GE2025 Jumaa Aweso aibuka kidedea kura za Maoni ubunge Jimbo la Pangani

GE2025 Jumaa Aweso aibuka kidedea kura za Maoni ubunge Jimbo la Pangani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mtia nia wa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Pangani mkoani Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumaa Aweso, ameibuka mshindi kwa kishindo katika kura za maoni zilizofanyika jimboni humo baada ya kupata kura zote za ndiyo katika kata zote zilizopiga kura.

Aweso amepitishwa na wajumbe wote wa CCM kwa kupata asilimia 100 ya kura dhidi ya wapinzani wake wawili waliokuwa wakichuana naye katika mchakato huo wa ndani ya chama, ambao hata hivyo hawakuambulia kura hata moja. Katika taarifa aliyoiweka kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aweso amewashukuru wajumbe kwa imani waliyoionyesha kwake akisema: “Asanteni Wajumbe wa CCM Pangani kwa kura zote za ndiyo... Imani hii mlionipa nitailipa kwa matendo.

” Matokeo ya awali ya kura za maoni katika kata zote 14 zilizoshiriki yanaonesha kuwa Jumaa Aweso alipata kura zote, huku wapinzani wake Ramadhan Zuberi na Mariam Abdallah wakitoka kapa kata hadi kata. Kata kama Pangani Magharibi, Kipumbwi, Mikinguni, Mkwaja, Mwera na nyinginezo zilionesha uungwaji mkono wa hali ya juu kwa Aweso, ambaye ni Waziri wa Maji katika serikali ya awamu ya sita.
993527609.jpg
 
Mmmh inakuaje kata zote mtu asipate hata kura moja ? Ina maana hata wapambe wao hawakuwapigia kura?
 
Hongera nyingi zimuendee mganga wake kwa kucheza kibibgwa ! 📢📢😆
Mwambieni Aweso kuna maeneo Dar hayana maji kwa hio uwaziri wake wa Maji bado una gepu kubwa sana maana hajamaliza kero
 
Juma Awesu the bilingual beast, anatema yai zaidi ya Wakazi Swagga Bovu.
 
Inapigwa Tanzania
Alimdanganya Mama Eti Mwakitori Wachawi Mpaka Mabomba Ya Maji Yanapaa Usiku
 
Mbunge wa Jimbo la Pangani aliyemaliza muda wake, Jumaa Aweso, ameibuka kidedea katika matokeo ya awali ya kura za maoni ndani ya chama cha Mapinduzi kwa ushindi wa kishindo, akipata kura 3,806 kati ya kata 14 za jimbo hilo.

Katika uchaguzi huo wa ndani ya chama, ambao ni hatua ya kuchuja majina ya wagombea wanaotaka kugombea ubunge kupitia chama hicho kwa uchaguzi mkuu ujao, Jumaa Aweso aliwashinda kwa mbali wagombea wenzake wawili – Ramadhan Zuberi na Mariam Abdalah – ambao hawakupata kura hata moja katika kata yoyote.

Kura za maoni zilifanyika katika kata zote 14 za Jimbo la Pangani, zikiwemo Pangani Magharibi, Mwera, Mkalamo, Kipumbwi, na Mkwaja. Aweso alionekana kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wajumbe, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kuridhika kwa wanachama juu ya utendaji wake katika nafasi ya ubunge na uwaziri.

Kata ya Pangani Magharibi ndiyo iliongoza kwa kumpa kura nyingi zaidi — 489 — ikifuatiwa na Kipumbwi yenye 414.

Hii inaashiria nguvu ya Aweso katika maeneo ya pwani na yale yenye changamoto za upatikanaji wa maji, sekta ambayo ameiongoza kwa muda mrefu.

Chanzo: Manara TV
 
Kpi za Waziri ni nini?
Kpi za mbunge ni nini?

ndani ya mitaa ya Kabul - Afghanistan.
 
Mmmh inakuaje kata zote mtu asipate hata kura moja ? Ina maana hata wapambe wao hawakuwapigia kura?
Hii inashangaza,kwamba hata ndugu zao hawakuwapigia kura?
 
Mmmh inakuaje kata zote mtu asipate hata kura moja ? Ina maana hata wapambe wao hawakuwapigia kura?
Hao wote walio rudi nao aliwachukulia fomu ssa inataka apate mpinzani wa kutoka wapi wote wake mkuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom