DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 561
Mniwie radhi, najaribu kuamua kama niweke sasa hivi, mida ya usiku au mapema kesho kwani tukio na kile ambacho nataka niwaambie kitatokea Alhamisi... Nafikiri itakuwa ni too early to break the news kwani nikiweka sasa hivi, serikali will act tomorrow na kuvuruga mipango ya Alhamisi...
Mniwie radhi, najaribu kuamua kama niweke sasa hivi, mida ya usiku au mapema kesho kwani tukio na kile ambacho nataka niwaambie kitatokea Alhamisi... Nafikiri itakuwa ni too early to break the news kwani nikiweka sasa hivi, serikali will act tomorrow na kuvuruga mipango ya Alhamisi...
Dar si Lamu,
Eeeeh mwenzetu wee ni mwanamama?... maanake majibu yako kidogo yameniacha nje kuwa wajua kwa nini wanafunzi wa vyuo vyetu wanajiuza.
Ama ndio Dar sii Lamu kweli?..
Sikiliza ndugu yangu kutembea na wanaume wengi kama starehe ni umalaya ambao unatokana na hulka ya mtu lakini mwanamke wa chuoni anapo UZA mwili wake kama biashara ya kusukuma maisha hili ni swala zito zaidi ya unavyofikiria wewe....Unless una hoja nyingineyo zaidi ya kuwashusha dada zetu kwa mtazamo wako.
Ni kweli Umalaya ulikuwepo toka zamani lakini umalaya huo haukuwa kwa wanafunzi kujiuza miili yao ila moja ya starehe zao...Walikuwa wakitoka majumbani mwao kwenda sehemu za starehe tena wengine watoto wa hawa vigogo lakini kutembea na mtu ilikuwa ni ktk starehe yao..Haikuwa na malipo zaidi ya chicken n Chips pale Mermaid!
Pili, sitegemei kabisa kwamba wewe mwanaume unaweza kunipa sababu zinahusu hisia za kike ktk swala hili. Na iweje leo iwe umalaya huu kwa wasichana wanaosoma vyuo vikuu wakati sikumbuki kuwepo kwa hulka kama hii miaka ya zamani.
Nitafurahi zaidi ikiwa kuna mwanamke humu ambaye anaweza kunambia kuhusu wimbi hili la wasichana kuuza miili yao kwa madai ya kutafuta Ada ya chuo anachosoma.
Pili, ndugu Dar hata huku nje UGENINI, wasichana wetu wengi wanajisomesha na kuna kila haja ya wao kupenda anasa zaidi ya huko nyumbani maanake vishawishi ni vingi zaidi, kila kitu kipo madukani kwa daraja tofauti.
Lakini hata hivyo wengi wao wameweza kutafuta njia nyingine nje ya kuuza miili yao, wakifanya kazi mbuzi kabisa ambazo wewe hapo Bongo huwezi kuzifanya wala kumshauri mtu kufanya. Na wameweza kulipa ada ya shule.. Wanaofanya umalaya kwa starehe wanafahamika na haihusiani kabisa na utafutaji wa karo ya shule...
why did yoy tell us in the first place? watu presha hiyo!
mwanasiasa... I was too excited... then I thought suala la time difference na advantage ambayo serikali itakuwa nayo... so.. I'm holding back for few hours, kwani for now I'm the only one who could break that news...!!! Unless serikali wa ni preempty... otherwise...
Dar si Lamu,
mengine wayaongeza mwenyewe maanake umesema unafahamu kwa uhakika kwa nini wanawake wanauza miili yao. Hili ni swala la maamuzi ya mtu na hata kisayansi sio rahisi kwa mwanamke kufahamu kwa nini mwanamme ni malaya! Hakuna hakika zaidi toka nje unless wewe ni mmoja wao. Huo ndio ukweli na yatubidi kuukubali....hatuzungumzii imani za dini hapa.
Sasa ikiwa hao wanawake wanafanya Umalaya kwa sababu kuendekeza maisha ya anasa na kutaka kuishi maisha wasiyoyaweza au ya kuiga!. Ni maisha gani hayo?.. bia wanapewa bure, kwenda club wanaume wanatoa offer na wengine wapo radhi kununua magari ikiwa mtoto wa kike ataweza kujiheshimu. Na wengi wamefanikisha maisha hayo nje ya vyuo... tatizo langu kubwa ni hili wimbi la wasichana wa shule kuweka NIPE - NIKUPE mbele ya starehe hizo hizo unazozizungumzia. Na ukitazama maisha yao hawana starehe hata kidogo labda ungepata muda ukakaa nao na kuwahoji kuhusu swala hili.
Dar si lamu,
Nimefanya hivyo, nimekaa na baadhi ya wasichana na kuwauliza kwa undani zaidi kuhusu maisha yao vyuoni na niamini naposema hawafanyi haya kwa kupenda anasa. Hii ni hukumu ya kiume mbele ya wanawake na wala sikujaribu.. hajaribiwi mtu isipokuwa hoja kujibiwa kwa hoja! Kilichotangulia ni lugha ya Dar ama Lamu ambayo kama unavyosema wewe sii tusi wala kumjaribu mtu. Nipe source ya madai yako utakuwa umerahisisha zaidi....
Tanzanianjema,
Haya ndio maneno nayoyazungumza humu wala usije fikiria nawalaumu hawa dada zetu ila system nzima. Tumelivaa soko huria kama vile soko la Kariakoo ambalo halina viwango ktk kila kinachopokelewa maadam somo linasema huu ni wakati wa biashara.
Hao wanaohusika na madangulo haya ni mafisi ambao kamwe hatuwezi kuwazungumzia ikiwa sisi wenyewe tumesababisha kuwepo kwa mizoga!...hakuna mizoga fisi hawana nafasi ila huko mwituni -Joly club!
Kinachosikitisha zaidi ni pale serikali inapohesabu ukubwa wa jeshi kama la Saadam ktk Elimu kutangaza mafanikio hali jeshi dogo kama la Israel (Botswana) linatutoa kapa.... Hii ni dalili mbaya sana ya viongozi wetu kutofahamu umuhimu wa elimu bora ktk nchi maskini. Asilimia kubwa ya wanafunzi nchini inatoka ktk familia ambazo pato lake kwa siku ni chini ya dollar moja!..Na maisha ya wenzetu hasa nchi za magharibi hayawezi kuigwa wala kufananishwa na sisi hata kidogo kwa sababu wana uwezo wa kujisomesha. Maskini tuna malengo yetu na hao Matajiri wana malengo yao na wala hoja hii haiondoi hoja ya kuwepo kwa shule za private!.
Tunakokwenda sisi ndiko wao walikotoka na kamwe haitatokea tairi la gari la nyuma kulikamata la mbele...labda tu gari hili limeharibika!..Siku Tanzania itakapo weza tengeneza hata baiskeli yake basi jua magari yatakuwa yakiruka hewani huko Ulaya..
Nitaiomba serikali yetu ijaribu kufikiria upya elimu nchini na hasa sehemu muhimu kama vyuo vyetu ambako ndiko tunakotegemea zaidi ktk ufanisi wa kila hatua ya maendeleo yetu. Kilio cha wanafunzi hakikutoka bure na hakikuanza jana. Tena basi moja ya mikakati ya serikali ni kufuta umaskini jambo ambalo huwezi kulimaliza kirahisi ikiwa fedha itakuwa msingi wa kumaliza umaskini huo!..
Maskini husaidiwa kupunguza uzito wa mzigo na sio kuongezewa mzigo.