JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

Watu wanawaza miaka 50 nyuma uko ni kuingilia uhuru wa habari kama majeshi yapo chini ya UN kwa nini yeye akataze labda magazeti yao ila sio vyombo vingine
 
kusema tutegemee taarifa baada ya wiki mbili huo utakuwa ni ubabe tena taarifa zenyewe lazima wazitoe wao kwa nini wanatakaa tupate taarifa zilizochakachuliwa? hapo mimi siungi mkono ila ushauri kwa vyombo vyetu vya habari ni kutafuta habari za uhakika na sio kuandika habari za uchochezi na mihemko ya waandishi wao wa habari ili kusudi tu wao afanye biashara bila kuangalia athari zake baadae huu mgogoro wa Rwanda na Tanzania kwa kiasi kikubwa umekuzwa na vyombo vya habari mfano serikali ilipoamuru wahamiaji haramu waondoke vyombo vya habari badala ya kutangaza ukweli vyenyewe vikaegemea kutangaza waliofukuzwa ni wanyarwanda
 
Magazeti ya jamhuri na mtanzania
 
Halafu kule twitter kuna account ya JWTZ ila hatujui kama ni genuine. Je ku retweet news za kule inaweza kuwa issue pia?
 
Hapa katika blue....tuko pamoja na sahihi kabisa....umesema bila fitina....but kwenye red ni siamini kama mtu yeyote mwenye mamlaka akisema anawakilisha CCM.... ila ukweli ukileta politics katka sehem ambazo ni non politics ni tatizo...hapa jeshi limeleta siasa katika hili...limesemea kiushabiki..sijajua Polisi wana nafasi gani kusimamia katazo hili...!!
CCM inaharibu nchi kama sio kutupeleka katika civil war. Unakumbuka 2010 kabla ya uchaguzi, Shimbo alitumiwa kuwatisha wananchi. Hivi vyombo vinatakiwa visiingiliwe na vifanye kazi kwa mujibu wa sheria
 
Kama kuna vyombo vya habari vya nyumbani vitakubali agizo hili la kijinga basi utakuwa ndio mwisho wa uhuru wa habari nchini.
 
Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.

Unajua nimeshangaa sana,wakati M23 na wengineo wapo tweer muda wote unapata habari za frontline.sisi tusubiri Two weeks!
 
JF ipo watu watakutafuta updates na picha

JWTZ bado wako Kwenye 16th Century
 
We acha tu rafiki. Yaani kauli za asilimia kubwa ya watendaji wa juu katika taasisi mbali mbali nchini ni za kushangaza sana. Sijui wanaishi dunia ipi!!!! labda ya kusadikika hivyo kudhani kwamba wakisemacho wao basi kinakuwa ni sheria ambayo kila mtu ni lazima aifuate.

Sasa ndugu zetu walio vitani tutajuaje taarifa zao. Hili katazo ni kwa Tanzania tuu au na nchi zingine ni hivyo hivyo. Tupate taarifa baada ya wiki 2 mmmmh kuna kitu hapa si bure.
 
We acha tu rafiki. Yaani kauli za asilimia kubwa ya watendaji wa juu katika taasisi mbali mbali nchini ni za kushangaza sana. Sijui wanaishi dunia ipi!!!! labda ya kusadikika hivyo kudhani kwamba wakisemacho wao basi kinakuwa ni sheria ambayo kila mtu ni lazima aifuate.
Hawa ndio viongozi wetu bro wao hudhani wanaongoza watu wasioweza kufikiri wala kuhoji.
 
Kwa hiyo hata vyombo vya habari vya kimataifa vikieleza habari za vita hiyo haitakiwi ku quote habari hiyo? Tanzania ina vichekesho kweli. Jee ametaja sheria iliyotumika kutoa katazo hilo? Magazeti ya Kenya,Uganda na hata ya nchi mbali mbali za Duniani yanakuja kila siku,jee yakiwa na habari za vita ya Congo yatazuiwa kuuzwa? Mitandao na Radio za nje jee nazo zitasubiri taarifa ya msemaji wa TPDF baada ya wiki mbili?
Tamko hilo ni utata mwingine tena.
UKISEMA UKWELI JUU YA VITA IPIGANAYO NA jwtz UNACHUKIWA. mTANGAZAJI MAARUFU ENZI ZA SABINI, bEN kIKO ALIWAHI KUPATA MATATIZO NA SERIKALI KWA KUTANGAZA UKWELI JUU YA VITA VYA KAGERA. apparently, Tanzania , TWTZ wanataka kutoa habari zao za propaganda kila kukicha ili sisi tusielewe kitu. maana wataalamu wa propaganda jeshini hivi sasa hawana kazi, ila tukiacha kuandika kinachotokea Congo wao wataanza kazi zao za kupootosha umma. kusubiri wiki mbili, huo ni ukomunisti uliokubuhu!!!!
 
ni moja ya maajabu yanayopatikana nchini ila hayajapta fursa ya kitangaza nchi yetu

ila mimi sioni ajabu, elimu ya wanajeshi wetu tunaijua, Rais kilaza si ametokea hukohuko.
 
huyu Membe ni mbeya,amesema ni kikao cha faragha halafu yeye anakuja na kauli “Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali" halafu alikuwepo kwenye kikaoooooo......aache porojo zake hapa....
 
Wajinga wakubwa hawa Wanajeshi wana akili za sisiminzi, Hivi wanafikiri WaTanzania wa leo ni wa mwaka 47? au wa enzi cha Chama kimoja? Au wanafikiri bado WaTanzania wanendeshwa na mawazo ya Kimla (dictatorship)? Wajeshi hawa wamekuwa watu muflisi kabisa.

Na waviwache vyomba vya habari viendelee kupasha wanachi kupitia vyanzo vya habari na wao Wajeshi wamwage hizo propaganda zao kila baada wiki mbili sis Wananchi sio mazezeta kwani tuna akili ya kuchuja mbivu na mbichi ni zipi.

ABC News TV husema " WE Report, You Decide" Kwa hiyo na tuwache kila chombo cha habari kiripoti taarifa zake mwisho wa siku Wananchi tutaamua tushike lipi.
 
Watanzania tunamidomo sana wana JF tunaongea kuchochea ujinga alafu kunawatu wanajifanya wanauchungu na taarifa za kutoka Congo hamna lolote hauwezi kuwa na uchungu kuliko walioko ,front line wanapigana walitoaga picha za ku edit kwamba askari wetu eti wanabaka mabinti congo kumbe uongo, mm naona hii mijitu mingine sio mitanzania kabisa wewe ninani kila siku upewe taarifa za jwtz tumieni akili msilete masiasa kwenye wanaume wakazi walojitoleaga kufa sababu ya tz na Africa, tuwe na uelewa kufikiri
 
Kwenye article ya 'Human Rights" ambayo Tanzania imeridhia No. 19 na nukuu
"Everyone has the right to freedom of thought,expression;this right includes freedom to hold opinion without interference and to seek,receive and impart information and ideas through any media and regardless of frontiers".
Wanatafsiri vipi haki hii ya msingi ya kupata taarifa?

Labda chingereza chigumu
 
Back
Top Bottom