Justin Nyari ameanza mbio za kumrithi Lema Arusha

Nyari na Banjoo wameandikwa katika vitabu vya Historia ya Arusha kwa kuteka magari kule kikatiti na kingori na kuwaibia pamoja na kuuwa watu wasiokuwa na hatia. Wakijaribu tu kumleta huyu jambazi wajue imekula kwao kwani hakuna mwananchi aliyeko tayari kuona mji wa Arusha ukirejea tena katika ujambazi ambao pioneer wake alikuwa Nyari. Wahindi ndo hawatampa kura kabisa kwa sababu aliwapora wengi Tanzanite wakielekea kusafirisha airport.
 
Mkuu si alitakaswa na mahakama ya rufaa kama alivyotakaswa Rage.


Mkuu kwa magamba kila kitu kinawezekana
na wanaweza kusimama a kumtetea mpaka mapuvu yawatoke kuwa jamaa ni mtu safi mwenye nia ya maendeleo ya wanaarusha na hana hila wala sio fisadi
Na kwa nguvu zote wakamsema kuwa ile ilikuwa ni mbinu ya magwanda kumchafulia jina lake
yeye ni mtu safi na ana nia ya kuwaletea wanaarusha maendeleo
 
Justin Nyari alishafungwa kwa kosa la jinai. Haruhusiwi kugombea.

Kama alisha fungwa hilo ni swala lingine tena,ilikuwaje sasa wakampa kazi ya udiwani?

kwanza rufaa yenyewe nasikia itasikilizwa mwaka 2014 mwezi wa 12 tarehe 31 jioni.wakti huo tunajiandaa na uchaguzi mkuu
 
Nyari na Banjoo wameandikwa katika vitabu vya Historia ya Arusha kwa kuteka magari kule kikatiti na kingori na kuwaibia pamoja na kuuwa watu wasiokuwa na hatia. Wakijaribu tu kumleta huyu jambazi wajue imekula kwao kwani hakuna mwananchi aliyeko tayari kuona mji wa Arusha ukirejea tena katika ujambazi ambao pioneer wake alikuwa Nyari. Wahindi ndo hawatampa kura kabisa kwa sababu aliwapora wengi Tanzanite wakielekea kusafirisha airport.

Mbona Lema alikuwa jambazi mwizi wa magari na akapewa kura? Arusha mjini hawajali sana historia ya ujambazi wa mtu, muhimu kwao uwe chalii mwenzao tu.
 
Jambazi ni jambazi tu labda kama wangesema sasa ameokoka hapo anaweza kuaminika, laikini Mahakama kumtakasa mtu hiyo ni mpya kabisa

Duh mkuu umenifanya nicheke. Mimi nilikuwa naongelea suala la kupigwa marufuku kugombea ubunge kwa kuwa alifungwa kwa kosa la jinai! Ndio nikasema alishasafishwa na mahakama kama alivyofanyiwa Aden Rage.
 
Duh mmenikumbusha mbali kuhusu huyu jamaa Justin Nyari! Mara ya mwisho kupata habari zake japokua na mimi niko A.Town ni pale nilipoona matangazo barabarani yakidai wazazi wa Justin Nyari wanataka kuvunja Chungu kwa wale waliomsingizia kua mwanao ni jambazi! kwa hiyo wajitokeze kwenda kuomba msamaha! Sijui Chungu kilivunjwa?
 
Hivi nani alikuwa hakimu kiongozi kwenye mahakama ya rufaa na hivi sasa yuko wapi?

Mahakama yamwokoa kifungo miaka 30 mfanyabiashara maarufu Arusha
Na Mussa Juma, Arusha

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Arusha, Justine Nyari, ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na Makama ya Hakimu Mkazi Arusha, ameachiwa huru na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.


Mamia ya wakazi wa jijini Arusha, wakiwamo maafisa wa Usalama wa Taifa, polisi kawaida na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa katika magari mawili, jana walifurika katika viwanja vya Mahakama Kuu kusikiliza hukumu ya rufani hiyo.


Nyari kabla ya kutia hatiani, alikuwa ni mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamanda wa Vijana na wa CCM Wilaya ya Simanjiro, ilikuwa nadra kwa viongozi wa kitaifa kufika Arusha bila kuonana na Nyari.


Akisoma maamuzi ya rufani hiyo yaliyochukuwa saa matatu na nusu, kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:35, Jaji Othaman Chande wa mahakama hiyo, alisema amekubaliana na hoja za mawakili wa Nyari, Loom Ojare na Medium Mwale kuwa Nyari alikuwa hana hatia.

Kazi kwako.

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/5362-nyari-aachiwa-2.html
 
Nyari. alikichangia chama cha magamba pesa mingi sana. enzi Kapa alipokuwa madarakani na alikua anashirikiana sana na Ex IGP Mahita. Walikula pamoja madili ila mahita alimgeuka hakuamini.
 
Wanabodi. Habari kutoka Arusha zimemtaja mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Justin Nyari ambaye ni Diwani wa Kata ya Marerani ametajwa kuanza mikakati kuwania jimbo hilo. Kwa sasa anasubiri rufaa ya Lema...ameona ni bora kuanza sasa kuonesha nia ya kugombea ili mchakato ukifika iwe rahisi kupiga kampeni. CCM Arusha wanasema safari hii lazima waweke mtu makini mwenye ushawishi.
kwa hiyo wanataka kumuweka jambazi, haishangazi kwani ni sera zao
 
Wanabodi.

Habari kutoka Arusha zimemtaja mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Justin Nyari ambaye ni Diwani wa Kata ya Marerani ametajwa kuanza mikakati kuwania jimbo hilo.

Kwa sasa anasubiri rufaa ya Lema...ameona ni bora kuanza sasa kuonesha nia ya kugombea ili mchakato ukifika iwe rahisi kupiga kampeni.

CCM Arusha wanasema safari hii lazima waweke mtu makini mwenye ushawishi.

Nyari hana ushawishi wowote Arusha, na hata huko mirerani ambapo yeye ni diwani nimefanya kazi pale wanamlalamikia sana tena sana na wanajuta kumchagua. Pia jamaa ana kundi la uharifu balaa. pita mitaa yote Mirerani ulizia, kote Cairo, songambele, kilimahewa yaani hana alifanyalo

 
Mbona Lema alikuwa jambazi mwizi wa magari na akapewa kura? Arusha mjini hawajali sana historia ya ujambazi wa mtu, muhimu kwao uwe chalii mwenzao tu.

Mkuu wangu watu hawajui tu Lema na Nyari ni wamoja na deal zao zinafanana ndio maana hata siku moja huwezi kumsikia Lema akimsema vibaya Nyari kwenye majukwaa ya siasa.
 
kwa hiyo wanataka kumuweka jambazi, haishangazi kwani ni sera zao

Wakuu mnataka kutuambia kwamba Arusha ni mji wa majambazi? Manake Lema naye alishasemwa kuwa ni jambazi na huyu Nyari naye ni jambazi!

Bora wapambane hao hao wanatuhumiwa kwa ujambazi.
 
Nyari huyu mfuasi wa Lowasa???? Ambaye kifungo chake kilitenguliwa baada ya Lowasa kupata uwaziri mkuu???? Leo tena apewe Arusha c itakuwa nu sawa Lowasa ndiye mbunge wa Arusha mjini jamani ametesa watu na kuua raia wasio na hatia... Hivi hawa magamba wanadhani tunasahau kirahisi namna hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom