Msanii Black wa Uswazi

Feb 6, 2024
40
54
BLACK WA USWAZI .
_____________________

Hatimaye leo tumefanikiwa kumpata mmoja Kati ya wachonga barabara kwenye Tasnia hii ya Muziki wa Bongo Fleva ambao juhudi zao ndio zimefanya Muziki Huu kuwa Hapa ulipo .

Kuna changamoto nyingi sana wamepitia wachonga barabara hawa Enzi Hizo ili kuumpa Heshima Muziki Huu wa Bongo Fleva

Muziki Ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ni sehemu ya Ajila kwa vijana wengi ambao wameamua kufanya Muziki kama sehemu ya kujiingizia kipato ( Ajila)

Wakongwe hawa walijitoa kwa hali na mali ili kulifanikisha hilo nadhani wadau wengi wa Muziki wanalitambua jambo hilo .. wakongwe hawa walifanya mambo yote hayo pasipo kuangalia faida & Hasara / gharama watakazotumia kufanikisha jambo Hilo..

Wadau wengi wa Muziki wanataja jina Hili la "Bongo Fleva" pasipo kufahamu ni kina nani ambao juhudi zao zilitumika kufanikisha mambo yote haya ambayo yanaonekana lakini hasa ni matunda yanaonekana kwenye Muziki kwa Sasa..

Na huyu si mwingine ni msanii anajulikana kwa jina la kisanii kama "Black wa uswazi"

Hatatueleza kuhusu Historia ya Maisha yake kwa ujumla lakini sisi kama wana " ukwaju wa kitambo " tutajikita zaidi kuzungumza nae kuhusu Maisha yake katika tasnia hii ya Muziki wa Bongo Fleva..

Ukwaju wa kitambo:

Wadau wengi wa Muziki tunakufahamu kwa jina la kisanii "black wa uswazi" wadau wa Muziki Wanashahuku ya kufahamu "black wa uswazi" ni nani na Harakati za Muziki ulianza lini..

Black wa uswazi

Kwanye upande wa Muziki mimi safari yangu ilianza mwaka 1998 Enzi Hizo nikiwa shuleni..

lakini wakati huo huo shuleni nilikuwa nacheza mchezo Aina ya "Baisket Ball" ๐Ÿ€ majina yangu kamili tukiachana na Hili la kisanii ambalo wanalifahamu watu wengi la "black wa uswazi" mimi naitwa "Felician pongo"
Kwa jina jingine ni "kulwa" maana nina pacha wangu ambae nilizaliwa nae siku moja.

Ukwaju wa kitambo:

"Vip kwa kipindi hicho Baada ya kumaliza shule ulijiunga na crew yoyote ya Muziki au ulikuwa kama solo arts" ukaendelea na Game ya Bongo Fleva..

Black wa uswazi:

"Tulikuwa na kundi letu moja linajulikana kwa jina la " family Crew" ambalo liliundwa na pacha wangu na jamaa mmoja rafiki yangu anaitwa "dazdari " pamoja na mimi kundi ambalo mimi ndio nilikuwa kama kiongozi wao , maana nilitoa msaada mkubwa sana katika kundi Hili la Muziki hasa kwenye upande wa kuandika lycris ( uandishi wa mashairi) tulikuwa tunafanya Hizi movement kwenye mtaa wa kigamboni jijini Dar es Salaam, kulikuwa na chuo cha sanaa kinaitwa "YICC" na fire pale mtaa wa kariakoo kwenye chuo hicho hicho cha "YICC" cha sanaa kuna project nyingi tulifanya kwa producer mikka Mwamba lakini hatukufanikiwa kupeleka nyimbo Hizo ๐Ÿ“ป "radioni"
Na kwenye media yoyote ile sio television ๐Ÿ“บ wala ๐Ÿ“ป radioni

Ngoma zote tulifanya kwa producer mikka Mwamba list ya nyimbo Hizo ni :

1. Mfanyakazi
2. dada huyua
3. nipe mic

Gharama za kurekondi nyimbo studio kwa producer mikka Mwamba Enzi Hizo ilikuwa ni tsh 30,000/= . Tulifanikiwa kulipia nyimbo mbili ( 2) tu..

na Nyimbo ya Tatu mikka Mwamba alitufanyia for free kama kutukaribisha kwenye Game ya Bongo Fleva..

Nakumbuka pia wakati ule nilifanya Tukio fulani hivi ambalo siwezi kusahau katika maisha yangu ..

Nakumbuka nilichukua kiasi fulani cha Fedha kwenye sehemu anapohifadhi Fedha zake za Akiba ..
mama Yangu mzazi ili tupate fedha kwaajili ya kulipia Hizo nyimbo studio .. kwa nyakati zile pia wazazi wangu walikuwa hawataki kabisa mimi nifanye Muziki walijitahidi sana kunishauri ni focus kwenye Elimu zaidi na sio kufuatilia mambo ya Muziki ...

Dah Enzi Hizo pale home kulitokea Bonge la kesi kwa Sababu ya lile tukio nililofanya lakini namshukuru Mungu nilifanya kitu kimoja nilikwenda studio nikachukua nyimbo zangu kwa producer mikka Mwamba na Baadae nikaja kumsikilizisha mama nyimbo Hizo tukiwa wote nyumbani.

Mwanzoni kabla ajasikia nyimbo zangu Marehemu mama Yangu alikuwa amekasirika sana lakini Baada ya kusikiliza nyimbo Hizo alisema "

nachukua hela ndani naacha hata kununua vitu vya msingi kama vitu kama vile madaftari na amua kupeleka Fedha studio kweli.. alisikitika sana..

Lakini nilimuomba msamaha kisha Marehemu mama Yangu alinisamehe na akanipa Baraka zote kama mzazi kwa mwanae..

Ndio maana waswahili husema ( nani kama mama)

namshukuru sana mama kwa kunipa Baraka zote kama mzazi . Thanks mum..

Enzi Hizo nakumbuka Muziki ulikuwa hauna hata hela kabisa show moja tulikuwa tunafanya kwa shilingi laki moja tu ..kiukweli pia kuhusu inshu ya "wadosi" wahindi mimi sikufanya nao kabisa Kazi ( sikuwapelekea nyimbo zangu kwaajili ya usambazaji) maana mimi nyimbo zangu sikuwahi kupeleka kwenye media yoyote ila mimi na Adam juma tulikuwa tunafanya video tu.. lakini mimi nimejulikana sana hasa ni kwaajili ya video tu

Lakini mwaka 2002 ndio nikaingia studio na kuachia Ngoma inaitwa "sema ooh ๐Ÿ˜ฒ" nadhani nyimbo hii ilileta taswira mpya katika safari yangu ya Muziki Hapa nilikuwa kama solo artist Baada ya crew yetu ya Mwanzo kabisa iliyojulikana kwa jina la "family Crew" kuvunjika kwa Sababu za Hapa na pale na changamoto Katika Muziki zilikuwa nyingi Enzi Hizo nahisi ndio kilikuwa ni chanzo cha kundi letu kuvunjika.

Lakini hiyo Ngoma inayoitwa "sema ooh " ilileta taswira mpya katika safari yangu ya Muziki ambapo mimi na Adamu juma tulikuja na idea ya kuanzisha crew inayoitwa "uswazi"

Ambao tulikuwa mimi

๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ Jelly
๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ A.T
๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ J.i

Kwa kifupi tulikuwa tunataka crew ya "uswazi" iwe kama chuo fulani hivi cha sanaa.. ili tuwe tunatoa Elimu kuhusu michezo mbalimbali kama Baisket , mpira nk...

Tulifanya nao project kadhaa tukiwa kama crew ila mwisho wa siku malengo yakashindwa kutimia na kila msanii alipita njia yake.

Siunajua Tena Muziki kibongo Bongo

Ila kwa kifupi crew ya uswazi tulianzisha mimi na Adamu Juma.

Mtu aliyeni inspire kufanya Muziki kwa wakati ule walikuwa wasanii wengi kutokea nchini Marekani wasanii kama vile :

๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ Mc hammer
๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ Snoop doggy
๐Ÿ‘‰๐Ÿฟ Robert kelly

Watu hawa ndio walini inspire sana na kunifanya nitamani kuwa msanii kama wao makundi kama naughty by nature..

Na sisi Enzi Hizo tulifanya mazoezi ya kurap kupitia zile beat zao tukawa tunajirekodi kwenye vijiredio

๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ
Ukwaju wa kitambo:

Vip kibongo kuna msanii ambaye alikuwa anakuumiza kichwa sana na ukawa unatamani kufanya nae collabo

Black wa uswazi:

Mmm kwa kipindi kile hakuna alioniumizaga kichwa mana wote tulikua wakali kwaiyo lazima mtu ufanye kweli !

Ukwaju wa kitambo :

Ukiachana na producer mikka Mwamba ni producer Gani mwingine Enzi Hizo ulifanya nae Kazi..

Lakini samahani kwa kukurudisha nyuma ww ni mzaliwa wa mkoa Gani..

Vip ulikwisha wahi kutoa Album. Vip crew ya uswazi kuna vijana inawaandaa kwa sasa au kila mmoja ana fight kivyake kuachana na hao wasanii kama At , jelly na j.i. ambao wanafight kama solo artist

Black wa uswazi:

Wasanii karibuni wote wa zamani walikua hawana mkataba ..mnakubaliana kwa maneno๐Ÿ˜„

Ndo Maana wengi walikuwa wanadhurumiwa na pa kwenda huna

Kwa Sasa kila mtu ana pambana kivyake Kama solo artist
Na kuhusu kabila baba alikuwa mpogoro .mama baba yake alikua mkaburu !!
Kwenye upande wa Album sijawaigi kutoa
Nimezaliwa hapa Hapa jijini Dar es salaam maeneo ya aghakhan
Lakini kwa sasa mimi " black wa uswazi" nina project nyingi na bado narecord ! Soon nitaanza kutoa ngoma Kuna Mambo nayaweka vizuri kwanza..

๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

Wewe mdau wa Muziki una jambo lipi la kumshauri "black wa uswazi".

Jah๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

Team mond mara Team kiba & konde Gang nk..

Sometimes kabla hamtaja record label Hizo kumbukeni pia wakongwe hawa...

"Ndio maana professor jay anakuambia " born town kitambo mtanieleza Enzi wengi wenu hamjafika mjini "

Kwahiyo tuwape Heshima inayostahili wasanii wakongwe bila chonyo sio kisa hawasikiki ndio kiwe chanzo cha kutokuheshimiwa"

Afande SELE anasema " simba mzee lakini bado meno makali , ...

๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
 

Attachments

  • FB_IMG_1709977250753.jpg
    FB_IMG_1709977250753.jpg
    24 KB · Views: 12

Similar Discussions

Back
Top Bottom