NICK2275
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 3,931
- 918
tusiwe na mtazamo finyu wana jf, waislamu hawawezi kuunda mahakama ya kadhi bila kupata muafaka wa serikali na hasa wa kisheria kwa sababu tayari zipo sheria ambazo zinasimamia makosa ambayo mahakama ya kadhi inatakiwa kusimamia. Kama mahakama ya kadhi itatokea kuhukumu kesi ambayo sheria ya nchi nayo inahukumu tofauti huoni kutakuwa na mkanganyiko wa maamuzi. Vilevile kuwepo kwa mahakama ya kadhi kutahitaji kubadilishwa/kurekebishwa kwa vifungu vya sheria za mirathi na ndoa ili waislamu zisiwaguse. Haitajuzu kwa muislamu mmoja kutawaliwa na sheria za nchi halafu na tena sheria za kiislamu. Tujadili kwa busara
raisi ashatoa maamuzi-huu mjadala unatakiwa kufungwa