JWTZ na Polisi mna ugomvi gani usioisha!

JWTZ na Polisi mna ugomvi gani usioisha!

Usilolijua ni kama usiku wa giza totoro. Kama hujui tofauti ya majeshi hayo, utabaki na umbumbu wa kudumu lkn ikiyajua, utagundua kwa nini wanatifuana na kwa nini isiwe zima moto na magereza.

Viapo vya kazi zao ni tofauti sana. Wakati jwtz wanaapa kulitumikia taifa katika kulinda mipaka ya nchi, polisi wanaapa kusimamia sheria(objectivity) na kulinda raia na mali zao.

Kwa imani yangu, polisi aliyeiva hata akiwa na msuli kiasi gani, kama anajitambua, hapaswi unyanyua mkono ili kumpiga mtu, labda kujilinda tu. Polisi anakupiga na sheria anayoisimamia wkt jwtz kwake ni fahali kupigana.


kisheria jeshi linajifunza kulinda na kutumia nguvu kubwa ndani na nje ya mipaka ya nchi, na ndio maana unaona serkali inaghalamia silaha kubwa kwa sababu ya jeshi la wananchi,

police wanajifunza kulinda mali na laiya kwa kushirikiana nao na pia ikiwezekana kuwapa elimu laiya hao hasa jinsi ya kuacha uhalifu na kuwaficha wahalifu hata akiwa mwanao, sasa cha ajabu police huyohuyo badala ya anapo muona mtu amekosea kidogo tena mtu yule anaomba hata msamaha kwa kutokujua alichofanya yeye anamkokota, tena mbaya zaidi unaweza kuona yule mtu anaekokotwa kweli ni mtu wa shida lakini anaweza kumwambia waanbie ndugu zako waje wakufuate,watu wanajichanga ile hela ya chakula anaenda kumtoa ndugu yake, nao wanaipokea bila ya huluma na kuelimisha kua mtu hapaswi kuchukuliwa dhamana kwa kutoa pesa labda.kunavitu tu vya kuleta apewe dhamana.

ww ukitaka uamini kua police hawawaelimishi laiya ipasavyo, hebu fanya uchunguzi mdogo tu! police ili amkamate mtu anatakiwa ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisha,ampe namba yake, na kituochake cha kazi, laki malanyingi hawafanyi hivyo, wanampeleka mtu kituoni na hata ukimuuliza police aliekupeleka kituoni nani unakuta hamjui. huoni kunashida ya laiya kutopata elimu vizuri!
 


....

....Hiii fani nyingine kabisaaa sio ya virungu


Peruvian-Army-610x459.jpg
 
Tatizo Tanzania nchi ya amani wanajeshi wana miss kupigana.. ndìo maana wanajinoa kwa polisi.
 
Kiboko yao wavaa kofia nyekundu (FFU) ....labda Komandoo lakini JWTZ wa kawaida hasogei kwa mvaa kofia nyekundu ...
hao wenye nyekundu hamna kitu labda wakupambana nae ni km Wa magereza mtaani wanachapika hao kofia nyekundu wako
 
....

.....unavalishwa tairi la scania shingoni then Kilometa ishirini zinakuhusu bora kusikia tu !!!

F2013111413170478567200000.jpg
 
Upo nyuma sana mkuu. Darasa la saba ilikuwa ni enzi za mwalimu, ambao wengi sasa hivi wamestaafu au wamebaki kidogo sana.

Sasa hivi askari ngazi ya chini qualification ni form four na huu utaratibu una muda mrefu tu.
Maafisa wa jeshi qualification ni degree ya kwanza, na wale walioajiriwa wakiwa na elimu ya form six wengi wamejiendeleza kielemu.
Na pia mishahara ya wanajeshi imeboreshwa ni ya kuridhisha, zamani walikuwa hawana uwezo wa kukopa kutoka taasisi za kifedha ila sasa hivi wanakopesheka, hata askari wa ngazi za chini maisha yao yameboreshwa si kama zamani.


Tuwe tunaongea vitu ambavyo tuna uhakika navyo na si kupotosha.

Mi nadhani tujadili tabia zao ambazo kweli haziridhishi. Ni wababe pasipo sababu.
Mwambie aende kama la saba huko JKT aone kama atapata nafasi kirahisi nadhani hata form for, kuanzi 27 ndiyo huchukuliwa sasa je kuna wangapi wenye 25 nimeona ivi amshawahi kuona umati wawatu kwenye ofisi za wakuu wa wilaya wanaofukuzia kwenda JKT.
 
Poa mkuu wapo vizuri, je, operational order wanapokea kutoka KDF au Police force wawapo kwenye mission?
Je KDF wanavikosi vya komando au hakuna? Ntafurahi ukinijib mkuu

Saguda47
Kwa vile shughuli zao ni kwa ajili ya usalama wa ndani ya nchi hivyo amri wanapata kutoka kwa wakuu wa polisi. Japo wana bajeti yao maalum, sasa hivi wana hadi chopa zao kadhaa. Hii hapa video wakiwa kwenye mafunzo


KDF pia wana special force commandos ambao wanahusika sana sana kwenye operations za kijeshi. Wapo kule Somalia na ndio snipers. Hii hapa video kuhusu KDF special forces
 
ni kwamba, kiutawala, JWTZ ni maboss wa askari, hata kiweledi tu na kila kitu. sasa polisi hilo huwa hawataki kukubali, wanataka na wao waonekane wa maana na wana nguvu na heshima kama ile wanayopokea JWTZ. hao wanajeshi wanakuambia polisi ni raia wakakamavu tu wala si askari, kwao ni kama mgambo tu.
Nani kasema kuna mtu anamzid mwenzie heshima?wote ni askari na kila mmoja ana majukumu yake kiutendaji.heshima ni sawa
 
MMOJA ANALINDA MIPAKA YA NCHI ISIVAMIWE NA MAADUI,mmoja analinda usalama wa raia ndani ya nchi. MMOJA MKUBWA,mwingine mdogo......
kuna nchi moja yalifanyika mapinduzi wanajeshi wakatangaza 'kuanzia sasa polisi wote ni raia' ikabidi polisi wafiche nguo na kukimbia kambi zao. kwa ujumla wote wanafanya kazi zao vizuri ila kuna baba na mtoto. nilihudhuria mazishi ya generali mmoja, wakati wa kupiga mizinga ya heshima hawa wa 'ndani' tulijaa nao hofu kwa mingurumo!!
Mkuu nazan majenerali wote wapo hai sasa sjui ni jenero gani huyo? Alafu kama ni meja jenero au brigedia jenerali zitalia risasi idadi kulingana na cheo chake.iyo mizinga ni ipi mku?
 
mkuu utawaponza hao wenye kofia nyekundu unaowasema mana wataanza kupigwa kushinda hawa wengine.ngoja hii comment waione jwtz halafu usikie kesho pale madafu ukonga kumetokea nini.watafuatwa mule mule
FFU ni high trained personel pia wana special force ya police comando .sema hawajawai kupata field ya kutoa weled wao wote zaid ya kutawanya raia
 
Wanajeshi hawana akili
Kwa coment kama hii unajiabisha mkuu, mwanadam akizaliwa tu anaujazo wa akili CC 50, hii cc 50 sawa na ujazo akili ya nyani mkubwa. Akili ya mwanadamu huongezeka kadiri anavyokuwa na akifika umri fulani hukoma, sasa ukisema hawana akili sijui unamaanisha nini, sidhani kama wewe unaakili nyingi kuliko wanajeshi walioko jeshini, sijuwi unamaanisha hawa wa kwetu tu, Duniani kote. Kitendo cha kujiunga na jeshi lazima akili itumike, kumkabili muhalifu/ adui akili hutumika pia. Inawezekana mtu akapata tatizo la akili, maana kuna maradhi ya akili, zitapungua tu na siyo kukosa kabisa akili labda kijiti ndicho hakina akilli.
 
Kwa coment kama hii unajiabisha mkuu, mwanadam akizaliwa tu anaujazo wa akili CC 50, hii cc 50 sawa na ujazo akili ya nyani mkubwa. Akili ya mwanadamu huongezeka kadiri anavyokuwa na akifika umri fulani hukoma, sasa ukisema hawana akili sijui unamaanisha nini, sidhani kama wewe unaakili nyingi kuliko wanajeshi walioko jeshini, sijuwi unamaanisha hawa wa kwetu tu, Duniani kote. Kitendo cha kujiunga na jeshi lazima akili itumike, kumkabili muhalifu/ adui akili hutumika pia. Inawezekana mtu akapata tatizo la akili, maana kuna maradhi ya akili, zitapungua tu na siyo kukosa kabisa akili labda kijiti ndicho hakina akilli.
Mkuu jkt mafunzon tuliambiwa ivi 'jeshi ni kundi la wajinga linaloongozwa na mjinga mmoja ambae ni mwamunyange' pia wajeda uwezo wao wa kufikiri ni mdogo kulingana na depo na mazingira ya kazi .
 
Mkuu jkt mafunzon tuliambiwa ivi 'jeshi ni kundi la wajinga linaloongozwa na mjinga mmoja ambae ni mwamunyange' pia wajeda uwezo wao wa kufikiri ni mdogo kulingana na depo na mazingira ya kazi .
Sasa nawe pia ni mjinga, maana ulikubali kudanganywa, maana ya ujinga ni kutojua na si kukosa akili, kumbe baada ya JKT ulijiunga na polisi, na haya unayoyandika hapa ni mwendelezo wa huo ugomvi wenu? Mimi siku zote najua polisi, JWTZ, Magereza, Zimamoto, JKT yote ni majeshi, ukisema jeshi tu unamaana unajumuisha majeshi yote, ila mpaka useme jeshi la ndipo utakuwa umetenganisha.
 
Jwtz kiuhalisia ndo kila kitu katika suala la usalama, jiulize kwanini mkuu wa majeshi (CDF) Mwamnyange ndio anaekaa na rais kwenye gari ya maalum ya wazi... Kwanini IGP asikae nae kwenye hilo gari? Pia kwanini bodyguard wa rais maranyingi anatoka JWTZ. na sio polisi? Hivyo jwtz ni wakubwa kwa polisi kulingana na majukumu yao.
 
Back
Top Bottom