es Salaam, ilikuwa ukisimuliwa habari zake ulikuwa unajenga picha gani kichwani?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
570
1,229
Habari wana JF,

Binafsi kabla sijafika Dar nilikuwa na picha ya tofauti kidogo kichwani hasa ubungo na wakati huo anayekusimulia ametoka Dar eti amesahau hadi kilugha si unajua wanyakyusa tena kwa mbwembwe ndizi alianza kuuliza eti zinaitwaje kilugha? na amekuja na mikate ile mikubwa huku anakusimulia habari za ubungo bus terminal wakati ule.

Sasa siku nmefika, tena siku hiyo nilikuta mvua imenyesha. Nilichokuwa nakiwaza kuhusu Dar na nilichokikuta ilikuwa vitu viwili tofauti, zaidi nilifika keko madawa alipokuwa akiishi rafiki yangu yaani nilichoka, nikagundua kumbe kinaigizwa Maisha ya uswazi kwa movie ni real vile vyoo vya kuoga humohumo unaoneka nusu, nusu umejificha.

Hakika nikagundua Dar ni chuo cha Maisha. Wewe ulikuwa na picha gani ( mental picture) kichwani kuhusu Dar?
 
Zamani Wakati Mkoani kuko hoi Kwa Kila kitu ilikuwa ukienda Dar kweli unashabgaa maana unakutana na vitu ambavyo havipo Mkoani.

Ila Kwa Sasa Mkoani labda hakuna watu wa upinde tuu ila vingine vyote vipo.
DSM bado vitu kibao vipo ambavyo inabidi uvifate
  • Bandari kuu
  • Mpira utaziona timu 3 bora za Tanzania pamoja na mashindano ya kimataifa
  • Burudani ya muziki wasanii karibu 95% wenye majina wapo huku
  • Kariakoo soko kubwa zaidi wafanyabiashara wa mikoani wanajumulia huku
 
Niliafikiri.maisha ya dar ni kama nilivyokuwa naona kwenye movier za rambo na chucknoris, huko hakuna shida ya maji,wala umeme, watu wanishi magorofani tu, hakuna vumbi, daaah ,nilipofika kibaha nikaanza kuchoka
 
Daslam bhana watoto wa huku na zile ongea zao za mwana vipi una mizinguo kibao.
 
Kuna jamaa alipita na basi Dar akiwa anaelekea Lindi kutokea Shinyanga, yaani ile kupita tu hadi leo anaongea kidaslamu.
 
Nilidhani dar nzima inafanana na posta au makumbusho kumbe dar ni kijiji chenye magari mengi na vibanda vyA mpesa
 
Sikuwa na picha kichwani wala excitement, wazazi wangu waliposeparate sikutaka kuishi na mmojawapo so miaka yote nilikuwa either kwa aunt, mjomba, bibi ama mamkubwa. Baada ya sekondari ndio nikaja kwa mzazi. Ile nafika stendi tunapanda daladala nikashangaa watu wengine wanasimama, nikajua traffic atawashusha tulipomfikia nikaona hana habari anaongea na konda.

Ile nimekaa kidogo pembeni yangu kuna mbibi nilimuona anasoma gazeti mikono ina makunyanzi, nikataka nimsalimie nikamtazama nikaona ana wigi rangi damu ya mzee ila mbibi amejichubua, alafu ana wanja na kapaka rangi mdomoni 💄. Nikasahau kumsalimia, ile napiga jicho kwenye gazeti nakuta ni la udaku ilikuwa page inamtaja Wema Sepetu. Nilishangaa mbibi anasomaje habari za Wema.

Sikuwa impressed kabisa na watu wengi wa jiji.
 
Asilimia 70 yawatu wa mkoa wa manyara hawajawai toka mkoani kwao
Hahaaa hii kitu mbona inanikumbusha kitu,kipindi niko chuo kuna mzee mmoja wa manyara alikua inservice alikua ananiuliza ukifika pale segera dar unaelekea upande gani
 
Nilijenga picha kuwa mabomba yanatoa maziwa na nilidhani asali inapatikana bure
 
Back
Top Bottom