JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Kaweke akili charge. Battery low.

Kwa hilo Boko ulilolitoa kama akili zako zingekua zinaCharge a bit......

America wasingekua na wale jamaa wa NAVY SEALS au MARINES ambao wao wanavunja nazi kwa ugoko.

Kacharge akili izo au battery haikai na chaji??????

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Mbona umehamaki sana . Vile wanayembea kwenye wanakata mauno viwanjani ndio jeshi
 
Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

MTU ANAAJIRIWA HADI KUSTAAFU HAJUI KUWASHA COMPUTER, HAKIKA KUNA SHIDA KUBWA SANA
Hiii kamba kaka kaivuta sana
 
Sikatai some time uko sawa.

Ila sasa ujiangalie Hali ya Uchumi wako pia ujue kufika kule sio rahisi ikiwa wewe ulie post tuu huna hata cha ajabu ulicho kifanyia Jamii.

Mabadiliko mapinduzi yananzia na kwako hapo ulipo.Sasa kama kila mtu anatumia mitandao kukosoa lihali yeye mhusika nae ni mzigo katika taifa letu kwakuto kugundua tuu jinsi ya kutengeneza battery ya simu tuu ya Nokia ya Tochi si mzigo huo.

Kuhudumia Meli makombora na ndege vita kwa Budget yetu bado ni ndogo.

Sasa wewe unapokuja na Na wazo njoo na scientifically solution na sio porojo na siasa.

mkulima halisi
Watu hawapendi kuambiwa tuwadhaifu pande hizo. Ukipita makambini walevi watupu hadi aibu yaani
 
Unawaza kama mimi na hakuna nimekuwa nikikidharau kama kuona wanaoitwa makomandoo wetu wakishindana kuvunja tofali pale taifa, na kuruka kwenye ndege kwa kutumia parachuti,
Unasema tu hiiiiiiiii unanyamaza. Vita leo hii ni sayansi tupu, vita kubwa haziganwi kwa SMG, AK 47 nk, leo hii watu wanacheza na computa Dude linakufata huko huko.
Vita ya bunduki ni kwa ajili ya kupambana na vikundu vya waasi lkn nchi kwa nchi taifa kwa taifa hatuhitaji askari wa kuvunja matofali kwa mikono wala kwa vichwa.
Unavyokiwazia chombo sivyo kabisa yani. Ningekwambia jambo ila najua utaniletea ubishi tu kuna integrated Air Defence System za maana najua huna unachokielewa.
 
Ukiwekeza kwenye teknologia jeshi la foot soldiers "milioni moja na malaki" la nini?
Jeshi la miguu kila nchi lipo( infantry solders) ni sehem ya kamandi ya jeshi.

Tuna kamandi ya jeshi la anga( Airforce)
Tuna kamandi ya jeshi la miguu( infantry)
Tuna kamand ya jeshi la maji( Navy)

Jeshi la miguu la miguu la miguu limegawanyika,

1. Mizinga
2. Vifaru
3. Askari wa miguu au ardhini.

Kwenye uwanja wa medani, hizo kamandi zinaweza kushirikiana kutegemea but inategemea .

Mfn.. Wakati askari wa miguu wanasonga mbele , kumfwata adaui alipo, nyuma , wazee wa mizinga watoa msaada , kumfurusha adui, huku jeshi la miguu la miguu linasonga , na vifaru..

Kikosi cha mizinga kinapokea frequency kutoka kwa captain, au yule msoma Raman, zile frequency ndio zinaonesha maadui walipo , kikosi cha mizinga kinatuma mzinga unaenda kutua pale pale kwenye point walio pewa ..ambako maadui wapo.. Sasa captain ataoe direction tofauti..

Kama kamandi ya anga au Navy wataitajika, wanaingia mzigoni.
 
Kwahyo jeshi lazima liwepo, bila kujali wapo kiasi gani .

Alafu haya mambo ya majeshi, yana usiri sana, RAIA kama ww sio lazima ujue power tuliyo nayo... .
 
Mi ntafurahi wakibadilisha hata zile adhabu zao kwa raia....
1. Kuna Dereva wa hiace alijitusu akaingia kambi ya Jeshi. Wakamwambia kwanza mchafu adhabu yake ikawa kuoga maji lita 1 na sabuni ile ya mia tano... sharti sabuni iishe, jamaa alikoma kuringa.

2. Mi nikiwa mdogo tulipita eneo lao tukapita krb na jiko lao tukiokota maembe wakatusimanisha wakatwambia nyie mnaonekana mna njaa. Wakapakua wali ndoo kubwa ile wakamimina na maharage wakatwambia mle huu wali hadi uishe Imagine tulikuwa 4.... awali tuliona jamaa wana upendo mkuu...baada tumeshiba wakatukazania tumalize uke wali aisee tulitoka matumbo yamechomoza kama tunaenda Labour.
Duuuh
 
Kaweke akili charge. Battery low.

Kwa hilo Boko ulilolitoa kama akili zako zingekua zinaCharge a bit......

America wasingekua na wale jamaa wa NAVY SEALS au MARINES ambao wao wanavunja nazi kwa ugoko.

Kacharge akili izo au battery haikai na chaji??????

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
huna akili kabisa ndg.
acha tukueleweshe. utendaji kazi wa navy seal wanapokuwa ktk operation zao, asilimia kubwa unakuwa supported na zana za kiteknolojia.

huko angani kuna satellite ambazo mmarekani kaziweka ziweze kumsaidia ktk kuspy activities za maadui ili kuwarahisisha kazi navy seal kuvamia ngome ya adui.

katika masuala ya medani, ukusanyaji wa taarifa wa aina hii hufahamika kama imagery intelligence na signals intelligence. kwa asilimia 100 unakuwa supported na zana za kisasa zilizoundwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

hoja ya mleta mada ina logic, usiibeze.
 
Kwahyo jeshi lazima liwepo, bila kujali wapo kiasi gani .

Alafu haya mambo ya majeshi, yana usiri sana, RAIA kama ww sio lazima ujue power tuliyo nayo... .
Sawa pamoja na usiri mambo ya jeshi, sote tulishuhudia jinsi jeshi la anga la marekani lilivyo
sambaratisha jeshi la miguu , kikosi cha vifaruu vya Saddam kwa kipindi kisichozidi miezi minne .Air power muhimu modern warfare. Chini ya miezi minne jeshi la footsoldier milioni moja hoi bin taaban .
 
Nilimsikia Kagame anataka kununua S-300 kutoka Russia
Hana hela hiyo, hana adui na wala hana jirani mwenye ndege za kupigwa na S-300 ambayo kwanza hawezi uziwa na Urusi wala hawezi ruhusiwa na US kuinunua.
 
Mleta mada uko very wrong kulinganisha nchi yenye defense budget ya $20 billion dhidi ya nchi yenye $1 billion na point. Bado hatulingani kwenye teknolojia na mambo kibao.

Hiyo Iron Dome unajua kuwa US ndio alifadhiri mradi huo, pamoja na ule mfumo mwingine mkubwa zaidi. Gharama za kufadhiri defense project ni kubwa mno Tanzania hatuwezi.

Kwanza nchi zote ununua silaha kulingana na uhitaji na maadui waliopo. Unanunua air defense nzito vile dhidi ya nani. Vipaumbele havioneshi kama tunahitaji air defense hata hiyo Israel ina silaha zinakoseana idadi kama submarines kwa vile sio kipaumbele na maadui wake hawapigwi kwa hizo wala hawatumii bahari kushambulia.

Nchi inayonunua panpasi na pedi nje ndio unataka itengeneze air defense system?
 
Pamoja na kwamba teknolojia ni muhimu, lakini bado tunahitaji askari wakakamavu.

Teknolojia ina mahala pake, na askari wana mahala pake.

Huwezi kuwa na jeshi la kutumia kompyuta tu. Unahitaji vijana wa kazi.

Halafu pia tunaangalia na mahitaji ya nchi pamoja na aina ya matishio ya kiusalama ambayo tunakabiliana nayo.

Sisi maadui zetu ni nani hasa? Hawa panya rodi na wajinga wajinga wa mpakani?

Ukishabaini aina ya matishio ya kiusalama tuliyonayo, utaona kwa kiasi kikubwa tunahitaji askari wakakamavu badala ya hizo kompyuta.

Bajeti ya nchi pia inazingatiwa. Hatuwezi kuacha kusambaza maji halafu turukie kununua teknolojia ambazo hazina matumizi ya msingi.

Tukombe bajeti yote tukanunue hiyo IRON DOME kwa ajili ya nani?
 
Mada hii imekaa Kidharau dharau dhidi ya Jeshi letu la wananchi.. wanakulinda wale Lakini ukiwa Umelala Usingizi na kuendelea na mambo yako kwa Amani.
Mambo yao mengi ni ya Siri.
Na ndo taratibu zao kiutendaji.
 
Back
Top Bottom