Juliana Shonza ni hatari kuliko tunavyodhani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,933
2,817
Wakuu nimekuwa nikifuatilia mtiririko wa matukio tangu kuibuliwa kwa hoja ya masalia hadi kufukuzwa na hatimaye kufikia hatua ya kuhamia chama tawala baadhi ya masalia akiwepo Juliana na Mwampamba.

Kuibuka kwa ile hoja ni jambo ambalo japo lilijadiliwa sana, chanzo chake ni tata. Waliohamia CCM ni wawili; Juliana na Mtela lakini anayesikika zaidi ni huyu dada. Awali alisema yeye bado ni BAVICHA na hautambui utenguzi uliofanyika. Mara tukasikia yuko CCM na kapokelewa na Rais! Akiwa yeye na mwenzake. Mara anatoa kauli kuwa yeye ni mzawa wa Ubungo na yuko tayari kupambana na Mnyika.

Niseme tu kwamba kazi aliyotumwa sio kwamba ameikamilisha. Ndio kwanza inaanza. Huyu ni Delila. Ni mzuri wa sura na umbo lakini ana akili ya nyoka.

CHADEMA itambue yafuatayo;
1. Safari ya Juliana kuzunguka Tanzania nzima kueneza sumu dhidi ya CHADEMA ndio imeanza.
2. Juliana ni hatari kuliko Mwigulu na Nape.
3. Juliana ana hasira za kweli (japo ni kwa upuuzi wake) juu ya CHADEMA na viongozi wake.
4. Juliana atakachoomba toka CCM kwa ajili ya kuikandamiza CHADEMA atapewa. Kumbuka huyu ni Delila.
5. Watu watavutika kumsikiliza huyu binti kwa kuwa ni mwanamke na ana mvuto. Atajenga huruma kwa wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau.
6. Kwa bahati mbaya kila atakachosema sasa na baadaye kitakuwa habari, hivyo athari yake si ndogo.

CHADEMA watambue sasa kuwa hawajaondoa tatizo bali wamezaa tatizo. Wamezaa si kwa kosa lao bali wakati mwingine inatokea tu. Wajipange katika kudhibiti athari zitakazotokana na kauli za huyu msichana.

Historia isijeandikwa kupitia sumu ya huyu mtoto na kamwe asipuuzwe. Harakati zake kipindi cha masalia na PM7 dhidi ya CHADEMA zinajulikana, nazo zilikuwa za faragha na ziliathiri chama. Sasa hizi za hadharani nazo zikipuuzwa si balaa?
 
Mi naona mnamkuza bure tu huyu, kama yeye ni mzawa wa Ubungo, wenzie sisi sio tu wazawa, bali ni waasisi wa Ubungo, yeye ameikuta kwasababu labda kazaliwa hapa lakini yeye si zaidi ya sisi tulioiasisi ubungo. Yeye kakuta ubungo tayari kumeshajengwa barabara nne, sie enzi zile huku ubungo ni mashamba tu ya mikoroshi, huko kimara ilikuwa ni pori tu. walokuwa wanathubutu kufika Kimara walikuwa wanaishia kunyonywa damu na mumiani, sasa huyo dada asitubabaishe na uzawa wake. Atueleze kwa uzawa wake amechangia nini katika maendeleo ya Ubungo?? Aache kubwabwaja. Halafu na sie naona tunakuwa wajinga kama yeye kwasababu tunam[andisha sana chati kwa kumjadili. Tumuache aende kwa amani kwa magamba wenzake huko ndo kunamfaa. Buriani Dada Shombo
 
Tatizo mkuu SHONZA anajulikana tu humu JF na kwenye baadhi ya watu walio wafuatiliji wazuri wa siasa....Inabidi kwanza kujitambulisha yeye ni nani katika kupambana kwake na CDM...

Pili mitaani unapoipondea CHADEMA na DR SLAA believe me wananchi hawakuelewi...Ana kazi kubwa sana ya kufanya hili....

Tatu watanzania wameshaichoka CCM..hata akifufuka NYERERE leo na kuanza kuipigia chepuo CCM itabidi afanye kazi ya ziada...
 
1. Safari ya Juliana kuzunguka Tanzania nzima kueneza sumu dhidi ya chadema ndio imeanza.
2. Juliana ni hatari kuliko Mwigulu na Nape.
3. Juliana ana hasira za kweli (japo ni kwa upuuzi wake) juu ya cdm na viongozi wake.
4. Juliana atakachoomba toka ccm kwa ajili ya kuikandamiza cdm atapewa. Kumbuka huyu ni Delila.
5. Watu watavutika kumsikiliza huyu binti kwa kuwa ni mwanamke na ana mvuto. Atajenga huruma kwa wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau.
6. Kwa bahati mbaya kila atakachosema sasa na baadaye kitakuwa habari, hivyo athari yake si ndogo.

Tunamkaribisha sana ulingoni!... Unacholinganisha ni sawa na kumchukua BONDIA FRANCIS CHEKA wa MOROGORO na kumpambanisha na mwanafunzi wa DARASA la tatu, kisha ukamtisha CHEKA ukamwambia LEO UTAPIGWA!... Haitatokea SHONZA akawa tishio kamwe!... Ingekuwa hivyo Lamwai na kabourou wangeua upinzani!
 
Juliana Shonza ni SUMU kwa CHADEMA.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kuwepo na kutokuwepo kwake chadema naona sawa tu. huu mwezi ukiisha naye ataisha yaani ndo mwisho wa kumsikia. mia
 
Juliana hana uwezo huo , kuitetea CCM siyo kazi rahisi , ni sawa na kumtetea shetani ndani ya nyumba ya Mungu ! Kuna maswali machache sana ambayo tumemuandalia huyo Masalia atakapopanda kwenye jukwaa la Nape , hatoweza kuyajibu , na ndiyo utakuwa mwisho wake .
 
....Ni mzuri wa sura na umbo....
mkuu Raia Fulani unaniangusha bana, ana uzuri gani aisee? hujawahi kuona mabinti waliopo CCM wewe, kuna mabinti ni wazuri balaa, yaani inasikitisha kuwaona wapo CCM, ni warembo kinoma lakini bado hawasikilizwi kwenye majukwaa sembuse huyo kipori shonza?
kule kwetu Lushoto binti kama Shonza tunamuita kinukachupi kichamba na umande.
 
Last edited by a moderator:
Yah angalizo zuri, hasa ukizingatia siasa zetu za kutengeneza upepo magazetini na vyombo vya habari njaa basi lolote linawezekana.

Ila kitu kimoja mkuu RF pamoja na yote hayo dawa ya huyu mtoto ambaye ana amini katika siasa za social media pekee dawa yake ni kumpotezea kwenye hizi corridor, pia ikumbukwe ye ni wa ngazi za BAVICHA tu hana hadhi ya makao makuu.
Tuombe uzima utaiona siasa yake inavyopotea ndani ya CCM kabla hata hyo 2014 haijaisha
 
Naona ume mpamba bure huyo mtupu! Hana uwezo wa kupambana na chadema ndio maana alidhibitiwa! Mimi kwangu huyu ni kichwa maji!
 
Back
Top Bottom