Kabila teule.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabila teule....

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Kijakazi, Mar 12, 2008.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kuhusu kabila teule hapa naongelea WACHAGA, mimi ninafikiri au ninapendekeza kuwa hili kabila lipewe haki ya kikatiba ya kutawala Tanzania ktk nyanja zoote za nchi yetu kwa muda fulani...ili waweze kufundisha makabila mengine kuhusu mambo ya kimaendeleo.. pendekezo langu hili linatokana na utafiti wangu (wa kienyeji /sio rasmi) nilioufanya kuhusu hawa watu na kungundua kwamba wana utamaduni tofauti sana ukilinganisha na makabila mengine ya nchi yetu, na utamaduni wao umeelekea zaidi ktk mambo ya kimaendeleo kuliko makabila mengine mfano mdogo tuu ni kwenye elimu wakati wa nyerere ambaye hakuweza kujenga shule yeyote ile ya sekondari ktk kipindi chote alichokaa madarakani, lkni hawa watu wachaga walikuwa wanajenga shule za wazazi ambapo wazazi walikuwa wanalazimka kuchangia na matokeo yake tuliyaona kwamba pamoja na siasa za nyerere watu hawa bado walifanikiwa sana ktk kujenga shule nyingi... pia kingine ni mafanikio ya hawa watu ya kimaendeleo popote pale walipo ktk nchi yetu, kwani ushahidi wangu unaonyesha kwamba ktka kila ncha ya nchi yetu niliyotembelea na niliwakuta hawa watu kuanzia nyumbani asilia kwa wazazi wangu tabora vijijini mpaka sumbawanga na kila nilipowakuta walikua wamefanikiwa zaidi kuliko wenyeji kimaendeleo na woote tunawaita mangi...
  Pia ukienda mkoa wao kwa kweli unavutia jinsi ulivyopambwa kwa maua mazuri hata vijijini kwao wameweza kujenga nyumba bora pamoja na miundo mbinu imara ukilinganisha na makabila mengine.. kwa hiyo kutokana na hiyo mifano michache mimi nafikiri kuna kitu maalaumu ambacho hawa wau wanacho na makabila mengine wamekosa na hivyo naona haitakuwa vibaya kama tukiwabidhi nchi na kutufundisha utamaduni wao kwani unaonekana ni wa kimaendeleo.....
   
 2. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  okay...here we go.......
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hizi ndoto zingine bwana..........mods..........please do the needful....nafikir hii itafaa kuleee kwenye maoni au habari mchanganyiko
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Jina lako limebeba maana nzima ya kwa nini umekuja na bandiko hili...
   
 5. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele..... Ogah, au labda waieweke kule kwenye "Udaku/Jokes" manake duh siasa na Uchaga, kaaz kweli kweli JF mwaka huuu

  Kija.....No offense intended Mkuu, lakini..........
   
 6. S

  Semanao JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mimi sijawahi kuona utafiti usiokuwa na FACTS and FIGURES. Ninachokiona hapa ni maneno ya kijiweni. Weka comparative figures ku-authenticate your arguments.
   
 7. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Kijakazi,

  Mimi ni msukuma. Kwel ulichokiongea mimi sijakifanyia utafiti kama wewe lakini siwezi kuku dismiss kwamba unaongea uongo au unaendekeza ukabila.

  Nadhani wote ambao hawakubaliani na wewe wakuchallenge kwa hoja zao na sio kukimbilia kuhamisha thread.

  Ila kwa haraka haraka, naweza sema ni kweli wachagga wengi ambao nimekutana nao na wengine washkaji zangu ni hardworking sana kuliko baadhi ya ndugu zangu wasukuma na nadhani mafanikio yako synonimous na kufanya kazi kwa bidii! Ni mara chache mwanafunzi anayekesha akisoma amebandika miguu kwenye karai ya maji ya baridi akaambulia zero! Hilo liko wazi. Ila nadhani kuna makabila mengine vile vile yanajitahidi kupiga kazi sema tuu..unakuta jamaa ndo kasoma kijiji kizima...huo ni mtihani mwingine...


  Anyway labda umeiweka hii thread si mahala pake..lakini kuna ukweli wa aina fulani katika uliyoyaandika.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tulishaambiwa tutakula nyasi bali ndege ya raisi inunuliwe iyo stm itaniuma mpaka kufa.

  Hii inaonyesha jinsi gani uyu mtu asivyojari utu bali ni fedha tuu.

  Kwa maendeleo nawasifu ila sometimes wamekuwa extremist kt suala la hela.

  Unakuta mchaga kazimia kisa njaa ukisachi mfukoni ana laki ati ukiuliza mtaji..........am kidding
   
 9. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kijakazi:
  Utafiti wako haujakamilika. Mbona hujafika kule Mbeya/Iringa? waliko wafanya biashara hodari ambao sio wachaga?

  Je, Masai nao wawe kabila teule basi kwa vile ni hodari wa ufugaji; na wakerewe (uvuvi); na wazaramo (minazi), n.k.
  Nadhani Watanzania wote ni taifa teule kwa ujumla wake!

  Hatuhitaji kugawanywa vipande vipande tena. Tuendelee kuimarisha utaifa wetu kwa kila mmoja wetu kwa kuchapa kazi kwa nguvu na maarifa kwa maendeleo ya taifa letu.

  Hebu tuwekee mjadala mwingine unaotuunganisha zaidi kuliko huu unaolenga kutugawanya.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo mwenye nacho aongezewe sio?
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tukienda hivi patakuwa hapatoshi. maana tutadai mengi usultani urejeshwe maaana nao ulikuwa na nguvu zaidi na maendelelo makubwa.

  wengine watadai uchifu wengine watataka watu wa kabila fulani wahame ili wao wakamate eneo lao maana kurudi kwao nyuma ni kabila fulani.

  fikra kama hizi ktk tanzania ilio huru hazina nafasi. akaungane na watu wa kongo kule wenye kudai sijui dola gani lirejeshwe na mipaka ivunjwe kongo na afrika ya kati na nchi za pale ziungane warejeshe utawala
   
 12. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Hili ni jambo moja na kijinga kuliko lote nililowahi kusikia . Kabila teule maana yake nini ? Kwanza nani kakwambia kuna kabila la kichagga? Unajua tofauti na makabila mengine ndani ya wachagga hawazungumzi lugha moja . Kuna lugha zaidi ya 30 mule ndani ...mfano wachaga wa Machame, Rombo, Marangu , Kibosho n.k lugha zao ni tofauti kama kichina na kijapani . Ssa unapozungumzia wachaga ni vizuri kusema unazungumzia wachaga wa wapi.

  Lakini jambo la msingi hapa ni kuwa hii topic ni ya kijinga na ambayo hiko too stereotypical.
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  nipo nawe Mkuu Rufiji,
  kabila teule? unataka kuleta uhutu na utusi? kwani wachagga hawapo madarakani? je wachagga wote waliopewa madaraka wanafanya vizuri? (msikilize sasa Njowepo anasema nini juu ya ununuzi wa ndege ya Rais).

  fikra za kikabila/kibaguzi ni fikra finyu ktk ulimwengu wa sasa. damn to hell
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tuanze na kuwarudisha wakoloni kwanza maana kipindi cha ukoloni kulikuwa na maendeleo na ufisadi haukuwepo.

  Kule south nao warudishe makaburu hao akina Mbeki na Zuma hakuna lolote magumashi matupu...
   
 15. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JF kweli kuna demokrasia, yaani Kijakazi naye anakuja na hoja kama hii na kuna watu wanamjibu kwa hoja tena nzuri tu zilizoenda skuli..!!
   
 16. Bangusilo

  Bangusilo Senior Member

  #16
  Mar 13, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  This Absolutely ridiculous, who are the chaggas by the way, like other Bantus right?, this will create more tribalism, and even bring cast system. Aryan started the same way. The only solution is to give equal opportunity to all.
   
 17. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kijakazi jina lako na maoni uliyotoa vinawiana kabisa, kijakazi maana yake "housegirl" umetumwa ama wamekununulia nguo za sikukuu??????? ukawa umefurahi kupita kiasi. TANZANIA HATUTAKI UKABILA AU KABILA FULANI KUTUKUZWA KAMA ULIVYOAHINISHA. MFANO HALISI NI KENYA NASHANGAA TAYARI UMESAHAU KWAMBA MAPIGANO YALIYOZUKA KENYA YALICHOCHEWA ZAIDI NA UKABILA, YAANI KATI YA KABILA KUBWA LA WAKIKUYU NA JINGINE KUBWA LA WALUO. USITURUDISHE HUKO KAMA UMEPENDA SANA BASI OLEWA HUKO ILI NAWE UWE "INDUCED"
  Mnazungumza makabila, dhambi ya ukabila ni mbaya sana. Dhambi ya makabila haina mwisho, ni sawa na kula nyama ya mtu huwezi kuacha... Mwl. J K Nyerere
   
 18. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Siyo siri yaani hata kama tuna uhuru wa kuandika chochote ni muhimu sana ukatafakari kabla ya kurusha hewani. Kwa kuwa hapa JF hakiharibiki kitu nadhani anajuta kwa maandishi yake MACHAFU YASIYO NA MAANA. NI MUNGU TU ALILITEUA TAIFA TEULE YAANI ISRAEL LAKINI SI HUYU "HOUSEGIRL" kuteua kile anachokiita kabila teule
   
 19. k

  kamtu Member

  #19
  Mar 13, 2008
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nakubaliana na nyie kabisa kwambahoja haina msingi tena haifai lakini ili kumtendea haki aliyoileta mngeiweka kwenye maoni, mapendekezo etc na si kwenye jokes, i dont think this is a joke anyway. Wakati kule kwenye jukwaa la siasa kuna thread inayosema ngoma london na ipo imetulia tuli wakati si mahala pake kabisaaaa.
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  wakuu
  mnarushiana maneno bure kwani mtoa hoja ameanzisha moto halafu huyoooo kaingia mitini, Tuuzime moto badala ya kuuchochea, simple as ignore the topic and concentrating with major issues which squeezes our country.
  This ukabila thingies ni just as kuishiwa fikra na ni hoja ya kipuuzi...
   
Loading...