JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Sep 7, 2013.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,105
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limevitaka vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), badala yake taarifa rasmi zitakuwa zikitolewa na jeshi hilo kila baada ya wiki mbili.

  Katazo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meja Erick Komba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo.

  Alisema hali hiyo inatokana na jeshi hilo kubaini kuwa baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaandika habari za uchochezi zinazotaka kuziingiza vitani nchi ya Tanzania na Rwanda.

  Meja Komba alisema hategemei kama kutakuwa na chombo chochote cha habari kitakachotoa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo bila kupata taarifa rasmi kutoka jeshi hilo.

  Alionya kuwa chombo chochote kitakachokwenda kinyume kitakuwa kina tatizo.
  Meja Komba alisema wananchi wanapaswa kuelezwa kuwa kikosi cha Tanzania kilichoko DRC ni sehemu ya Brigedia ya SADC, iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (Monusco).

  Alitaja majukumu ya kikosi hicho kuwa ni kuzuia waasi wa M23 na wengine kujitanua, kuvunja nguvu zao na kuyapokonya silaha makundi yote ya waasi.
  "Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Monusco, inamaanisha kuwa operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa," alisema.

  Aliongeza kuwa Tanzania haikupeleka kikosi chake DRC kwa ajili ya kupigana na M23, pia ieleweke kuwa haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo ambapo Rwanda ilitoa ridhaa kikosi cha Tanzania kwenda DRC.

  Meja Komba alisema Rwanda ni miongoni mwa wanachama wa nchi za Maziwa Makuu, ambayo imesaidia kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

  "Tanzania inashiriki katika operesheni hiyo ya ulinzi wa amani nchini DRC kutokana na mgogoro kati ya serikali na waasi hususan kikundi cha M23," alisema.
  Mgogoro huo ulianza Aprili mwaka jana, ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika jeshi la serikali na kuanzisha mapigano yaliyosababisha hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.

  Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Benard, amesema kuwa marais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda wamemaliza tofauti zilizokuwa zimejitokeza kati yao hivi karibuni.
  Marais hao walikutana na kufanya kikao cha faragha jijini Kampala nchini Uganda juzi baada ya mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na baadaye kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.

  Kuzorota kwa mahusiano kati ya viongozi hao kulikuja kufuatia kauli ya Rais Kikwete ya kumtaka Rais Kagame kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake vilivyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ushauri ulioonekana kumkera Rais Kagame.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Membe alisema marais hao walitumia mazungumzo yao yaliyochukua muda wa saa moja kujadiliana na kueleweshana mambo mbalimbali yaliyosababisha kutoelewana.
  "Baada ya mkutano huo ambao uliwapa fursa za kuchambua, kujadili na kurejesha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili, marais wetu walitoka na nyuso za furaha," alisema.

  Moja ya maazimio ya kikao chao ni kuwa na vikao vingine kati ya Rwanda na Tanzania katika siku zijazo.

  "Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali," alisema.

  Mbali ya kikao hicho pia Rais Kikwete alifanya kikao kingine cha faragha na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambapo walipata muda wa kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali kuhusu nchi zao na mambo ya migogoro katika nchi za Maziwa Makuu.

  Akizungumzia yale yaliyokubaliwa katika mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu, Membe alisema kuwa mkutano huo kwanza ulimruhusu Rais Museveni aendelee kusuluhisha vita ya serikali ya DRC na waasi.

  Alisema kuwa viongozi hao walilaani mashambulizi ya M23 yaliyojeruhi na kumuua Meja Mshindo wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa askari walioko nchini Congo katika kusimamia amani chini ya Umoja wa Mataifa.
   
 2. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2013
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,795
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
  Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
  Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.
   
 3. M

  MOSSAD II JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2013
  Joined: Apr 14, 2013
  Messages: 3,974
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hilo katazo ni kwa vyombo vya habari Tanzania tu? JWTZ iko chini ya majeshi ya UN, je na UN imetoa katazo kama hilo?
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,009
  Likes Received: 4,273
  Trophy Points: 280
  JWTZ wasitufanye wajinga labda niseme hivyo kwa ufupi.
   
 5. F

  Farudume JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2013
  Joined: Jan 10, 2013
  Messages: 3,918
  Likes Received: 2,916
  Trophy Points: 280
  Naunga Mkono Hoja.Kuna watu walikuwa wanashinikiza JWTZ ipige hadi Kigali bila kuainisha sababu za kufanya hivyo.Nashukuru JWTZ wameshtukia Janja ya hawa Wachumia Tumbo na Wauza Unga.
   
 6. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2013
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 14,387
  Likes Received: 2,531
  Trophy Points: 280
  Sa na hii habari yao isingeandikwa nani angejua?!
   
 7. j

  jacben90 Member

  #7
  Sep 7, 2013
  Joined: Jul 29, 2013
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yap yap kweli kabisa wanatuletea amri wakat ndugu zetu wako vitan kwa hiyo mtu akifa kule watatupa taarifa baada ya wiki mbili??? Ujinva gani huo??
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2013
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,198
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Unaambiwa jeshi lilijimega kutoka serikali ya Congo na kuwa waasi!!!!!!
  Halafu alishauriwa aondoe vikundi vya waasi wa nchi yake vilivyoko Congo!!!!!
   
 9. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2013
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jwtz wako sahihi kabisa, Magazet hasa Mtanzania lilikuwa na Agenda ya siri kuchochea ghasia labda bos wao nae ni Mdau katika biashara ya Silaha!
   
 10. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #10
  Sep 7, 2013
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,331
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  JF itakuwa excluded katika hilo katazo.
  Watatusamehe kwa hilo
   
 11. K

  Konya JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2013
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 918
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sidhani kama itasaidia, japo itawanyima fursa watanzania walio wengi kupata taarifa kwa wakati kwa yanayojiri huko DRC kwa sababu hata baadhi ya hivyo vyombo vya habari vya ndani vinategemea kupata hizo taarifa kutoka vyanzo vingine na vingi vikiwa vya nje, cha msingi nafikiri angetoa muongozo wa jinsi gani hizo habari ziandikwe ili kupunguza au kuacha kabisa upotoshaji wa baadhi ya hizo media
   
 12. f

  frank cain JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2013
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah. Kwahiyo tutegemee vyombo vya nje na internet tu?
   
 13. D

  Demarco JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2013
  Joined: Aug 3, 2013
  Messages: 553
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  what?
  Wakataze habari miaka hii
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2013
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 22,308
  Likes Received: 18,029
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hata vyombo vya habari vya kimataifa vikieleza habari za vita hiyo haitakiwi ku quote habari hiyo? Tanzania ina vichekesho kweli. Jee ametaja sheria iliyotumika kutoa katazo hilo? Magazeti ya Kenya,Uganda na hata ya nchi mbali mbali za Duniani yanakuja kila siku,jee yakiwa na habari za vita ya Congo yatazuiwa kuuzwa? Mitandao na Radio za nje jee nazo zitasubiri taarifa ya msemaji wa TPDF baada ya wiki mbili?
  Tamko hilo ni utata mwingine tena.
   
 15. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2013
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,005
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Utter nonsense!hili linchi!!mmmhhh.
   
 16. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2013
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 10,434
  Likes Received: 3,646
  Trophy Points: 280
  => Wht..? After 2 weeks ndio habari itoke...?? Huyu kilaza kweli....kaaahh....hivi hajui wanaishi kwa KODI ZETU...??
  what world is he living in...?? OMG...!!

  ==> We need infos DAILY & with updated development in DRC....huyu meja shuleless or..??
  heeee....!!!
   
 17. Msingida

  Msingida JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2013
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 3,436
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 180
  Kwenye article ya 'Human Rights" ambayo Tanzania imeridhia No. 19 na nukuu
  "Everyone has the right to freedom of thought,expression;this right includes freedom to hold opinion without interference and to seek,receive and impart information and ideas through any media and regardless of frontiers".
  Wanatafsiri vipi haki hii ya msingi ya kupata taarifa?
   
 18. Chinga One

  Chinga One JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2013
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 7,527
  Likes Received: 2,100
  Trophy Points: 280
  Hapa jf bado tutaendelea kupata news za moto moto.hao wa magazeti watajua wenyewe.
   
 19. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2013
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,448
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Mbona wanazungumza kama wao ndio UN, kwani wao ni mbwa kuwa hawana akili na utashi wakiambiwa 'SHIKA' wanaenda tu bila kuhoji? Yani maoni tu ya watu yanawafanya waweweseke? Ingekuwa TZ peke yao wapo kule hoja yao ingekuwa na nguvu kidogo lakini hapo hawakupima uzito wa hoja yao maana nchi zaidi ya moja zinashiriki kule nao vipi kwa upande wao?.
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2013
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,799
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  hivi hili ndilo suluhisho kweli?? ama kweli Tz bado sana
   
Loading...