Mzee inaonekana unai-miss Jolly? Lol
Ndugu yangu kuna asiyekujua sokoni?..
Usifanye mchezo...heee heee heee!
Mikuki,
Very unfortunate indeed!..
Yet, it is possible...'cause ignorance and selfishness has always been ahead of traits of an effective leadership. I sometimes wonder if we do have good leaders at all...
Our leaders do not have vision, structure or values and they are not accountable for anything!. They can't communicate, see forces and ecosystem, sythesize viewpoints e.t.c on the other hand we do have the society which is driven by the force of evil.... MONEY! - Again, always wonder if we were/are fit to have Independence!...
Where to start - At those schools!... next time around thing will be different. Not this generation but self-fulfilling prophesy will come from these schools. A new generation of leadership...2nd time around Independence.
I do hope this is a lesson learned!
DAR si LAMU,
nadhani tunachosema ni kwamba mabadiliko yanaweza kuanzisha ktk hizi shule!...hapa hatutaki kufuga kizazi hiki ambacho kinaweza leta matokeo kama uliyoyasema. Ni kizazi ambacho wewe na mimi tumekulia.. Kwa hiyo kama kuna mabadiliko basi yaanzie katika shule zetu.... ndiko iwe mlengwa wa somo lolote tunalojadili humu.
Hao ndio watakuwa viongozi bora zaidi ikiwa mabadiliko yameanza kwao wao!
Wanafunzi wawapigwa marufuku kukutana
*Chuo chanyofoa matangazo ya wanafunzi
Na Waandishi Wetu
HALI katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Mlimani bado si shwari baada ya mgogoro kuibuka upya baaina ya wanafunzi na uongozi kuhusiana na hatua ya wanafunzi kutaka kufanya mkutano.
Mapema jana asubuhi, wanafunzi walibandika matangazo katika maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa ajili ya kufanya mkutano katika Ukumbi wa Nkurumah saa saba mchana, lakini ghafla uongozi wa chuo ulinyofoa matangazo ya wanafunzi na badala yake ukaweka mengine ambayo yalipiga marufuku wanafunzi kufanya mkutano.
Hali hiyo ilidhihirika jana baada ya uongozi wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso) kupinga amri ya utawala ya chuo na kusisitiza kwamba mkutano wao lazima ufanyike. Katika mkutano huo wanafunzi walipanga kuzungumza masuala kadha hasa ya wanafunzi 56 ambao wamezuia kurejea masomoni.
Pia walikuwa wanatarajia kuongelea hatua ya uongozi wa chuo kuwasainisha mkataba kwa wakili, ambao unawataka kutogoma tena. Katika maeneo ya chuo, wanafunzi walionekana wamejipanga katika makundi huku wakijadili masuala kadhaa yanayohusu kurejea kwao.
Kutokana na hali hiyo, hofu ya kuzuka mapambano baina ya askari wa FFU na wanafunzi imetanda miongoni mwa wanachuo wengi.
Makamu wa Rais wa Daruso, Bernadeta Rushahu, alisema baada ya kushikilia msimamo wa kufanya mkutano wao, amepokea ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi kutoka kwa mtu wa karibu yake serikalini kuwa askari wa FFU walikuwa njiani kwenda chuoni hapo kuwatawanya iwapo watafanya mkutano huo.
Amri hiyo ya UDSM iliyosainiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Makenya Makoko na kubandikwa katika ubao wa matangazo chuoni hapo imetolewa saa chache baada ya uongozi wa chuo kung'oa tangazo la Daruso lililokuwa limewataka wanafunzi kuhudhuria mkutano huo.
Katika hatua nyingine, barua walizoandikiwa wanafunzi 56 waliosimamishwa masomo na utawala wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) zikiwataka kukutana na Kamati ya Nidhamu ya Chuo hicho leo, zimebaini utata hali inayofumbua hoja kuhusu umakini katika uendeshaji wa chuo hicho.
Gazeti hili lina nakala ya moja ya barua hizo ikionyesha kuandikwa Mei 15, 2004, huku ikibainisha makosa ya wanafunzi hao kufanywa miaka minne baadaye yaani mwaka 2007.
"Kinachoonekana hapa ni hali ya mtu kuchukua barua za huko nyuma na kisha kuzichapa bila kutazama. Hali hii ni kukosa umakini hasa kwa taasisi kubwa kama hii," alisema mmoja wa wanafunzi waliokabidhiwa barua hizo na akaongeza;
"Inaonyesha walishajiandaa kutuhukumu na kama hivi ndivyo watuambie walikuwa na maana gani kutuandikia barua kuanzia mwaka huo na kisha kuzitoa sasa. Hali hii inaonyesha maamuzi ya kukurupuka," alisema
Katika barua hizo zenye makundi kadhaa, zipo ambazo zinatolewa nakala kwa Makamu Mkuu wa Chuo, huku zingine zikiwa hazina nakala kwa yeyote.
Kuna hali ya mashinikizo ya ndani na nje ya chuo ambayo yamesababisha Kamati hii kukaa mapema. Katika migomo iliyowahi kutokea huko nyuma, Kamati hii ilikuwa ikikutana baada ya muda fulani na wanafunzi wanaosimamishwa kurejeshwa chuoni kwa masharti ambayo hutoka kwa Makamu Mkuu wa chuo.
Kukaa kwa Kamati hii mapema kuna athari mbili. Moja ni kuwatoa katika kesi wale wanaoonekana kutohusika na pia baadhi yao kubakia kafara ya mgomo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alikaririwa na chombo kimoja cha habari akisema kuwa wanafunzi watakaobainika kutohusika na mgomo wataachwa huru.
Katika mgomo uliofanyika Aprili 15-16, 2007, kulikuwa na baraka za kisheria na kitaratibu kufuatia Bunge la wanafunzi kuuidhinisha. Kitendo hicho kilionyesha tayari kuwepo wahusika waliouhamasisha ambao ni viongozi wa wanafunzi kutokana na nguvu za uwakilishi wa wanafunzi wenzao.
Kutokana na utaratibu huo, kila aliyehusika alifanya hivyo kufuatia kubaini uhalali wa serikali ya wanafunzi Daruso kuwa na uwezo wa kuitisha mgomo.
Kama kutakuwa na kuathiriwa kwa baadhi ya wanafunzi, huenda kukawa na hali tete zaidi chuoni hapo. Kumekuwa tayari na taarifa za fujo chuoni hapo kufuatia kusimamishwa kwa wanafunzi hao 56 huku wakitakiwa kuanza mitihani ya mwisho ya semista wiki ijayo.
soko lenye deal ni mabibo hostel....upo hapo!
Hakuna kitu kinachoudhi kama ubabe wa serikali. Inasikitisha kuona kuwa katika Tanzania tunatikiwa kuinama na kupigwa bong'oa kwa vile serikali imesema jambo fulani. Katika suala hili la wanafunzi wa vyuo vikuu kufukuzwa na serikali kushikilia msimamo wake wa kuwataka walipe fedha za chuo kikuu, wakati umefika kuwaonesha serikali kuwa "nguvu iko kwa watu"!!
Nyinyi wanafunzi wa vyuo vikuu ambao mmekubali kuburuzwa na serikali na utawala wa vyuo kwa vile mnaona hamna njia nyingine nawasihi mtulizane na kutafakari upya. Mtaendelea kusukumwa sukumwa kwani baadaye wakiwaambia "tumeona mnaweza kulipa asilimia 40, sasa itabidi mlipie asilimia 60" mtakataa!! Ni lazima mchore mstari ardhini na kuiambia serikali kuwa hakisomeki kitu hadi suala hili la malipo linatafutiwa ufumbuzi once and for all!!
It is about time to put your feet on the ground and don't you dare move! Viongozi wa Daruso na wengine wenye maslahi nawashaurini mfanye kile ambacho hufanywa mara nyingi kwenye nchi za kidemokrasia, siyo maandamano na mabango bali kukaa chini (Sit Ins)
a. Wanafunzi wote rudini vyuoni kwenu kwa makundi (siyo mtu mmoja mmoja) Mkishikilia mabango yasemayo yenye kuhamasisha serikali kuwaruhusu wote kurudi shuleni na kukabili tatizo zima la kulipia elimu ya juu. Mmekubali kugawanywa, hamuwezi kufika mbali! La maana wale walioruhusiwa kurudi wagome kurudi hadi wenzao wote nao wamerudi!
b. Jifungeni vitambaa midomoni (ishara ya kunyamazishwa!). Na mnaweza kuvaa nguo nyeusi kuonesha msiba mkubwa wa elimu ya juu Tanzania.
c. Nendeni na kukaa kwenye maeneo ya vyuo (hasa kwenye milango ya madarasa) na msiondoke hadi muondolewe kwa nguvu huku kamera zinaroll na picha zinapigwa ili kuionesha serikali mbele ya umma!
Mbinu hii ya kukaa chini, imetumiwa tangu wakati wa Mahtma Gandhi, na wakati wa kutafuta haki za raia kule Marekani. NI mbinu ambayo haina uchokozaji kwa serikali. Lengo kubwa la kutumia mbinu ni hii ni kulazimisha hoja ya watu isikilizwe na kuonesha hadhara kubwa kuwa kutotumia nguvu kwaweza kujibiwa kwa matumizi ya nguvu. Nina uhakika mkiamua kukaa chini kwenye milango na viwanja vya vyuo vyetu, watawaleta polisi na kuwasomea "Riot Act".. msibabaike, wala msikimbie, kaeni chini kama watawabeba na kuwapeleka kwenye makarandinga wawabebeni... mtazijaza mahakama, na jela, lakini wakati wa kuchukua msimamo umefika... woga wenu ndio umewaponza hadi hivi sasa!!
Wanafunzi wenzenu kwenye vyuo vikuu vingi duniani ndio wamekuwa chachu ya mabadiliko.. katika kupiga vita Ubaguzi wa Rangi Afrika ya Kusini, Sera ya Utenganisho wa Rangi huko Marekani, Vita vya Vietnam, kule Ujerumani mwaka 1968 n.k
There comes a point in a relationship between the State and the People when the people have to take a stand. Hili suala la kulipia asilimia 40 ni wakati kama huo, na watanzania tuwaunge mkono kuhakikisha kuwa vijana wetu wanarudi shuleni bila kubaguliwa kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha!! Lengo la "kukaa chini" ni kuhakikisha Msolla anaondolewa na bodi ya Mikopo inavunjwa ili apatikane Waziri mpya na Bodi mpya yenye uwezo wa kukabiliana na matatizo ya elimu ya juu na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu!
let there be a showdown.. yes, this looming showdown between the state and unarmed, peaceful body of students!! Let the Kikwete's government take a stand and make a choice!!
Siku zote elimu inatanguliwa na IMANI....hata katika dini zetu kwanza unatakiwa Kuamini ambayo ina misingi yake kisha Elimu ambayop inakuonyesha jinsi ya kufanya Ibada. Tupo wengi sana wenye elimu hiyo iwe ya dini ama elimu dunia isipokuwa tumekosa Imani. Katika dini hawamwogopi MUNGU na katika serikali zetu hawaogopi SHERIA...
NI bora sana kuwa na waumini wasiokuwa na elimu lakini wana imani kuliko kuwa na wasomi wasiokuwa na imani. Hii ndiyo Tanzania ya leo, Tanzania ambayo inatanguliza mahitaji yake mbele ya imani.
Kwa hiyo labda wapo waliokwisha kata tamaa ya pepo na hivyo the ONLY way for them (ubinafsi huo) ni pepo ya hapa duniani... FEDHA!