Serikali inayotumia mabavu inaweza ikawakalia wanafunzi shingoni na wasiweze kabisa kufanya chochote. Chini ya serikali ya Mao Tse Tung, kwenye miaka ya 70, mitihani na digrii viliondoloewa kwenye vyuo vikuu, na wanafunzi hawakuweza kupinga.
Serikali ya sasa ya CCM inatumia nguvu za jeshi la polisi kukandamiza wanafunzi. Inatumia vile vile wasomi wakandamizaji kama VC wa UDSM, kudhalimu wanafunzi, na kuzorotesha uhuru wa Watanzania kwa ujumla.
Kwa upande mwingine, wanafunzi wanavuna walichopanda. Wamekuwa hawamwangalii JK kwa akili. Amewadanganya mengi, nao wakawa wanamshangilia tu kama vile mtu anavyoshangilia mpira.
Wanafunzi wamepata somo la nguvu. Kuanzia hapa, watakuwa na mtizamo wa kukaa na kufikiria ni nini kinasemwa na watawala. Hawatashangilia tena bila kufikiri. Hata VC wao watakuwa wamemwona kwa ukweli kwamba anaweza kulishauri Baraza la Chuo liwatimue na kuwapa muda kidogo tu wa kuondoka, bila huruma. Na wanawaona sasa wasivyojali kabisa umasikini wao. It is a very hard lesson. The guys in their Admin Building are not "in loco parentis". They are their persecutors.
Wananchi wanapashwa kushirikiana na kuibana serikali iwarudishe wanafunzi wote, na iwape mikopo kwa asilimia 100. Fedha zipo. Makusanyo ya TRA ya mwezi 1 (260bn/-) ni zaidi ya mara tatu ya fedha ambazo serikali inatakiwa iongeze ili wanafunzi wote wapate mikopo ya kwa silimia 100.