JWTZ na Polisi mna ugomvi gani usioisha!

JWTZ na Polisi mna ugomvi gani usioisha!

jwtz kwa jinsi alivyo jifunza anauwezo wa kumfahamu askari yeyote hata akiwa kwenye daladala, na vilevile anaweza kumsaidi mtu akiwa na shida kwa moyo mmoja, tofauti na police wao pesa mbele na akiona mtu kakosea hata kidogo na kwa kutokuelewa kwao kwa kushindwa kuwasoma watu, ndio maana wakati mwingine police wanawakamata hata wakubwa wao na ananga 'anga 'anua kutengeneza mazingila ya rushwa matokeo yake anakuta anaomba rushwa kwa bosi wake kinanuka, askari anatakiwa kuwa smart, unamsoma mtu alivyo na anavyoongea na anavyokujibu unapomuuliza swali tayari unatakiwa ujue mtu huyo ni wa aina gani. SASA KINACHO WAPONZA POLICE NI ILE TABIA YAO YA ANAPO MPATA MTU NA KOSA ANASHINDWA KUMSOMA, ANAPOTENGENEZA MAZINGILA YA RUSHWA ANAKUTA KUMBE MJEDA, NA MJEDA HATAKI UONEVU ANAKUTA ANAPIGWA. ah! police kunavitu vya ziada wanatakiwa kujifunza au kufundishwa la sivyo kila siku watadhalilishana tu.

mmmh! hivi kuwa mjeda au wew unaamini mjenda ana nguvu za kjmpiga kila mtu achilia mbali na kumpiga polisi?
 
Jwtz kiuhalisia ndo kila kitu katika suala la usalama, jiulize kwanini mkuu wa majeshi (CDF) Mwamnyange ndio anaekaa na rais kwenye gari ya maalum ya wazi... Kwanini IGP asikae nae kwenye hilo gari? Pia kwanini bodyguard wa rais maranyingi anatoka JWTZ. na sio polisi? Hivyo jwtz ni wakubwa kwa polisi kulingana na majukumu yao.


bodyguard wa rais anatokana na matakwa ya rais na mapendekezo ya usalama wa taifa..nyerere alikuwa analindwa na bodyguard wa kutoka polisi..alagu rais kukaa na CDF ni utaratibu tu.
 
wanajeshi hawataki kuwatii askari polisi,wanawadharau sana sometimes wanajeshi wanakuwa na nguo za kiraia na wanafanya kosa,askari polisi akitaka kutimiza wajibu wake kisheria bhas atapata kipondo (nimesema mjeshi akiwa kavaa kiraia,kwa sababu najua akivaa gwanda askari polisi hawez fanya chochote)
Sema polisi ni waoga tu, hawawezi kudiriki kusimamisha gari la jeshi hata kama kuna makosa masikini, wanaogopa kichapo
Mkuu hata mimi nimeshawahi kukumbana na kadhia yao enzi hizo kabla ya simu za mkononi, nilikuwa mkoani huko, nikakatiza nyumba ambayo askari mmoja anademu wake. Nyumba ile ilikuwa na uwa wa miazi (bambuu) kwa wenyeji wa Nachingwea wanaijua uwa za aina hii, sasa yule asikri alitaka demu ajue yeye tayari yupo nje, alichofanya ni kunikamata mimi kwanini natembelea baiskeri isiyo na taa. Ni kweli baiskeri haikuwa na taa, ila kwa Nach, kipindi hicho hilo sio kosa, maana usafiri mkubwa ulikua ni baiskeri na hata hao polisi walitembelea baiskeri ambazo pia hazina taa. Na mbaya zaidi baada kunikamata wengine walikuwa wanapita bila taa hata kuulizwa kitu, walipojaa watu na wale mademu zao wakaja, wao ndiyo waliotuachanisha ugomvi ule askari walikua wawili.

Na jwtz wanao vaa kofia nyekundu je? Yaani MP. Nao wanachapika na hao FFU?
 
bodyguard wa rais anatokana na matakwa ya rais na mapendekezo ya usalama wa taifa..nyerere alikuwa analindwa na bodyguard wa kutoka polisi..alagu rais kukaa na CDF ni utaratibu tu.

Huyo bodyguard anaitwa nani? Halafu kwani bodyguard wa rais ni mmoja?
 
Saguda47
Kwa vile shughuli zao ni kwa ajili ya usalama wa ndani ya nchi hivyo amri wanapata kutoka kwa wakuu wa polisi. Japo wana bajeti yao maalum, sasa hivi wana hadi chopa zao kadhaa. Hii hapa video wakiwa kwenye mafunzo


KDF pia wana special force commandos ambao wanahusika sana sana kwenye operations za kijeshi. Wapo kule Somalia na ndio snipers. Hii hapa video kuhusu KDF special forces

wanajeshi wa Kenya niliwadharau sana walivyowashindwa kuwakamata wale jamaa waliovamia west gate
 
Hapakua na fursa ya kuunda joint command, ndio ilikua mara yetu ya kwanza kuvamiwa na magaidi waliongia kwenye jengo na kuanza kuua kila asiye muislamu. Ikawa kila kikosi kufanya mchakato wa kufika pale haraka iwezekanavyo, kwa vile makomando huwa wamesubiria matukio kama haya, wao walifika mara moja na kutathmini ngoma ilivyo, wakabuni fasta mkakati wa kufunga kitabu kwa dakika thelathini na wakaanza shughuli kishujaa na kikomando.

Ghafla KDF wakaingia kwa vurugu na ubabe, maana wao wamefunzwa kupiga bila kukamata. Kwa bahati mbaya wakampiga askari mmoja ambaye alikua kiongozi wa wale makomando, alikua anaongoza jeshi lake kwa mbele. Pakaibuka majibizano na ugomvi baina yao, makomando wakaona busara wageuze na kuwaachia wababe.

Sasa baada ya hilo tukio, mikakati imebuniwa ya kuwawezesha kufanya kazi pamoja, kifupi ni kwamba wakati inatokea ngoma kama hii, makomando wanapewa kipao mbele. Kama jinsi ilitendeka pale Garissa, makomando walifika na kuzima ngoma ndani ya dakika 12. Tazama hii video


acha uongo wewe hao makomandoo walishindwa kufanya chochote alshabaab waliwazidi maarifa....badala ya kuingia front wenyewe walikuwa nje wamejificha kwenye mitaro...makomandoo feki wale hakuna kitu
 
Huyo bodyguard anaitwa nani? Halafu kwani bodyguard wa rais ni mmoja?
Huyu jamaaa anachanganya madesa, rais halindwi na mtu mmoja bali yule anaekaa nyuma yake ni mpambe wa kumhudumia kwa ukaribu zaidi rais, lakini pia na yeye ni mlinzi wake, walinzi wa rais hukaa pembeni kidogo, na wanavaa kawaida tu, na huwa wako makini sana.
 
umw
Huyu jamaaa anachanganya madesa, rais halindwi na mtu mmoja bali yule anaekaa nyuma yake ni mpambe wa kumhudumia kwa ukaribu zaidi rais, lakini pia na yeye ni mlinzi wake, walinzi wa rais hukaa pembeni kidogo, na wanavaa kawaida tu, na huwa wako makini sana.

umeweka sawa
 
Sema polisi ni waoga tu, hawawezi kudiriki kusimamisha gari la jeshi hata kama kuna makosa masikini, wanaogopa kichapo


swala la kupigwa na mtu hasa kupigwa na JWTZ ni uoga tu na ni kuwa affected saikolojia, watu wamejingea kuwa jwtz wana nguvu na wana weza kupiga..kupigana ni ujuzi na uwezo wa mtu..
 
dah mnanikumbusha siku nliorudi nyumban kifua wazi baada ya mjeda kuchukua tshirt yangu ya mabaka mabaka, lol, wale sio watu ni mijitu.
 
Mkuu nazan majenerali wote wapo hai sasa sjui ni jenero gani huyo? Alafu kama ni meja jenero au brigedia jenerali zitalia risasi idadi kulingana na cheo chake.iyo mizinga ni ipi mku?
mejenerali wote wapo hai!!!!???
 
Wanajeshi wengi bangi na shule yao ndogo.afu pia wanajesh huwa wanawaonea wivu police kimaslahi,maana ingawa police wanalipwa kidogo kuliko wanajesh lakin police wengi wengi wamejijenga kiuchumi kuliko wajeshi.
Not kweli hii
 
Wanajeshi wengi bangi na shule yao ndogo.afu pia wanajesh huwa wanawaonea wivu police kimaslahi,maana ingawa police wanalipwa kidogo kuliko wanajesh lakin police wengi wengi wamejijenga kiuchumi kuliko wajeshi.
Hahahaaaaaaaa
 
Majeshi yote ni muhimu ....JWTZ fahari yetu ....wanaopigana ni utovu wa nidhamu
 
Jeshi muda wote lipo kazini huwezi jua unavyo mzuia mjeda katika foleni unamchelewesha katika kazi muhim kiasi gani,kwanza hata heshima ya mjeda na hawa mwera ni tofauti hadhi ya mjeda ipo juu sana kuliko polisi.
 
Back
Top Bottom