JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

Mimi siachi hata na nitakuwa na post humu na mods wakiwa wanafuta nitakuwa na wapm tu.huwezi kumpangia mtu jinsi ya kupata habari anayoitaka kwann iwe kwa tz wakati bbc aljazeera VOA n.k wanaendelea kuto taarifa jamani wana jf huu si u k.sasa huyu kaja na amri za kijeshi ambazo hazitekelezeki uraiani
 
Itakua dunia nzima au tanzania tu? Mimi nikizicopy kutoka bbc au telegraph itakuwaje?. wanatuonea. Tanzania tuna haki ya kupata habari. Mia
 
labda kikwete na kagame wameambiana kuwa tunachonganishwa . lakini wao wana wajibu wa kupima taarifa mimi naona bado hawajapatana kidhati na ndiyo maana wamekurupuka , itakuwa kila mmoja anasema mimi nimesikia toka TZ/RW unanilaumu kulikoni mzee mwenzangu, sasa hapo soon utasikia na rwanda wanakataza taarifa za jeshi kuripotiwa wakihisi eti ni kahatua kamaridhiano. kumbe mtusi ansubiria kumi na nane zake zitimie
 
Mimi binafsi toka awali nilikuwa napinga sana watu kushabikia VITA na Rwanda wengine hata walikuwa hawaitambui MONUSCO Badala yake kila M23 wanapopigwa na Majeshi ya Monusco vyombo vyetu vya habari Vilitoa HONGERA kwa JWTZ ni sawa maana nao ni sehemu ya Monusco.Lakini kitendo cha kusema askari wetu wa JWTZ waende mpaka KIGALI hii haikubaliki kabisa.Na kuhusu hili katazo JWTZ wamechelewa sana kulitoa hasa ukichukulia na Teckinologia ya leo hili katazo halina maana kabisa.
 
Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.

Duh JF sijui nacho ni chombo cha habari! Kama ndivyo ina maana nayo imepigwa marufuku?
 
nikisema jwtz limejaa wabalaji akina R.B na wapuuzi wenzako mnanishambulia kwa matusi haya sasa andika tena habari za wabakaji kwenye kigazeti uone watakavyo kubaka kama walivyo wafanyia wana mtwara..
 
Last edited by a moderator:
Amri za Geshi bana au nao siasa ndiyo zimeshaingia geshini?? Wasije wakatofautiana kesho ukamsikia Membe anatoa taarifa ya Geshi.
Haya geshi tumemisikieni vizuri, vp kuhusu CNN,BBC,DW,UBC,CITIZEN etc nao mmeahawaambia wasitoe habari yoyote au tukiona hizo habari kwenye TV tufunge macho na kwenye radio tuzibe masikio tukisikia hizo habari???
Geshi hizi zama nyingine ktk khabari.
 
Mimi binafsi toka awali nilikuwa napinga sana watu kushabikia VITA na Rwanda wengine hata walikuwa hawaitambui MONUSCO Badala yake kila M23 wanapopigwa na Majeshi ya Monusco vyombo vyetu vya habari Vilitoa HONGERA kwa JWTZ ni sawa maana nao ni sehemu ya Monusco.Lakini kitendo cha kusema askari wetu wa JWTZ waende mpaka KIGALI hii haikubaliki kabisa.Na kuhusu hili katazo JWTZ wamechelewa sana kulitoa hasa ukichukulia na Teckinologia ya leo hili katazo halina maana kabisa.

sasa umeandika nini maana naona umejikanyaga tu..
 
nikisema jwtz limejaa wabalaji akina R.B na wapuuzi wenzako mnanishambulia kwa matusi haya sasa andika tena habari za wabakaji kwenye kigazeti uone watakavyo kubaka kama walivyo wafanyia wana mtwara..
Mkuu Crashwise hawa akina R.B ndio wabakaji wakubwa huko Mtwara
 
Last edited by a moderator:
Nadhani heading imekosewa kwakuwa jeshi halina mamlaka hayo.

Itakuwa jeshi limevitaka/kuviomba vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za kichochezi.
 
hivi hili ndilo suluhisho kweli?? Ama kweli tz bado sana


nina support sana ila daa kwa hili sidhani inaweza ikawa ni suluhisho kwa karne hii maana kwa uzoefu wangu kukaa na jamii siku hizi taarifa wanachi wengi kupitia hivi wanachi lazima watapeana taarifa tuu kwa njia hizi hata kama mtu hana t.v
1.facebook
2.yotube
3.blogs tofauti
4.aljazeera/sky news/bbc
5.twitter
6.whats up
7.redio mbaoo
8.vijiwe vya wazee kahawa
9.vijiwe vya bangi na sigara
10.vilabu vya pombe haramu
11.kwenye madaladala
12.vijiwe vya wazee wacheza bao na karata
13.vijiwe vya pool table

ushauli wangu....ni kutoa elimu wa wananchi ..ya kujielewa....ni vigumu sana kuzuia watu kupeana taarifa japo zipo za ukweli na nyingine si za kweli na zingine uchochezi
 
Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.
  • Yap ni kweli hiki ndicho alipaswa kusisitiza, na si vinginevyo.
 
Katiaka zama hizi za uwazi unaotokana na maendeleo ya teknolojia,bado kuna watu wanaamini kuzuia habari kutasaidia.Ni kosa kubwa kwa kitengo cha PR na maboss wa JWTZ kwa ujumla kuzuia taarifa, wanapaswa kuhamasisha mawasiliano ili kuondoa mikanganyiko isiyokuwa ya ulazima.
 
Kwa dunia ya sasa yenye teknologia kubwa ni ngumu kuzuia watu wasipeane taarifa. Kinachotakiwa,chanzo chochote cha taarifa kihakikishe kinatoa au kinasambaza taarifa reliable na credible. Si kuzuia. Hivi JW itawezaje kuzuia taarifa zinazosomwa na kuonwa kila siku na watanzania toka DW,ALJAZEERA,CNN,BBC,ABC NEWS,CCTV,CBN,FOX NEWS,REUTERS,VOA,RFI,NYASATIMES,CITIZEN,UBC nk. Wote hawa na wengineo wameshakatazwa wasionyeshe au kuandika lolote?. Nadhani uwezo huo hawana. Magazeti TV na radio za Tanzania yasipoonyesha au kuandika habari zinazohusu Tanzania au maendeleo huko DRC watanzania watapata habari toka nje ambazo nyingine zinaweza kuwa ni za uongo. Nadhani watu wa information wa Jw wafanye kazi kisasa zaidi.
 
Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.

Uko sahihi mkuu, kama sasa tunaambiwa M23 wanajikusanya upya kujibu mapigo na jeshi litasubiri wiki mbili zijazp ndio watuambie, je, waandishi waliopo Goma nao wameambiwa?
 
ah basi mi na-follow @fardc13, Monusco, M23 drc napata news kila sekunde through twitter..
 
Last edited by a moderator:
Ulinzi wa taifa ni jukumu la kila raia mwema
 
Nadhani hili tangazo mimi halinihusu kwahiyo sina la kuchangia, nina information nyingi zaidi ya rais na siku hizi hata ninaposafiri kwa barabara sihitaji tena kusoma vibao vya kilometers maana Galaxy yangu inatosha kuiuliza kwenye Google map.

Hili ni tangazo kutoka kwa mtu mjinga ambaye hana tofauti na maafisa vilaza wa uhamiaji ambao ukipeleka maombi ya passport wanataka upeleke barua ya mwaliko wakati hawajui unaweza ukafunguwa email account kwa jina la kizungu halafu ukajitumia mwenyewe kwenye account nyingine.
 
Back
Top Bottom