JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

Huwa najiuliza sana juu ya busara na hekima ya wengi wa viongozi wetu, na sasa suala hili limeangukia kwa uongozi wa JWTZ. Hivi kweli JWTZ walijiuliza kwa makini kabla ya kutoa katazo hadharanai kwamba ni marufuku kuandika habari za mgogoro wa DRC?

Katika karne hii unatoa katazo hama hilo - labda uwe mtu wa aina aliyepanda cheo kutoka private miaka ya 70 na sasa umekuwa na cheo kikubwa cha kukuwezesha kutoa amri za ujumla kama hii. Labda huko jeshini inawezekana, lakini uraiani utapata shida sana ukianza amri kama hizi. Uraiani hatuna watu waliomaliza darasa la pili wakapanda cheo kuwa ma judge katika mahakama zetu.

Kwanza, nikiandika habari za kweli na zenye kuthibitika juu ya mgogoro wa Rwanda, utanifanya nini, au utanishitaki kwa sheria gani?

Kwa maneno mengine - tatizo ni kuandika habari au kuandika habari za uzushi?

Kama ni suala la kuandika habari za uzushi - basi hilo ndilo lapaswa kushughulikiwa, sio kutoa amri ya ujumla kwamba hakuna kuandika kuhusu mgogoro wa DRC.

Nitawashangaa sana taasisi za habari kama watakaa kimya juu ya hili.

Amri ya JWTZ kupiga marufuku kuandika juu ya mgogoro wa DRC naifananisha na mambo yafuatayo;

  • Baadhi ya madereva wanaendesha magari vibaya Dar - Moro na kusababisha ajali - Waziri anapiga marufuku kuendesha magari barabara ya Dar - Moro kwa madereva wote
  • Baadhi ya wanaume wanapata mfadhaiko kwenye daladala na kuwafanyia vitendo vibaya wanawake - Waziri anapiga marufuku wanaume kupanda daladala
  • My wife nyumbani anaunguza mboga - nampiga marufuku kunipikia!

Nchi hii bwana, kila mtu anakuja kivyake vyake tu!
 
kwa hiyo na vyombo vya nje ya nchi nani atavizua wasiandike........halafu watu kama ITV wanamwakilishi wao kule drc Bw. Malimbika kila siku anaripoti kinachoendelea huyu nnaye wanamdhibiti vipi......na kwa nini magazeti yaandike kutokana na ripoti ya jeshi je, kama gazeti lina mwandishi wake kule vip......wao walitakiwa kukanusha au kueleza ukweli kwa habari zote zitakazoripotiwa kwenye magazeti ambazo ni za uongo....hii si ndiyo kazi ya afisa habari wao au.....shida hapo uvivu tu idara ya habari......hiyo kazi apewe mtu serious afanye kazi tofauti na sasa
 
"Alisema kuwa viongozi hao walilaani mashambulizi ya M23 yaliyojeruhi na kumuua Meja Mshindo wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa askari walioko nchini Congo katika kusimamia amani chini ya Umoja wa Mataifa". HIVI kagame na museveni NAO WALILAANI KWELI? WAKATI WAO NDIO "wauaji" kwa maana ya kuwasapoti watutsi wenzao m23? Nitandelea kusisitiza kuwa, waTanzania tuwe makini sana na watutsi! Hawaaminiki hata kidogo...
 
Jeshi halina mamlaka kuzuia magazeti kuandika habari za JWTZ, wanachoweza ni kuyashitaki magazeti yanayopotosha au kuzusha habari za uongo. Kuna mihimili mitatu ndio yenye kuweka maamuzi nayo ni Bunge, Mahakama na Watawala. Meja wa JWTZ sio mtawala na kama ni mtawala basi ni huko huko kambini kwao au Mtwara. CCM imefanya nchi hii kuwa kama chaka la wajing a, kila mtu anadhani anaweza kutoa onyo.

Hapa katika blue....tuko pamoja na sahihi kabisa....umesema bila fitina....but kwenye red ni siamini kama mtu yeyote mwenye mamlaka akisema anawakilisha CCM.... ila ukweli ukileta politics katka sehem ambazo ni non politics ni tatizo...hapa jeshi limeleta siasa katika hili...limesemea kiushabiki..sijajua Polisi wana nafasi gani kusimamia katazo hili...!!
 
Dunia ya utandawazi huwezi zuia mvua....... We have right to be informed and to inform bila kuvunja Sheria.

Jeshi halitungi Sheria kwa hiyo hawawezi kutoa amri isiyofuata Sheria...Simpo as that,kama kuna mtu atakiuka Sheria afunguliwe mashtaka na si Jeshi kuingilia uhuru wa kuhabarishana.....
 
Mimi nataka kipata updates kila saa kuhusu Jeshi letu linavyoendesha hiii operation huko Congo dhidi ya m23, kama hawataki basi nitahitaji updates kuhusu MONUSCO, kama vipi nitapata updates kupitia vyombo vya habari vya nchi jirani hata Rwanda watatuhabarisha tu
 
Ni tamko la kijinga kabisa.
JWTZ kwa sasa kumejaa wajinga watupu?

Eti vyombo vya habari visiandike na taarifa itatolewa kila baada ya wiki 2, kwanini?

Watanzania kwa sasa tunataka habari moto moto, breaking news, Live coverage, Balanced information nk. Sasa JWTZ wako karne gani?
 
dunia ya utandawazi huwezi zuia mvua....... We have right to be informed and to inform bila kuvunja sheria.

Jeshi halitungi sheria kwa hiyo hawawezi kutoa amri isiyofuata sheria...simpo as that,kama kuna mtu atakiuka sheria afunguliwe mashtaka na si jeshi kuingilia uhuru wa kuhabarishana.....



hawa wanajeshi wa tanzania hawajui kuwa utandawazi una ngguvu kuliko jeshi lenyewe
 
Nilimsikiliza yule major kwa kweli nilifadhaika sana sana... Hiv kweli kwan nchi haina uongozi au utaratibu maalum???! Vyombo vya habari vinaweza vikapeleka nchi kwenye vita na nchi nyingine??! Haiwezekan.. Yan JK au Mwamunyange atoa amri yakuingia vitan kisa eti Mtanzania, Nipashe ama JF. Naamini maneno yamwanzo hajaagizwa aseme vile ama alikosea.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Nilimsikiliza yule major kwa kweli nilifadhaika sana sana... Hiv kweli kwan nchi haina uongozi au utaratibu maalum???! Vyombo vya habari vinaweza vikapeleka nchi kwenye vita na nchi nyingine??! Haiwezekan.. Yan JK au Mwamunyange atoa amri yakuingia vitan kisa eti Mtanzania, Nipashe ama JF. Naamini maneno yamwanzo hajaagizwa aseme vile ama alikosea.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Tanzania yenyewe ni ajabu la nane la dunia.
 
Nafikiri jeshi liko sahihi! Hata hivyo lilichelewa kutoa tamko hilo maana wengine hapa kama Mr. P...walijifanya wasemaji wa jeshi hilo, bila hata busara kidogo wakiongozwa na mihemuko binafsi na uzalendo bandia.
 
Naunga mkono hoja ya JWTZ kwani waandishi wetu wengi ni makanjanja na wepesi kutumiwa kwa rupia na ratiri moja.
 
Huku ni kuigwaya Rwanda na Kagame; inaonekana Kikwete alipigwa mkwara na Kagame au yule madam walipokuwa chobingo. Duh!! Washikaji wamegwaya kabisa!! Watz wanachekesha sana!
 
Mie nilivyoina hii article nikabaki kushangaa tu, kwamba kule jeshini bado kuna maofisa ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri hasa katika dunia hii ya leo ya mtandao. Vyombo vha habari mbali mbali duniani vinafuatilia kinachoendelea kule DRC hivi kukitokea kitu ambacho vyombo hivyo vinaona kina umuhimu wa kutangazwa/kuandika anadhani wataacha kufanya hivyo!?

Hilo katazo ni kwa vyombo vya habari Tanzania tu? JWTZ iko chini ya majeshi ya UN, je na UN imetoa katazo kama hilo?
 
Sasa ndugu zetu walio vitani tutajuaje taarifa zao. Hili katazo ni kwa Tanzania tuu au na nchi zingine ni hivyo hivyo. Tupate taarifa baada ya wiki 2 mmmmh kuna kitu hapa si bure.
 
Mie nilivyoina hii article nikabaki kushangaa tu, kwamba kule jeshini bado kuna maofisa ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri hasa katika dunia hii ya leo ya mtandao. Vyombo vha habari mbali mbali duniani vinafuatilia kinachoendelea kule DRC hivi kukitokea kitu ambacho vyombo hivyo vinaona kina umuhimu wa kutangazwa/kuandika anadhani wataacha kufanya hivyo!?
Tz bado sana rafiki, nami nimeduwaa sitaki kuamini kama patakua na utekelezaji ktk hili.
 
Back
Top Bottom