yes kwa kiasi fulani tumeanza kwenda pamoja mengine yanahitaji kuelimshana tu mfano ni Rahisi kwa mkristo kujigeuza mwislaamu kwa muda (aka act kama alivyofanya Mzee wetu kwani kwa imani yenu haina shida ingawa kwa imani yetu tunamuita mtu huyo mnafiki na kwa imani yetu mtu huyo akifa bila kutubia mahala pake motoni)
Mkuu naiona nia yako ya maridhiano ila kama ulivyosema kwa "uchungu",bado kuna element ya kutoaminiana kati yako na Wakristu.Well, sasa mtu kama mwalimu unayesema ameact akitubu kama ulivyosema atatubu kupitia dini gani ili asiende motoni?Je angebaki huko alipo bila kuact asingeenda motoni?
Ingawa siamini sana kama Mzee alikuwa an act au alikuwa kaiwasindikiza waislam.Ni mara nyingi Wakrsitu huwasindikiza waislam na wengin hujikuta wakiingia katk uislam kwa muda au kabisa.Kwa waislam pia wapo wahudhuriao maombi na kubadilika, wapo mabinti wapendao wanaume wa Kikristu tuu, wapo wapendao harusi za Kikristu tuu, na wapo waliozaliwa ktk usilam ila wanauchukia tuu bila kujua au kuwa na sababu nyingine na hivyo kujikuta wakiwasindikiza Wakristu katika matendo yao.
kwetu sisi waislamu siruhusiwi hata siku moja kuiga mila ya dini yako kwani imani yako inaamini mungu baba,mwana na roho mtakatifu kwetu tunaamini kua mungu ni mmoja hakuzaa wala kuzaliwa na hafanani na kitu chochote tofauti na hayo nahesabiwa kua namshirikisha mungu na mungu yupo tayari kusamehe dhambi zoote kasoro kumshirikisha au kumfanya anamsaidizi katika uungu wake.so nikijifanya mkristo leo nikatekeleza mojawapo katika ibada yako nimerutadi.
Naona umeamua iita dini yangu,sidhani kama mimi nina dini+Hata Ukristu si dini na unaitwa dini kwa vile hakuna neno mbadala la kuita mfumo wa imani usio wa kisiasa na utamaduni.
Well, kwa wale waaminio kwa kushawishika na mafundisho ya msingi ya imani fulani , basi huwa wamesoma Theology ya hii imani.Imani ya Utatu wa Mungu haimaanishi uwepo wa Miungu 3,ila uwepo wake.kuna vitu vingi sana vimeumbwa na Mungu vinaweza tokea kwa zaidi ya aina moja ya uhasilia wake.Sifa nyingine ya Mungu kuweza kuwepo kila mahali haipingani an ahii dhana,kwani kama anaweza kuwa kila mahalai na ni muweza wa yote, bado pia ni wazi huwekz kuwa chochote.Wengi wa wapingao utatu hawan asababu ya msingi kwanini Mungu hawezi zaa, na kwanini hastahili fanya haivyo.Mungu kama ana weka kila kitu na kuwepo kila mahali kwa mara moja sidhani kwanini ashindwe zaliwa bila toka Mbunguni?Theology ya Wakristu ni kwamba Yesu kuzaliwa haikuwa kuafafa na bindamu ili mwanadamu aabudiwe,ila kumwonyesha mwanadamu kuwa anaweza ishi bila kutenda dhambi na hivyo kuadhibiwa kwake na Mungu ni kwa haki.Bibli an Al-Quran zinaweka wazi hilo(Yesu hakuwa na dhambi).Kuhusu Utatu kwa wakristu kumaanisha miungu watatu lina matata ,kama ilivyo Mungu mmoja aktk Quran linavyoweza sumbua watu.Kila nisomapo Quran nakuta aya nyingi zikitumia neno "We,TU" na nyingine zinakuwa zinamtaja Muhamad.Wengi wa wasomaji huona kuwa Uislam una miungu wengi,kwani wakati mtu anaongea uumbaji halafu usikie anamquote Mungu akitumi "WE na si I",then its obvious kuwa anaongelea Mungu mwenzie na si Muhamad wala malaika kama ilivyo katika mistari mingine isiyotaja ""Uumbaji.Kwani hakuna Muumbaji mwingine zaidi ya Mungu na Neno Lake.Neno la mugu linaumba,Neno la Mungu hutenda.Yesu ni neno la Mungu.Kwani malaika alimwambia maria nimekuletea neno La Mungu.Na qurani inathibitisha kuwa Yesu aliumba.Na hapa hata wengine waiongezea kwa uwezo wa Mungu atajikuta akiingia ktk mchezo wa Kuku na yai.
Sidhani kama uislam unakukataza soma na kuamini Biblia au Torat,pengine hilo ni geni kwako.Ila ukisoma hivyo vitabu kuna Mengi unaamriwa kufanya ambavyo si kama uislam upendanvyo.Sidhani kama kutekeleza ibaya sahihi ya Kikritu ni dhambi hata kwa mtazamoa wa Kiislam.Otherwise Quan itakuwa imekosea inapowataka waislam kusoma vitabu vyote vilivyotangulia.
ndo kua mahala nilishauri kua yaliyopita tuyaache ushahidi wa mwl Nyerere kuwakwaza waislaamu kwa makusudi upo na yeye akiwa hai aliombwa ajibu hizi shutuma na marehemu DK Othman Harubu hakujibu mpaka anakufa. so Tujadli namna ya kusonga mbele kama watanzania tukiangalia vp kila jamii inaweza kusonga mbele hadi kufikia ustawi mzuuri bila kutumia kejeli au dharau na lugha nyingine ambazo sio nzuri.Nashauri hivyo nikiwa nina uzoefu wa kuishi katika nchi zenye migogoro ya Kidini kikabila tofauti ya kipato mgawanyo mbovu wa ardhi na mgawanyo mbovu wa pato la Taifa. mataizo yao unakuatat yana Historia ya miaka hata 80 nyuma hasa kadri watu wanavyo kaa nayo moyoni siku yakilipuka ni mtihani kaka yangu so nakushukuru unaonekana muelewa.
Ukiwa mtenda ahki utakubali kuna majibu si kwmba yanajibika au haiyajibiki ila jibu lolote utakalotoa litakuwa na matoke mabaya.Hapo watu wengi wenye bisara huamua yapotezea.Kwa kutoa uchambuzi wa dini nyingine kwa satili fulani inayohitaji kujadili hilo halafu unataka wengine waendelee ni kuwakwanza na kuonyesha kuwa bado hujafungua moyo wako na kuongelea issues kwa urais zaidi.Najua ni ngumu kujizuia ila kama hakuna tukanana ,wala tumia maneno ya kejeli na yasiyoonyesha ukomavu ,ni rahisi kila mtu akaeleze kwa nini anaamini kitu fulani na anachukia kitu fulani.
Kuhusu masuala ya imani si mara zote ushawishi unaweza mbadili mtu dini,kwani imani ni kitu kigumu sana,kwani imani ya mtu humtuma hata kufukia mabonde kwa vitu asivyovielewa au au hata kutopenda visema ingawa anajua kuwa hayupo sahihi.
Mimi bado naamini mtu kama wewe mwenye uchungu sana,ukiamua funguka na kufuatilia vitu kwa umakini unaweza elewa kuwa kuna mengine yalitokea kweli ila mwalimu hakusika kwa makusudi au hata kabisa.najua katk haya unaweza kuwa msaada mkubwa kwa mwaslam ,kwani unaweza wapa moyo wa kuendelea na si kubaki hapa walipoangukia miaka nenda rudi.NI mahali pa kujua waisilam wenye mafweza na elimu dunia kubwa wamefanya nini kwa ajili ya kuendeleza wengine.Mashikh matajiri walao fedha za misikiti na kuwa na familia zinazopeta kwa nasa nao wanahitaji kupata ushauri wenu ,kwa kuwaonyesh akuwa kuibia msikitini angalau kwa sheria zenu nini kinasemwa.