JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,252
34,200
Nimekua nikifuatilia vita ya Israel na Hamas huko ukanda wa gaza. Ninachoshangaa hamna ngumi wala kareti ni makombora yanavurumushwa angani kama mvua!

Hiyo ni moja, mbili..

Nimevutiwa jinsi Israel inavyotumia "engineering na science" kulinda nchi yake... kombora zinarushwa kutoka gaza ila zinazo tua ardhini chache sana kutokana na nguvu ya technolojia ya kulinda anga ya IRON DOME.

Yani kombora kabla halija tua lina maliziwa huko huko angani..

Sasa najiuliza hayo makombora yaliyo rushwa kwenda Israel na yakamalizwa kabla hayajatua ardhini je yangetua pale Magogoni au pale posta au pale kariakoo kuna Mtanzania hata mmoja angepona kweli?

Nadhani ni wakati sasa TISS na JWTZ wakaanza kuwekeza kwenye technolojia zaidi maana vita vya kisasa ni technolojia na sio mabavu!!

Unaweza pigwa na kanchi kadogo kisa tu kanatumia technolojia wakati wewe umewekeza kwenye mabavu na kuvunja matofali kwa kichwa!

Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

Ajirini vijana wenye IQ/Akili kubwa ili muwatumie katika technolojia na tafiti mbalimbali za kitechnolojia!!

Acheni kuangalia TBC kila saa washa Aljazeera mjifunze kichoendelea huko gaza na jinsi wenzetu wanavyowekeza kwenye technolojia!!

Zindukeni dunia imebadilika hii!!

Naomba kuwasilisha!
 
Kaweke akili charge. Battery low.

Kwa hilo Boko ulilolitoa kama akili zako zingekua zinaCharge a bit......

America wasingekua na wale jamaa wa NAVY SEALS au MARINES ambao wao wanavunja nazi kwa ugoko.

Kacharge akili izo au battery haikai na chaji??????

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Mbona kama umepanic mzee hahaaa imeingia hyoo
 
Kaweke akili charge. Battery low.

Kwa hilo Boko ulilolitoa kama akili zako zingekua zinaCharge a bit......

America wasingekua na wale jamaa wa NAVY SEALS au MARINES ambao wao wanavunja nazi kwa ugoko.

Kacharge akili izo au battery haikai na chaji??????

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu kwa maswahibu yanayo kukuta..
 
Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

MTU ANAAJIRIWA HADI KUSTAAFU HAJUI KUWASHA COMPUTER, HAKIKA KUNA SHIDA KUBWA SANA
 
Kazi ipo..!!
 
Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

MTU NAAJIRIWA HADI KUSTAAFU HAJUI KUWASHA COMPUTER, HAKIKA KUNA SHIDA KUBWA SANA
Ni kweli kabisa sema hatujaingia kwenye serious trouble na watu wenye modern weapons saizi ya Boko Haram nadhani tutaamka
 
Sikatai some time uko sawa.

Ila sasa ujiangalie Hali ya Uchumi wako pia ujue kufika kule sio rahisi ikiwa wewe ulie post tuu huna hata cha ajabu ulicho kifanyia Jamii.

Mabadiliko mapinduzi yananzia na kwako hapo ulipo.Sasa kama kila mtu anatumia mitandao kukosoa lihali yeye mhusika nae ni mzigo katika taifa letu kwakuto kugundua tuu jinsi ya kutengeneza battery ya simu tuu ya Nokia ya Tochi si mzigo huo.

Kuhudumia Meli makombora na ndege vita kwa Budget yetu bado ni ndogo.

Sasa wewe unapokuja na Na wazo njoo na scientifically solution na sio porojo na siasa.

mkulima halisi
 
Back
Top Bottom