jumatatu.j'nne....hadi j'pili zilitungwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jumatatu.j'nne....hadi j'pili zilitungwa na nani?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by elf miaka, Nov 24, 2011.

 1. e

  elf miaka Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari!hivi hizi j'tatu-j'pili zilitungwa na nani na zina maana gani?mana naona kama kuna majina ya watu kwenye hizo siku mfano juma,tatu,pili,ali,hamisi n.k.vile vile kwa kiingereza monday-sunday.
  Vile vile hawa kina january-december walitokea wapi kwa ujumla?
  Nisaidie unachofahamu kwa manufaa ya wengi.
   
 2. B

  Bijou JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  kwanza wewe utuambie, efumiaka ilitoka wapi?????????????
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  swali zuri, hebu wajuzi tujuzeni ili nasi tupate kujua...
   
 4. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Topic: jumatatu.j'nne....hadi
  j'pili zilitungwa na nani?
  Na wanadamu.
   
 5. e

  elf miaka Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bijou elf miaka ilitokana na jamaa alinambia miaka elfu moja kwa Mungu ni siku moja.alinambia ataniambia imeandikwa wapi ila sjamfatilia.
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine tuyaache kama yalivyo..
   
 7. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu sio vibaya kuuliza
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  ujue ni nini mkuu, mambo mengine yanatia hasira. Wazungu wamekaa chini wametupangia mifumo ya maisha na sisi tumeikubali.
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Juma ni neno linalomaanisha kujumuika linalotokana na Kiarabu Juma'a ambayo ni siku ya Ijumaa (Ijmaa) kukusanyika, kumbuka Waislam hukusanyika (Ijmaa) miskitini siku moja kwa wiki ili kuelezana mambo yaliyojiri kwa juma zima katika jamii na baada ya Imamu kuelezea Khutba (Hotuba) ya Ijumaa humalizia kwa kuswali Rakaa mbili za pamoja. Kumbuka, siku zote zingine sala za mchana huswaliwa Rakaa nne lakini siku hii zile rakaa mbili hufidiwa na ile Khutba ya kukusanyika (Ijmaa).

  Juma = wiki
  Mosi = ni kiswahili safi kikimaanisha "first". Kwa hiyo Jumamosi ni siku ya kwanza baada ya Ijmaa (Ijumaa).
  Pili = ni kiswahili safi kikimaanisha "second" Kwa hiyo Jumapili ni siku ya pili baada ya Ijmaa (Ijumaa).
  Tatu = ni kiswahili safi kikimaanisha "third" Kwa hiyo Jumatatu ni siku ya tatu baada ya Ijmaa (Ijumaa).
  Nne = ni kiswahili safi kikimaanisha "fourth" Kwa hiyo Jumanne ni siku ya nne baada ya Ijmaa (Ijumaa).
  Tano = ni kiswahili safi kikimaanisha "fifth" Kwa hiyo Jumatanoi ni siku ya tano baada ya Ijmaa (Ijumaa).
  Alhamis = ni neno la kiarabu linalomaanisha "fifth day" (Al Khamis). Kumbuka siku za kiswahili mosi huanza Jumamosi, siku za Kiarabu Mosi huanza Jumapili (Youm 'l Ahad) Ahad ni "first" kwa Kiarabu ambayo tayari ni siku ya pili ya Kiswahili.

  Neno au jina Ali halipo kabisa katika hizo siku kama uonavyo kwenye hizo siku kuna "Al" na si Ali.

  Majina ya Juma kuwa jina la mtu inawezekama kabisa huyo mtu alizaliwa siku ya Ijumaa na Waarabu wanalo hilo jina wao huliita Juma'a kama ujuavyo Kiswahili kinafanyiwa kila njia kuzitowa zile lafdhi za Kiarabu na ndio linabaki kuwa Juma na si Juma'a ki uhalisia wake inatakiwa liwe Juma'a na si Juma.

  Hayo majina ya Pili, Tatu na Khamis (linauliwa na Hamisi) ni kuwa huyo ni mtoto wa Pili (second), Tatu (Third) na wa Tano (Khamis). Lakini kwa kuwa yameshakuwa majina na pengine yawe yamerithiwa kwa babu au bibi au Mjomba au ndugu au rafiki na huwa hayafati sana kuzaliwa kwa mtu, yaani inawezekana kabisa kuwa Tatu si mtoto wa Tatu bali alipewa hilo jina kwa kuwa shangazi yake anaitwa Tatu.

  Nadhani umeelewa haya ya Kiswahili kabla hatujaanza na hayo ya Kiingereza? kama una swali lolote kuhusu hayo usisite kuuliza.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe 100% kuuliza si ujinga ni kuelimika.
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  FaizaFoxy, nimekusoma!
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  bibie Faiza Foxy umenilog in na hayo mafundisho yako hapo juu,ubarikiwe sana. Nalog off
   
 13. e

  elf miaka Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante faiza,kwa kifupi nmeelewa kwamba hizi siku mizizi yake iko kwenye kiarabu au yako kiislamu zaidi.nmeona kwenye kitabu cha neno la Mungu cha kikrsto kimeandika siku ya kwanza,ya pili...mpaka ya saba sasa nkapata wasiwasi kuhusu uwepo wa jumatatu hadi jumapili.vilevile kwenye miezi nikajitahidi kutizama januari mpaka desemba sikuona ndiko maswali yakaanza kuja kichwani.haya mambo si ya kudharau kwasababu ukiambiwa ndege yako inaondoka saa nane mchana ukafika saa nane usiku hujaachwa?so tunapozungumzia majira ambazo ndo izi siku na miezi iliyopewa majina tuwe na taadhari ya kujifunza.faiza endelea kutujuza zaidi kama kwenye quraan labda wameandikaje na mengineyo.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Mmmh! Ngoja niingie library.
   
 15. e

  elf miaka Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kongosho ingia kwa kweli mana kuna dakika,saa,siku,mwezi hadi mwaka wa kila tukio iwe nila kufa au kuzaliwa au kupata pesa.sasa tusipojua haya majina majina chimbuko lake nahisi ndo tunadondokea kwenye majira ya mitego mibaya.yani unakuwa km umewekewa fence flani.information is power.elimu haina mwisho si unajua.
   
 16. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Miezi kwenye bible;
  Abibu,zivu,siwan,tamuz,abu,eluli,ethanim,buli,kisleu,thebet,shebath,Adari
   
 17. e

  elf miaka Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh marejesho naomba reference ya hayo majina nikajisomee.kwa hiyo kwenye hicho kitabu hakuna januari mpaka desemba?unafahamu zilitoka wapi na maana zake?

  JF elimu tosha kwa kweli
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Elf Miaka,nakumbuka ni kitabu cha Mwanzo mistari ntakupatia baadae kwani bible iko mbali kidogo!Hakuna January to December bali ni aina ya wazungu tu kutuweka sawa!!Kwa wanaosali kanisa la Siloam,wamekuwa wakifundisha sana kuhusu siku na miezi!
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kumbuka kwanza wakurusedi wa mwanzo (Vasco Da Gama na wenzake) walipoingia pwani ya bahari ya hindi walikuta kuna mji (Kilwa uliyo kuwa umeendelea kwa wakati huo kuliko hata miji ya kwao walikotoka, walikuta watu wanavaa mpaka hariri wakati kwao walikuwa hawaijuwi, walikuta watu wanapaka rangi za nyumba wakati kwao walikuwa hawazijuwi, walikuta watu wanatumia kauri za Kichina (China ware) wakati kwao walikuwa hawazijuwi, walikuta watu wanatumia sarafu za dhahabu kwa biashara zao na pia wakakuta watu hao ni Waislaam na wanaendesha mji wao Kiislaam.

  Kwa hiyo usishangae hizi siku zimekaa Kiislaam sana kwani hapa kwetu Uislaam ulikuwepo kabla ya Ukristo na pia Uswahili unahusishwa na Uislaam, maneno mengi ya Kiswahili yanatokana na Kiarabu ambacho ni lugha ya Qur'an kwa hiyo usishangae ukiyakuta ya Kiislam mengi kwenye Kiswahili.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kwanza nikupe huu muujiza wa hizi siku, miezi, na juma kwenye Qur'an, halafu mengine tutaendelea:

  • Neno Mwezi "month" (shahr) linatajwa mara 12.
  • Neno Siku (uwingi wa Siku au Kipindi) "days" (ayyam,yawmayn) linatajwa mara 30.
  • Neno Siku "day" (yawm) linatajwa mara 365.
  • Neno Sabbath (Siku ya Saba ya Juma) linatajwa mara 7.
   
Loading...