JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

Mnaongelea habari ya vita, leo iko mbali ingekua karibu je?, alafu watu tukumbuke swala la vita sio siasa za ccm.
 
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limevitaka vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), badala yake taarifa rasmi zitakuwa zikitolewa na jeshi hilo kila baada ya wiki mbili.

Katazo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meja Erick Komba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo.

Alisema hali hiyo inatokana na jeshi hilo kubaini kuwa baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaandika habari za uchochezi zinazotaka kuziingiza vitani nchi ya Tanzania na Rwanda.
Meja Komba alisema hategemei kama kutakuwa na chombo chochote cha habari kitakachotoa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo bila kupata taarifa rasmi kutoka jeshi hilo.

Alionya kuwa chombo chochote kitakachokwenda kinyume kitakuwa kina tatizo.
Meja Komba alisema wananchi wanapaswa kuelezwa kuwa kikosi cha Tanzania kilichoko DRC ni sehemu ya Brigedia ya SADC, iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (Monusco).

Alitaja majukumu ya kikosi hicho kuwa ni kuzuia waasi wa M23 na wengine kujitanua, kuvunja nguvu zao na kuyapokonya silaha makundi yote ya waasi.
“Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Monusco, inamaanisha kuwa operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa,” alisema.

Aliongeza kuwa Tanzania haikupeleka kikosi chake DRC kwa ajili ya kupigana na M23, pia ieleweke kuwa haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo ambapo Rwanda ilitoa ridhaa kikosi cha Tanzania kwenda DRC.

Meja Komba alisema Rwanda ni miongoni mwa wanachama wa nchi za Maziwa Makuu, ambayo imesaidia kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

“Tanzania inashiriki katika operesheni hiyo ya ulinzi wa amani nchini DRC kutokana na mgogoro kati ya serikali na waasi hususan kikundi cha M23,” alisema.
Mgogoro huo ulianza Aprili mwaka jana, ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika jeshi la serikali na kuanzisha mapigano yaliyosababisha hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Benard, amesema kuwa marais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda wamemaliza tofauti zilizokuwa zimejitokeza kati yao hivi karibuni.
Marais hao walikutana na kufanya kikao cha faragha jijini Kampala nchini Uganda juzi baada ya mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na baadaye kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.

Kuzorota kwa mahusiano kati ya viongozi hao kulikuja kufuatia kauli ya Rais Kikwete ya kumtaka Rais Kagame kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake vilivyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ushauri ulioonekana kumkera Rais Kagame.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Membe alisema marais hao walitumia mazungumzo yao yaliyochukua muda wa saa moja kujadiliana na kueleweshana mambo mbalimbali yaliyosababisha kutoelewana.
“Baada ya mkutano huo ambao uliwapa fursa za kuchambua, kujadili na kurejesha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili, marais wetu walitoka na nyuso za furaha,” alisema.

Moja ya maazimio ya kikao chao ni kuwa na vikao vingine kati ya Rwanda na Tanzania katika siku zijazo.

“Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali,” alisema.

Mbali ya kikao hicho pia Rais Kikwete alifanya kikao kingine cha faragha na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambapo walipata muda wa kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali kuhusu nchi zao na mambo ya migogoro katika nchi za Maziwa Makuu.

Akizungumzia yale yaliyokubaliwa katika mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu, Membe alisema kuwa mkutano huo kwanza ulimruhusu Rais Museveni aendelee kusuluhisha vita ya serikali ya DRC na waasi.

Alisema kuwa viongozi hao walilaani mashambulizi ya M23 yaliyojeruhi na kumuua Meja Mshindo wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa askari walioko nchini Congo katika kusimamia amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Wanataka kuturejesha Enzi zile za mwaklimu, Television alikuwa nayo yeye tu harafu anatujuza kupitia radio RTD aliyoyaona kwenye vyombo vya nje kupitia Luninga,ninachojua,tusipoandika sisi watanzania tunaoongopa amri halali ya viongozi wetu, vyombo vya nje vitaendelea kutujuza,wafunge na satlite zote zinazorusha taarifa ili zisitufikie ziwe zinaachiliwa baada ya wiki mbili.......Sina uhakika kama wamechanganua vizuri kabla ya kutoa taarifa hii. Zamani kwenye viwanda vya wahindi ilikuwa marufuku kupiga picha,siku hizi tunatembelea google earth nakuona kila kitu...haya bwana ,tekelezeni amri halali.
 
Wanataka kuturejesha Enzi zile za mwaklimu, Television alikuwa nayo yeye tu harafu anatujuza kupitia radio RTD aliyoyaona kwenye vyombo vya nje kupitia Luninga,ninachojua,tusipoandika sisi watanzania tunaoongopa amri halali ya viongozi wetu, vyombo vya nje vitaendelea kutujuza,wafunge na satlite zote zinazorusha taarifa ili zisitufikie ziwe zinaachiliwa baada ya wiki mbili.......Sina uhakika kama wamechanganua vizuri kabla ya kutoa taarifa hii. Zamani kwenye viwanda vya wahindi ilikuwa marufuku kupiga picha,siku hizi tunatembelea google earth nakuona kila kitu...haya bwana ,tekelezeni amri halali.
 
Safi sana,ilikua inanikela sana Ushabiki ulikuwepo ile sio JWTZ ile ni Munosco-UN,
 
Naunga Mkono Hoja.Kuna watu walikuwa wanashinikiza JWTZ ipige hadi Kigali bila kuainisha sababu za kufanya hivyo.Nashukuru JWTZ wameshtukia Janja ya hawa Wachumia Tumbo na Wauza Unga.
Hawajazuia maoni wamezuia ripoti zisizo rasmi kutoka front-line kama vile wangapi wamekufa n.k. Watazuiaje maoni kuwa wapige hadi Kigali ikiwa mzee wa Kigali anataka kutu-"hit"?
 
Watanzania tunamidomo sana wana JF tunaongea kuchochea ujinga alafu kunawatu wanajifanya wanauchungu na taarifa za kutoka Congo hamna lolote hauwezi kuwa na uchungu kuliko walioko ,front line wanapigana walitoaga picha za ku edit kwamba askari wetu eti wanabaka mabinti congo kumbe uongo, mm naona hii mijitu mingine sio mitanzania kabisa wewe ninani kila siku upewe taarifa za jwtz tumieni akili msilete masiasa kwenye wanaume wakazi walojitoleaga kufa sababu ya tz na Africa, tuwe na uelewa kufikiri

Kama wanabaka wanawake Mtwara watashindwa kubaka Huko Congo? Hivi we hujui akili za baadhi ya wanajeshi? Km makao makuu ya jeshi inaweza kukataza vyombo vya habari kuripoti habari za DRC je askari kuruta huko vitani atashindwa kufanya vitendo vya ajabu.
Waziri ametumbia mgogoro wa Jk na Kagame umemalizwa juzi kwenye mkutano wa Uganda, sasa hayo magazeti yatakayochochea vita kati ta Tz na Rwanda kwa kuandika habari ya DRC za uchochezi nani atazifanyia kazi hizo habari ? Maana majeshi ya tz wala Rwanda hayawezi kwenda vitani bila amri ya amiri jeshi mkuu, sasa km hawa maamiri jeshi wamemaliza tofauti zao، katazo la kuandika hizi habari imetokana na nn? Vinginevyo tuambiwe km kwenye ule mkutano hawa jamaa hawakuelewana,
maana picha tu za watu kupeana mkono haimaanishi kuwa walielewana, huenda walikua wanasalimiana au kuagana maana kikao chenyewe kilikua cha faragha.
 
huyu Membe ni mbeya,amesema ni kikao cha faragha halafu yeye anakuja na kauli “Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali" halafu alikuwepo kwenye kikaoooooo......aache porojo zake hapa....

Hii kauli ya Membe....kwangu nimemtoa credit.....waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje hapaswi kuzungumza kimapasho namna hii....unafikir wananchi wa Kigali na Tz wanaweza kuwachonganisha JK na PK? KAULI za viongozi hao ndio zimewaletea tofauti...hayo majungu yametoka wapi wakat kila PK alikuwa anaongea hadharan na JK alisema hadharani.....sipend kuona kiongozi kama Membe anatoa tamko kama vikund vya udaku vinapigana vijembe...sasa nimeamini kuwa taarifa zile za hotuba za kikwete na PK ndio wameshinikizwa kupiga marufuku news za kule.....sio sasa///
 
hili katazo ni kwa vyombo vya habari vya tanzainia tu,kwa sheria ipi?ikitokea chombo chochote cha habari kikaandika kuhusu brigedia ya SADC itakuaje?je vipi kwa BBC,CNN.AL
JAZEERA n.k?Jeshi letu linafikiri katika enzi za chama kushika hatamu(1978-1979 vita vya kagera)magazeti uhuru,mzalendo,mfanyakazi dailynews na sunday news.Walioko kongo ni kaka na dada zetu katika wa umoja wa mataifa wanajitolea kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu kwa kuhatarisha maisha yao ili wenzetu wawe na amani nasi tunaitaji kupata ukweli kwa kile kinachojiri na wala sio propaganda
 
Mimi nilidhani tuna jeshi la kisasa kumbe bado ni la kizamani lililo kwenye zile enzi za kuambiana kama huna "appetite" uazime ya mwenzako. Wameshasema JWTZ iko Congo kama sehemu ya kikosi cha UN chini ya mwavuli wa SADC. Sasa hili katazo lao kwa vyombo vya habari linatolewa katika muktadha upi? Inawezekana kweli ukazuia habari za UN zisitolewe kwa wananchi? Hii timeframe ya kutoa taarifa kila baada ya wiki mbili mbona haina mantiki kabisa? Habari za wiki mbili ni habari kweli wakati vyombo mbalimbali vya kimataifa vinaripoti karibu kila siku? Kuna haja kubwa ya jeshi letu kubadilika kifikra.
 
Hapa kuna jambo limejficha..
Wenyewe ndio wanasema JWTZ wataisambaratisha M23
Wamevamia Commoro ,hawajatoa katazo kwa vyombo vya habari,iweje sasa watoe katazo?
Wameshaona maji janazidi unga?
Watazuia na BBC,Al-Jaazera,CNN na DW!?
Jinga sana!
 
"Alisema kuwa viongozi hao walilaani mashambulizi ya M23 yaliyojeruhi na kumuua Meja Mshindo wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa askari walioko nchini Congo katika kusimamia amani chini ya Umoja wa Mataifa". HIVI kagame na museveni NAO WALILAANI KWELI? WAKATI WAO NDIO "wauaji" kwa maana ya kuwasapoti watutsi wenzao m23? Nitandelea kusisitiza kuwa, waTanzania tuwe makini sana na watutsi! Hawaaminiki hata kidogo...
Mkuu Rushasha nimeamini kwamba siasa ni michezo ya kuigiza, yaani inaonekana Tanzania, Rwanda na Uganda wote hatujui M23 wanakuwa funded na akina nani!! Alafu kilicho nishtua zaidi ni kule kusema wataruhusu tena wahamiaji haramu warudi mkoani Kagera ili waombe sijui urai nk - hii itatutengenezea a time bomb baada ya miaka kumi na tano/ishirini mkoa wa Kagera utakuwa kama KIVU, mambo ya Wanyamulenge yatahibuka kwa kasi ya ajabu - tumejaribu kutoa tahadhali mara nyingi tu, kwa bahati mbaya hakuna anaye tusikiliza, tunaendelea kuamini watu tu bila ya kufanya ka utafiti kuhusu hulka zao!!!
 
Kweli Tanzania ni zaidi ya unavyo ijua.....kila mtu anavunja katiba kwenye ofisi yakekama kamanda apo umewanyima watz haki yao kikatiba ya kupata habari na mleta uzi Mbona umeshatoa habari au hii haiusiani na habari za DRC?
 
MKUU APO KWENYE RED NASIKIA KAMA HARUFU YA UKWELI VILE 😛ray:😛ray:😛ray:


Hapa kuna jambo limejficha..
Wenyewe ndio wanasema JWTZ wataisambaratisha M23
Wamevamia Commoro ,hawajatoa katazo kwa vyombo vya habari,iweje sasa watoe katazo?
Wameshaona maji janazidi unga?
Watazuia na BBC,Al-Jaazera,CNN na DW!?
Jinga sana!
 
MKUU APO KWENYE RED NASIKIA KAMA HARUFU YA UKWELI VILE 😛ray:😛ray:😛ray:

Umeona eeh!! Jamaa wanapenda micfa sana, sasa M23 yaelekea wamejipanga na mambo yanakwenda ndivyocvyo,ili kujihami wanaanza kuvpga Ban vyombi vya habari...
Shame in U JWTZ
 
Mhh hebu nione itakavyokuwa! "sasa tunawapa habari za wiki mbili zilizopita kuishia jana ,yale yaliyotokea leo subirini wikimbili zijazo !" matukio ya mwezi mzima tutapewa cooked ,doctored ,concoted,fabricated summary ya nusu saa at most!janga kuuubwa hili!
 
Back
Top Bottom