Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza tarehe 04 Julai, 2023 alishiriki Baraza la UWT Wilaya ya Songwe ambapo alichangia Mifuko 50 ya Cement yenye thamani ya Shilingi Milioni Moja kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Songwe
Mhe. Shonza alielezea utekelezaji wa Ilani ya CCM awamu ya sita pamoja na mpango kazi wake ambapo amesema tarehe 07 Julai, 2023 anatarajia kuanza ziara rasmi kutembelea vikundi vya wanawake wajasiriamali katika Kata za Mkoa wa Songwe.
Mhe. Shonza amesema Barabara ya kutoka Mbarizi mpaka Mkwajuni mwaka huu wa fedha imewekwa kwenye bajeti mpya ambapo ujenzi utaanza kwani kimekuwa ni kilio cha muda mrefu sana na Wabunge walikuwa wanaomba kwa muda mwingi
Mhe. Shonza amemshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songwe ambayo imekamilika na ipo hatua za mwisho kuanza kazi kwani itasaidia kupunguza vifo vya mama na watoto katika Wilaya ya Songwe
Mhe. Shonza amesema Wilaya ya Songwe sasa imepata miradi mingi sana ya Maji ambayo itasiadia kutatua changamoto ya upatikanaji wa Maji
Mhe. Shonza ameishukuru Serikali kwa utowaji na ugawaji wa leseni za Uchimbaji Madini katika eneo la Ngwala ambapo wachimbaji wametengeneza barabara ambayo ilikuwa haipitiki ambapo sasa inapitika kirahisi kwa wananchi na Wafanyakazi wa mgodi
Mwisho, Mhe. Juliana Shonza ametoa ratiba ya ziara na mikutano ya hadhara anayotarajia kuifanya katika Jimbo la Songwe ambayo itaanza tarehe 07 Julai, 2023 ambapo ataongea na wananchi na kusikiliza kero zao.