Arusha Leo
Senior Member
- Mar 12, 2012
- 122
- 72
CHAMA cha Mapinduzi ccm jimbo la Arusha mjini ,kimeanza mchakato wa kusaka
mgombea ubunge kijana mwenye uwezo wa kuchuana na mbunge wa sasa Godbles Lema,,baada ya kubainika kuwa
kuwa walioonyesha nia hadi sasa hakuna mwenye mvuto wa kumng'oa
waliooneysha nia hadi sasa niwazee.
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho jijini
hapa,baada ya kufanyika kikao cha siri kujadili wagombea wa chama
hicho walioonyesha nia,zimedai kuwa ni lazima chama kishawishi ili
kupata mgombea aliyebora.
''Ni kweli viongozi wamepeana mkakati wa kusaka mgombea kijana
,machachari mwenye mvuto kwa wananchi ambaye ataweza kupambana na Lema
''alisema kada maarufu ambaye alidai si msemeji wa chama.
Katibu wa wilaya ,Feruzi Benno alisema alikiri kuwepo kwa mkakati wa
kumng'oa Lema nafasi ya ubunge,ila alisema chama kinataratibu zake na
ni mapema sana kuianika hadharani kwani kwa sasa.
''Nikweli lazima tuwe na mgombea mwenye sifa anayekubalika na wananchi
na tunaangalia mahitaji ya wananchi wa Arusha ni nini ,kwa sasa tuna
taratibu zetu na si lazima kila mtu azijue ,tulieni wakati ukifika
mtaona''alisema Benno.
Habari za kuaminika zinadai kuwa tayari chama hicho kimeanza ushawishi
kwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini hapa,Thomas Munis
kikimtaka achukue fomu ya kuwania ubunge wakati ukifika.
Hata hivyo Munisi alikiri kufanya mazungumzo na makada wa chama hicho
na kuwaahidi kuwajibu baada ya kukaa chini na kufikiria.
''Nikweli baadhi ya viongozi walikuja na kiniomba nigombee ubunge
Arusha mjini ,ila kwa sasa nafikiria kwanza sikuweza kuwajibu moja kwa
moja si unajua mambo ya siasa yalivyo kuwa magumu ila nitawajibu
soon''alisema Munisi
Hadi sasa walionyesha nia ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama
hicho jimbo la Arusha mjini wamefika 9,akiwemo mfanyabiashara Philemon
Mollel , wakili wa kujitengemea Vicktas Njau,dkta Anold Andason ,Deo
Mtui na mtanzania mwenye asili ya kiasia aliyefanamika kwa jina la
Panju.