Wakulima wa chai na parachichi Rungwe ni wakati wa kuifufua Tukuyu Stars

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Safari ya Tukuyu Stars na Isuzu Lao

20840821_1548063948583344_1018719444387863332_n.jpg

-Kikosi cha Tukuyu Stars, timu iliyopanda daraja mwaka 1985, katika kituo cha Shinyanga na kuja kucheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara wakati huo na kuchukua ubingwa kwa kupoteza mechi tatu tu.

-Mwaka huo wa kupanda daraja wa 1985, Tukuyu Stars hadi wanaondoka Shinyanga, kwa Lori la mmiliki wa timu yao, hawakuwa wamejua kuwa wamepanda daraja nafikiri ilitokana kufungana kwa pointi na timu mojawapo katika kituo cha Shinyanga huku wakiacha mechi moja ikichezwa kati ya timu moja ya Shinyanga na nyingine huku wao wakiwa wamemaliza mechi zao na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

-Matokeo ya mechi waliyoiacha yalikuja tofauti na wao walipata habari za kupanda kwao daraja kupitia kipindi cha michezo cha Redio Tanzania Dar es salaam wakiwa njiani maeneo ya Manyoni. Kwa furaha ya kupanda timu mmiliki wa timu hiyo aliyekuwa na duka kubwa maeneo ya Bagamaoyo, Tukuyu, Ramnik Patel aka Kaka aliendesha lori hilo la Isuzu yeye mwenyewe kutoka Manyoni, Singida hadi mjini Tukuyu.

Pichani ni majina ya kikosi hicho katika picha hii iliyopigwa uwanja wa zamani wa Taifa, sasa Uhuru mwaka huo wa 1986:

-Kutoka kushoto waliosimama
Kevin Haule(marehemu), Zitto Kiaratu, Karabi Mrisho, Godwin Aswile, Ali Kimwaga, Anayefutia nimemsahau, Kipa Mbwana Makatta, Kocha Athumani Juma Kalomba nambari nne wa zamani wa timu ya Simba(marehemu), Na mmiliki wa timu Ramnik Patel aka "Kaka".

-Waliochuchumaa
Golikipa nimemsahau, Anayefuatia Richard Lumumba (marehemu), Yusuf Kamba huyu alikuwa mwajiriwa wa NBC, Suleiman Mathew Luwongo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi siku hizi, John Alex, Daniel Chundu na mwisho ni Aston Pardon (marehemu).

-Hiki ni kikosi cha mwanzo cha dhahabu cha Banyambala kabla ya ujio wa nyota wengine baadaye kama kina Justin Nicodemus Mtekere, Augustino Sanga, Salumu Kabunda, John Moses Kanyiki na wengine wengi.

-Tukuyu Stars kama nilivyosema walipoteza mechi tatu tu zote wakifungwa bao 1-0 na RTC Kagera kule Kaitaba, kisha kwa Pamba ya Mwanza pale Kirumba halafu na kwa Simba Sports Club katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya bao la Edward Chumila baada ya pasi ya faulo kutoka kwa Ramadhani Lenny, aliyekuwa ameangalia Sokomatola, halafu akatoa pasi Mwanjelwa, Chumila akautokea na kuujaza wavuni akiwaacha mabeki wa Tukuyu wamezubaa.

Faulo hiyo ilitokana na Suleiman Mathew Luwongo kumkwatua kipande cha mtu Zuberi Magoha nje kidogo ya kumi na nane.

Simba ililipa kisasi kwani katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam, Simba ililala kwa mabao 2-1 kama watani zao Yanga pia walilala uwanja wa Uhuru kwa idadi hiyo ya mabao kutoka kwa Richard Lumumba na Yusuf Kamba na katika pambano la marudiano katika uwanja wa Sokoine Yanga wakalala tena safari hii kwa bao 1-0 bao la kona ya moja kwa moja kutoka kwa beki nambari tatu wa Tukuyu Stars kijana mpole na mkimya Daniel Chundu.

Siku hizi kabla ligi haijaanza bingwa tayari keshajulikana na timu za hapa mjini zikiwa zinaondoka pale stendi ya mkoa Ubungo kwenda mikoani tayari zinakuwa na matokeo yao mifukoni. Zamani ulikuwa huwezi kujua nani atashinda katika uwanja wowote ule. CREDIT: Golosoo Sports

MY TAKE
Kwa kuzingatia kazi nzuri, ari na mapenzi makubwa ya wanaTukuyu, wanaRungwe, wanaMbeya na wanaNyanda za Juu Kusini, pamoja na watanzania wote.

Vilevile, kwa kuzingatia kuwa Wilaya za Rungwe, Kyela na Halmashauri za Busokelo na Ileje zina uwezo wa kifedha kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi na kilimo zinazofanyika huku (chai, parachichi, gesi ya vinywaji TOL, kakao, makaa ya mawe Kiwira, mahindi, utalii na samaki wa Nyasa n.k.), na kwa kuendeleza kazi nzuri ya familia ya Patel, na kwa kuzingatia uwezo wa soka wa vijana wengi wa Juu Kusini (rejea Mzize), ni wakati sasa Tukuyu Stars ifufuliwe na idhaminiwe na taasisi za kiuchumi kama kampuni za majani chai, TOL, kampuni za parachichi n.k, inahitaji kurudi ligi kuu Tanzania Bara.

Hatua hii itaongeza ushindani wa Ligi Kuu ya Tanzania na kuongeza fursa za kiuchumi ikizingatiwa kwamba mpira ni ajira tena kubwa tuu.

20840821_1548063948583344_1018719444387863332_n.jpg

Kikosi cha Tukuyu Stars enzi hizo
- Kutoka kushoto waliosimama
Kevin Haule(marehemu), Zitto Kiaratu, Karabi Mrisho, Godwin Aswile, Ali Kimwaga, Anayefutia nimemsahau, Kipa Mbwana Makatta, Kocha Athumani Juma Kalomba nambari nne wa zamani wa timu ya Simba(marehemu), Na mmiliki wa timu Ramnik Patel aka "Kaka".

- Waliochuchumaa
Golikipa nimemsahau, Anayefuatia Richard Lumumba (marehemu), Yusuf Kamba huyu alikuwa mwajiriwa wa NBC, Suleiman Mathew Luwongo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi siku hizi, John Alex, Daniel Chundu na mwisho ni Aston Pardon (marehemu).

- Hiki ni kikosi cha mwanzo cha dhahabu cha Banyambala kabla ya ujio wa nyota wengine baadaye kama kina Justin Nicodemus Mtekere, Augustino Sanga, Salumu Kabunda, John Moses Kanyiki na wengine wengi.
 
Watu waliokuwa na mchango kwenye hii timu ni Yule Muhindi kaka (IRP)

Pia mzee mwaikela, mwaiseje (Irp)

Nadhani tangu wameondoka akina

Ivoh Mapunda
Shadrack nsajigwa.
Godfer Bonny (mwandaje)
Jofrey katepe.

Wengine nimewasahau nilikuwa mdogo sana
Kabla ya uwanJa wa mpira wa Ccm tukuyu mjini kuwa maduka na stand.

Home sweert home.
 
Uyu kaka banyambala aliwekaza mpaka kwenye magari miaka ya 2000 nimemsikia na kiyaona magari yake itakuwa alifirisika.
 
Watu waliokuwa na mchango kwenye hii timu ni Yule Muhindi kaka (IRP)

Pia mzee mwaikela, mwaiseje (Irp)

Nadhani tangu wameondoka akina

Ivoh Mapunda
Shadrack nsajigwa.
Godfer Bonny (mwandaje)
Jofrey katepe.

Wengine nimewasahau nilikuwa mdogo sana
Kabla ya uwanJa wa mpira wa Ccm tukuyu mjini kuwa maduka na stand.

Home sweert home.
Kuna timu za mchangani zinaubonda sana Lwangwa kule. Usajili makini na Uwekezaji kwenye uwanja nakadhalika unaweza kuirudisha Tukuyu kwenye ramani ya mpira. Nimewaza Glazer angeenda akawekeze kule maana ana uwekezaji wake kwenye mithai
Uyu kaka banyambala aliwekaza mpaka kwenye magari miaka ya 2000 nimemsikia na kiyaona magari yake itakuwa alifirisika.
Injinia tunazungumzia söka we unazungumzia mkandaji
 
Jamaa walikuwa wanatembeza gozi sio Kitoto na walikuwa na mapafu sana anasimulia Chuma wa Mbeya...Unaambiwa Simba na Yanga zilikuwa chamtoto mbele ya Hawa miamba
Kuna Timu nyingine ilikuwa inaitwa Mecco ya hapo hapo Mbeya Mjini. Jamaa walikuwa na mapafu ya mbwa walikuwa wanacheza hata dakika 180. Simba na Yanga zilikomeshwa sana na hao jamaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom