JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC


JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limevitaka vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), badala yake taarifa rasmi zitakuwa zikitolewa na jeshi hilo kila baada ya wiki mbili.
.

Safi sana maana kuna makajanja walikuwa wanatupeleka kuzimu kwa kutuletea taarifa za umbeya. Natamani sana watakotuletea tena vitaarifa vyao vile wapelekwe kambini wa................!
 
Huwa nashangaa sana hii trend ya CCM kuwa press conference ,halafu wanasema kirahisi tuu kuwa vyombo vya habari ndivyo vinachochea, vyombo vya habari ndio sababu....Hembu tuambieni ni vipi JK anaongeozwa namagazeti?

Kidogo sielewi hapa, kwani sasa kila gamba likipanda kelele kibao za mipasho kuwa sijui wachochezi, sijui nani....wachochezi hapa wanaweza kuwa marais ya nchi jirani na si waandishi makanjanja wanaoshiba kwa kumpamba JK.

Hembu kidogo CCM muwe na akili kidogo.
 
Huyu Mwanajeshi atakuwa Mjinga sana Jeshi kubwa kama la USA linaandikwa sembuse hawa mgambo wa TZ

Haya kakojoe ukalale tumeshakusikia, kwa kauli yako hii hata kuwa mama wa familia bado haujafikia, hauna tofauti na Ndugu ai.
 
.....Nadhani itakuwa vigumu sana kudhibiti hili.........hasa kwa teknologia ya sasa......kuna njia nyingi sana za kupata habari ......tena kwa kasi ya ajabu........hasa ukuchukulia kuwa hawajaweka bayana ni njia ipi wanayoisemea.........labda wawe na namna ya kutupasha habari kila baada ya saa moja hivi.....tena kutoka pande zote mbili..........kusubiri wiki 2 nadhani hata wao watakuwa nyuma kihabari...........ni mawazo yangu tu.......
 
Wanajeshi wetu nao wakifa tutangojea taarifa kila baada ya wiki 2 ? Je ikitokea kikosi kimepigwa hadi mpakani nako taarifa ni kila baada ya wiki 2 ?
 
Hilo katazo ni kwa vyombo vya habari Tanzania tu? JWTZ iko chini ya majeshi ya UN, je na UN imetoa katazo kama hilo?

hata mimi natafakari.itakuweje vya rwanda?itakuweje vya magharibi, magazeti na mitandao.
 
Kwa zama tulizonazo sasa huyu bwana kapima maji mguu...Muhimu hapa ni kushauri kutokuwepo kwa hapari zenye mrengo wa upotoshaji ambazo mwisho ndiyo huweza kuzaa uchochezi,uhasama na mambo mengine yanayofanana na hayo!
 
Ni kweli mkuu. Hao m23 wanarusha habari kila baada ya DAKIKA MBILI AU TATU kwenye twitter acount yao. Nyingi ya habari ni za propaganda za uongo. Je watanzania wawe wanangoja wiki mbili kuja kukanushwa habari hizi za uongo! Kumbuka information is power!

.....Nadhani itakuwa vigumu sana kudhibiti hili.........hasa kwa teknologia ya sasa......kuna njia nyingi sana za kupata habari ......tena kwa kasi ya ajabu........hasa ukuchukulia kuwa hawajaweka bayana ni njia ipi wanayoisemea.........labda wawe na namna ya kutupasha habari kila baada ya saa moja hivi.....tena kutoka pande zote mbili..........kusubiri wiki 2 nadhani hata wao watakuwa nyuma kihabari...........ni mawazo yangu tu.......
 
Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.

NI ngumu kupata briefing ya kila siku labda useme wiki moja hivi ....kumbuka battlefield siyo kwenye kiyoyozi hapo ulipo...
 
Hainingii akilini katka katazo hili..sidhani kama mpaka wanafikia maamuzi ya kutoa katazo hili hwakufikiria enzi zile zimepita...watu wanapata habari tena za uhakika hata bila kupitia vyombo vya habari vya nyumbani....

najiuliza:

Haki ya wananchi kupata habari kwa wakati iko wapi?
Jukwaa la wanahabari wamesemaje kutokana na katazo hili?
Kwani taarifa za congo tulikuwa tunazipata za kuhusu JWTZ peke yake? au juu ya mgogoro wa congo?

Nielewavyo mimi habari inatakiwa itolewe na mtu neutral mwenye kutoa hali halisi ya kitu bila kupendelea upande wowote ndio habari na ethics ya taaluma hiyo...hivi JWTZ ni neutral katika kutoa habari zitakazo wahusu??

:tape: Hii si Haki......kufunga midomo na kuzuia kalam za waandishi.....!!

“Digest-digests, digest-digest-digests. Politics? One column, two sentences, a headline!”
 
Huyu mwanajesh wa enzi za Musuguri. Siku hz unaweza kupata habari za tanza nia kupitia mitandao. Jwtz hawana twezo kutoa habari isiyochakachuliwa. Hzo habari baada ya wk2 wawapatie wanjesh wenzao sisi tutatumia independent sources kwa habari za ukweli.
 
Serikali ya tz, jeshi la tz, police tz bado wanaishi miaka 500 ilopita, na sasa wanawalizimisha watz wawaishie maisha yao.
Watu mnalipwa kodi zetu halafu tusijue manafanya nn?
 
wasomi bado wanahitajika jeshini..natamani na jeshi la marekani wakataze vyombo vyao kuandiaka kuhusu vita yao syria because itawagombanisha na russia..
KWA UJUMLA WAKE JWTZ WAMETOA AGIZO LA KIPUUZI NA HALINA MASHIKO YA KISHERIA..DUNIA IMEBADILIKA..NYIE TOENI TAARIFA ZETU MNAZOONA KUWA NDIO SAHIHI..WANAHABARI WATOE ZAO..WANANCHI WATACHAMBUA PUMBA NA MCHELE...
 
batllefield in drc goma iz something that TaNZANIANS feel pretty 2 mak folloup 2 know wat iz going on especially for those who like changes with peace stabilization in great lakes territoriees. Imformation is power, and we have a right 2 get them.
 
Hawa jamaa inaelekea wako kisiasa na wanafuata upepo wa siasa kama walivyo, inaelekea baada ya kuiona ile picha ya jk na pk wakipeana mikono Kampala wakajua mgogolo umeisha na sasa wanakuja na hii slogan ya vyombo vya habari kuchochea.
 
Jeshi halina mamlaka kuzuia magazeti kuandika habari za JWTZ, wanachoweza ni kuyashitaki magazeti yanayopotosha au kuzusha habari za uongo. Kuna mihimili mitatu ndio yenye kuweka maamuzi nayo ni Bunge, Mahakama na Watawala. Meja wa JWTZ sio mtawala na kama ni mtawala basi ni huko huko kambini kwao au Mtwara. CCM imefanya nchi hii kuwa kama chaka la wajing a, kila mtu anadhani anaweza kutoa onyo.
 
Back
Top Bottom